Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ezekieli

Ezekieli 36

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1“Na wewe, mwanadamu, itabirie milima ya Israeli na useme, 'Milima ya Israeli, lisikilizeni neno la Yahwe.
2Bwana Yahwe asema hivi: Adui amesema kuhusu ninyi, “Aha!” na “Mahala pa juu pa zamani pamekuwa milki yetu.”'
3Kwa hiyo tabiri na sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu ya ukiwa wenu na kwa sababu mashambulizi yaliyokuja juu yenu kutoka pande zote, mmekuwa milki ya mataifa mengine; mmeambiwa kwa midomo yao waongeao, na kwa masingizio ya watu.
4Kwa hiyo, milima ya Israeli, sikilizeni neno la Bwana Yahwe: Bwana Yahwe asema hivi kwa milima na vilima, mifereji ya maji na mabonde, mahali palipoharibika kuwa ukiwa na miji iliyoachwa ambayo imetekwa nyara na kutokuwa huru kwa kutaniwa na mataifa yaliyowazunguka-
5kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Hakika nimeongea katika moto wa hasira yangu juu ya mataifa meningine, juu ya Edemu na wote waliochukua nchi yangu kwa ajili yao wenyewe kama milki, dhidi ya wale walikuwa na furaha yote katika mioyo yao na dharau katika roho zao, kama walivyoitwaa nchi yangu kwamba wangeweza kudai nchi za malisho kwa ajili yao.
6Kwa hiyo, tabiri kwa nchi ya Israeli na sema kwa milima na vilima, hata kwenye mifereji na mabonde, Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Katika ghadhabu yangu na hasira yangu nasema hivi kwa sababu mmechukua fedheha za mataifa.
7Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi: Mimi mwenyewe nitainua mkono wangu kuapa kwamba mataifa yanayowazunguka yamkini yatawabebea aibu yao wenyewe.
8Lakini ninyi, milima ya Israeli, mtachipuza matawi na kuzaa matunda kwa ajili ya watu wangu Israeli, kwa kuwa watarudi kwenu.
9Maana tazama, nipo kwa ajili yenu, na kuwachukulia kwa fadhili; mtalimwa na kupandwa mbegu.
10Hivyo nitawaongeza juu ya milima yenu watu katika nyumba ya Israeli, yote. Miji itakaa na palipoharibiwa kujengwa.
11Nitaongeza mtu na wanyama juu yenu milima ili kwamba itaongezeka na kuzaa. Kisha nitawafanya kuishi kama mlivyokuwa, na nitawafanya kustawi zaidi kuliko mlivyokuwa zamani, kwa kuwa mtajua yakwamba mimi ni Yahwe.
12Nitawaleta watu, watu wangu Israeli, kutembea juu yenu. Watakumiliki, na utakuwa urithi wao, na hutasababisha tena watoto wao kufa.
13Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu wanakwambia, “Wewe unakula watu, na watoto wa nchi yako wamekufa,”
14kwa hiyo hautawala watu wangu tena, na hutalifanya tena taifa lako kuomboleza vifo vyao. Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
15Wala sintokuruhusu kusikiliza fedhiha za mataifa tena; hautachukua tena aibu ya watu au kufanya taifa lako kuanguka-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”'
16Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
17“Mwanadamu, wakati nyumba ya Israeli walipoikalia nchi yao, waliinajisi kwa njia zao na matendo yao. Njia zao zilikuwa kama uchafu wa hedhi ya mwanamke mbele yangu.
18Hivyo nilimwaga ghadhabu yangu juu yao kwa ajili ya damu ambayo waliyoimwaga juu ya nchi na kwa ajili ya uchafu wa hiyo kwa sanamu zao.

19Nimewatawanya miongoni mwa mataifa; walitawanyika katika nchi nyingi. Nimewahukumu kulingana na njia zao na matendo yao.
20Kisha wakaenda kati ya mataifa, na popote walipoenda, walilitukana jina langu takatifu wakati watu waliwasema, 'Je! hawa kweli ni watu wa Yahwe? Kwa kuwa wamefukuzwa nje ya nchi yake.
21Lakini nilikuwa na huruma kwa ajili ya jina langu takatifu ambalo nyumba ya Israeli walilinajisi miongoni mwa mataifa, walipoenda huko.
22Kwa hiyo waambie nyumba ya Israeli, 'Bwana Yahwe asema hivi: Sifanyi haya kwa ajili yenu, nyumba ya Israeli, lakini jina langu, mlilolitukana miongoni mwa mataifa kila sehemu mlipoenda.
23Kwa kuwa nitalifanya jina langu kuu kuwa takatifu, mlilolitukana miongoni mwa mataifa-katikati ya mataifa, mmelitukana. Kisha mataifa watajua kwamba mimi ni Yahwe-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe-asemavyo-wakati mtakapoona kwamba mimi ni mtakatifu.
24Nitawachukua kutoka mataifa na kuwakusanya kutoka kila nchi, na nitawaleta hata nchi yenu.
25Kisha nitanyunyiza maji masafi juu yenu ili muwe wasafi kutoka kwenye uchafu wote, na nitawasafisha kutoka sanamu zenu zenu.
26Nitawapatia moyo mpya na roho mpya sehemu zenu za ndani, na nitautoa moyo wa jiwe kutoka kwenye nyama zenu. Kwa kuwa nitawapatia moyo wa nyama.
27Nitaiweka Roho yangu ndani yenu na kuwawezesha kutembea katika sheria zangu na kuziweka hukumu zangu, hivyo mtazitenda.
28Kisha mtakaa katika nchi niliyowapa babu zenu; mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.
29Kwa kuwa nitawaokoa kutokana na uchafu wenu wote. Nitaita ngano kuiongeza. Sitaweka tena njaa juu yenu.
30Nitaongeza tunda la mti na kuzalisha kwenye mashamba ili kwamba msichukue tena aibu ya njaa juu ya mataifa.
31Kisha mtazikumbuka njia zenu mbaya na matendo yenu ambayo hayakuwa mazuri, na mtaonyesha chuki kwenye nyuso zenu kwa sababu ya dhambi zenu na matendo yenu maovu.
32Sifanyi hili kwa ajili yenu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-ijulikane kwenu. Hivyo tahayarikeni na kufadhaika kwa sababu ya njia zenu, nyumba ya Israeli.
33Bwana Yahwe asema hivi: Katika siku niliyowatakasa kutoka kwenye uovu wenu wote, nitawafanya miji ikaliwe na kuzijenga sehemu zilizoharibiwa.
34Kwa kuwa mtailima nchi iliyoharibiwa hadi itakapoonekana haijaaharibika mbele za macho ya wote wapitao karibu.
35Kisha watasema, “Hii nchi ilikuwa ukiwa, lakini imekuwa kama bustani ya Edeni; miji ya ukiwa na isiyo na wakaaji iliyo magofu ambayo ilibomolewa sasa inakaliwa.
36Kisha mataifa mengine waliowazunguka watajua yakwamba mimi ni Yahwe, kwamba nimejenga palipokuwa pameharibiwa na kuipanda mbegu sehemu iliyokuwa ukiwa.

37Bwana Yahwe asema hivi: Tena nitaulizwa na nyumba ya Israeli kufanya hivi kwa ajili yao, kuwaongeza kama kundi la watu.
38Kama kundi lililotengwa kwa ajili ya sadaka, kama kundi katika Yerusalimu katika sikukuu yake iliyoteuliwa, hivyo miji itaharibiwa kwa kujazwa na makundi ya watu na watajua kwamba mimi ni Yahwe.”'