Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ezekieli

Ezekieli 30

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Neno la Yahwe likanijia, kusema,
2“Mwanadamu, toa unabii na sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Maombolezo. “Ole unakuja siku hiyo.”
3siku ikaribu. Siku ikaribu kwa ajili ya Yahwe. Itakuwa siku ya mawingu, mda wa hukumu kwa ajili ya mataifa.
4Kisha upanga utakuja dhidi ya Misri, na huko kutakuwa na maumivu makali katika Kushi wakati wauaji wa watu watakapoanguka katika Misri-wakati watakapochukua utajiri, na wakati misingi yake itakapoharibiwa.
5Kushi, Putu, na Ludi, na wageni wote, pamoja na watu wa nyumba ya agano-wote wataanguka chini kwa upanga.
6Yahwe asema hivi: Basi wale wanaoisaidia Misri wataanguka, na kiburi cha uweza wake kitashuka chini. Kutoka Migdoli hata Sewene maaskari wao wataanguka kwa upanga-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
7Wataogofya kati ya nchi zilizotupwa, na miji yao itakuwa miongoni mwa miji yote iliharibika.
8Kisha watajua kwamba mimi ni Yahwe, nitakapouweka moto katika Misri, na wakati wasaidizi wake wote watakapoharibiwa.
9Katika siku hiyo wajumbe watatoka mbele yangu katika meli ili kuitia hofu Kushi iliyo salama, na kutakuwa na maumivu makali miongoni mwao katika siku ya kuangamizwa Misri. Kwa kuwa tazama! inakuja.
10Bwana Yahwe asema hivi: Nitaufanya mwisho wa watu wa Misri kwa mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli.
11Yeye na jeshi lake pamoja naye, hofu ya mataifa, italetwa kuiharibu nchi; watafuta panga zao juu ya Misri na kuijaza nchi pamoja na watu waliokufa.
12Nitaifanya mito kuwa nchi kavu, na nitaiuza nchi kwenye mkono wa watu waovu. Nitaifanya nchi na viijazavyo ukiwa kwa mkono wa wageni-mimi, Yahwe, nimesema.
13Bwana Yahwe asema hivi: Nitaziharibu sanamu, na nitaleta mwisho wa sanamu za ubatili za Nofu. Hakutakuwa na mkuu katika Misri, na nitaweka hofu katika nchi ya Misri.
14Kisha nitaifanya Pathrosi ukiwa na kuweka moto katika Soani, nitatekeleza matendo ya hukumu katika No.
15Kwa kuwa nitamwaga ghadhabu yangu juu Sini, ngome ya Misri, na kuwakatilia mbali watu wa mataifa.
16Kisha nitaweka moto katika Misri; Sini itakuwa katika dhiki kuu, No itavunjika, na Nofu itakabiliana na maadui kila siku.
17Vijana katika Oni na Pi-besethi wataanguka kwa upanga, na miji yao itaenda utumwani.
18Huko Tapanesi, siku itabadilika kuwa usiku nitakapo ivunja nira ya Misri huko, na kiburi cha uwezo wake kitaisha. Kutakuwa na wingu likimfunika, na binti zake wataenda utumwani.

19Nitatekeleza matendo ya hukumu katika Misri, hivyo watajua kwamba mimi ni Yahwe.”'
20Kisha ikawa katika mwaka wa kumi na moja, katika mwezi wa kwanza, katika siku ya saba ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,
21“Mwanadamu, nimeuvunja mkono wa Farao, mfalme wa Misri. Tazama! Haukufungwa, au kufungwa kwa kitambaa cha bendeji ili upone, hivyo basi uweze kuwa imara kushika upanga.
22Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, 'Tazama, mimi niko juu ya Farao, mfalme wa Misri. Kwa kuwa nitauvunja mkono wake, wote yule aliye hodari na yule aliyevunjika, nitaufanya upanga wangu kuanguka kutoka kwenye mkono wake.
23Kisha nitaitawanya Misri miongoni mwa mataifa na kuwatawanya katika nchi mbali mbali.
24Nitaunyoosha mikono kwa mfalme wa Babeli na kuweka upanga wangu katika mkono wake ili kwamba niweze kuiharibu mikono ya Farao. Atagugumia mbele ya mfalme wa Babeli kwa mgumio wa mtu anayekufa.
25Kwa kuwa nitainyoosha mikono ya mfalme wa Babeli, wakati mkono wa Farao utakapoanguka. Kisha watajua yakwamba mimi ni Yahwe, nitakapoweka upanga wangu kwenye mkono wa mfalme wa Babeli; kwa kuwa ataishambulia nchi ya Misri kwa huo.
26Hivyo nitaitawanya miongoni mwa mataifa na kuyatawanya kwenye nchi tofauti tofauti. Kisha watajua yakwamba mimi ni Yahwe.”'