Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ezekieli

Ezekieli 4

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1“Lakini wewe, mwana wa adamu, chukua tofali wewe mwenyewe na uliweke mbele yako. Kisha chonga mji wa Yerusalemu juu yake.
2Kisha laza kuizunguka, ngome juu yake. Anza kushambulia juu yake na weka makambi kuizunguka. Weka shambulio la ghasia kuizunguka.
3Kisha chukua kwa ajili yako mwenyewe sufuria ya chuma na itumie kama ukuta wa chuma kati yako mwenyewe na mji na weka uso wako dhidi yake. Kwa kuwa utazingirwa, na utaweka ukombozi juu yake. Hii itakuwa alama kwa nyumba ya Israeli.
4Kisha, lala juu upande wako wa kushoto na weka dhambi ya nyumba ya Israeli juu yake; utazibeba dhambi zao kwa hesabu za siku ambazo ulizolala juu ya nyumba ya Israeli.
5Mimi mwenyewe nakuagiza kwako siku moja kuwakilisha kila mwaka wa adhabu yao: siku 390! Katika njia hii, utachukua dhambi ya nyumba ya Israeli.
6Wakati utakapomaliza hizi siku, kisha lala chini kwa mara ya pili kwa upande wako wa kulia, kwa kuwa utabeba dhambi ya nyumba ya Yuda kwa siku arobaini. Nakuteua wewe siku moja kwa kila mwaka.
7Weka uso wako chini kuelekea Yerusalemu ambayo ni chini ya ngome, na kwa mkono wako funua unabii dhidi
8yake. Tazama! naweka vifungo juu yako hivyo hutarudi kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine hadi utakapoliza siku zako za kuzingirwa kwako.
9Chukua ngano kwa ajili yako, shayiri, dengu, mtama, kusemethi; viweke kwenye chombo kimoja na tengeneza mkate kwa ajili yako kulingana na hesabu ya siku ambazo utakazo lala katika ya upande wako. Kwa siku 390 utaula.
10Chakula utakachokula kitapimwa, shekeli ishirini kwa siku, na utakila kwa mda uliopangwa kila siku.
11Kisha utakunywa maji, kwa kuyapima sehemu ya sita ya hini, na utayanywa kwa mda uliopangwa.
12Utakila kama keki za shayiri, lakini utaioka kwenye kinyesi kikavu cha mwanadamu mbele ya macho yao!”
13Kwa kuwa Yahwe asema, “Hii inamaana kwamba ule mkate ambao watu wa Israeli watakula kitakuwa kinajisi, huko miongoni mwa mataifa ambapo nitakaowafukuza.”
14Lakini nikasema, “Ee, Bwana Yahwe! Sijawahi kuwa najisi! sijawahi kula kitu chochote ambacho kimekufa au kitu chochote kilichouawa na wanyama, kutoka mdomoni mwangu hadi sasa, wala nyama ya kunuka haijawahi kuingia kinywani mwangu!”
15Ndivyo alivvyo niambia, “Tazama! Nimekupa mbolea ya ng'ombe badala ya kinyesi cha mwanadamu ili uweze kuandaa mkate wako juu ya hayo.”
16Pia akanambia, “Mwana wa adamu! Tazama! Nalivunja gongo la mkate katika Yerusalemu, na watakula mkate ukiwa umepimwa katika wasiwasi na kunywa maji kwa kuyapima katika hofu.
17Kwa sabau watapungukiwa na mkate na maji, kila mtu atafadhaishwa na ndugu yake na kumpoteza kwa sababu ya udhalimu wao.”