Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ezekieli

Ezekieli 23

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Neno la Yahwe likanijia, kusema,
2“Mwanadamu, Kulikuwa na wanawake wawili, binti za mama mmoja.
3Walifanya ukahaba katika Misri katika kipindi cha ujana wao. Walitenda kama makahaba huko. Maziwa yao yalikuwa yamebana na ubikira wa chuchu zao zilipapaswa huko.
4Majina yao yalikuwa Ohola-dada mkubwa-na Oholiba-dada yake mdogo. Kisha wakawa wangu na kuzaa wana na binti. Majina yao yalikuwa yakimaanasha hivi: Ohola maana yake Samaria, na Oholiba maana yake Yerusalemu.
5Lakini Ohola alifanya kama kahaba hata alipokuwa wangu; aliwatamani wapenzi wake, kwa kuwa Waashuri na nguvu,
6liwali aliyekuwa amevaa urijuana, na kwa ajili ya maafisa wake, waliokuwa hodari na wanaume wa kuvutia, wote walikuwa waendesha farasi.
7Hivyo akajitoa yeye mwenyewe kama kahaba kwao, kwa watu bora wa Ashuru, na alijitia mwenyewe uchafu pamoja na kila mmoja aliyekuwa amemtamani-pamoja na sanamu zake zote.
8Kwa kuwa hakuacha tabia zake za kihaba nyuma katika Misri, wakati walipolala naye wakati alipokuwa msichana mdogo, wakati walipoanza kwanza kupapasa ubikira wa maziwa yake, wakati walipoanza kummwagia tabia ya uzinzi wao juu yake.
9Kwa hiyo nilimtia kwenye mkono wa wapenzi wake, kwenye mkono wa Waashuru kwa kuwa aliwatamani.
10Wakamfunua uchi wake. Wakawachukua wana wake na binti, na wakamuua kwa upanga, na akawa aibu kwa wanawake wengine, hivyo wakapitisha hukumu juu yake.
11Dada yake Oholiba akaliona hili, lakini aliyatamani zaidi na kufanya kama kahaba hata zaidi kuliko dada yake.
12Aliwatamanai Waashuru, mabosi na watawala waliokuwa wamevaa ngua za ushawishi, walikuwa watu waendesha farasi. Wote walikuwa hodari, wote vijana wa kuvutia.
13Nikaona kwamba alikuwa amefanya uchafu mwenyewe. Ilikuwa kama kwa wadada wote.
14Kisha akaongeza ukahaba wake tena zaidi. Aliona watu waume waliokuwa wamechorwa juu ya kuta, michoro ya Wakaldayo iliyochorwa kwa rangi nyekundu,
15waliovaa mikanda kuzunguka viuno vyao, na vilemba virefu juu ya vichwa vyao. Wote walikuwa na mwonekano wa maafisa wa jeshi la waendesha farasi, mfano wa wana wa Wababeli, ambao asili ya nchi ni Ukaldayo.
16Na mara macho yake yalipowaona, aliwatamani, hivyo akawatuma wajumbe wake kwao katika Ukaldayo.
17Kisha Wababeli wakaja katika kitanda chake cha tamaa, na walimfanya unajisi kwa uzinzi wao. Kwa kile alichokuwa amekifanya alifanya unajisi, basi akageuka mwenyewe kutoka kwao katika karaha.
18Alionyesha matendo yake ya ukahaba na alionyesha uchi wake, hivyo roho yangu ikagauka kutoka kwake, kama roho yangu ilivyogeuka kutoka kwa dada yake.

19Kisha alifanya matendo mengi zaidi ya ukahaba, akakumbuka na kutafakari siku za ujana wake, wakati alipotenda kama kahaba katika nchi ya Misri.
20Basi akawatamani wapenzi wake, ambao sehemu zao za siri zilikuwa kama zile za punda, na kile kizaliwacho hutoka kilikuwa kama wale farasi.
21Hivi ndivyo ulivyofanya matendo ya aibu ya ujana wako, wakati Wamisri walipopapasa chuchu zako kuyaminya maziwa ya ujana wako.
22Kwa hiyo, Oholiba, Bwana Yahwe asema hivi, 'Tazama! Nitawarudisha wapenzi wako dhidi yako. Wale ambao uliowarudisha, nitawaleta juu yako kutoka kila upande.
23Wababeli na Wakaldayo wote, Pekodi, Shoa, na Koa, na Waashuru wote pamoja nao, hodari, vijana wa kutamanika, magavana na maamiri jeshi, wote ni maafisa na watu wote wenye sifa, wote wenye kuendesha farasi.
24Watakuja juu yako kwa silaha, na kwa magari ya farasi na mikokoteni, na kundi kubwa la watu. Watapanga ngao kubwa, ngao ndogo, na kofia za chuma juu yako pande zote. Nitawapatia nafasi kukuadhibu, na watakuadhibu kwa matendo yao.
25Kwa kuwa nitaweka hasira yangu ya wivu juu yako, na watashughulika na wewe kwa hasira. Watakukatilia mbali pua zako na masikio yako, na masalia yako wataanguka kwa upanga. Watawachukua wana wako na binti zako, na masalia yako watateketea kwa moto.
26Watakuvua nguo zako na kuchukua mapambo yako ya vito.
27Hivyo nitaiondoa tabia yako ya aibu kutoka kwako na matendo yako ya kikahaba kutoka nchi ya Misri. Hutainua macho yako kuwaelekea kwa sahauku, na hutaikumbuka Misri tena.'
28Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi, 'Tazama! Nitakutia katika mkono wa wale uwachukiao, kukurudisha kwenye mkono wa wale ambao uliokuwa umewarudisha.
29Watashughulika pamoja nawe kwa chuki; watachukua milki zako zote na kukutelekeza uchi na kukuweka wazi. Uchi wa aibu ya ukahaba wako utafunuliwa, tabia yako ya aibu na uzinzi wako.
30Haya mambo yatafanyika kwako kwa kuwa umetenda kama kahaba, tamaa za mataifa kwazo umetiwa unajisi kwa sanamu zao.
31Umetembea katika njia za dada yako, hivyo nitaweka kikombe chake cha adhabu kwenye mkono wako.'
32Bwana Yahwe asema hivi, 'Utakinywea kikombe cha dada yako ambacho ni kirefu na kikubwa. Utakuwa dhihaka na kutawaliwa na dharau-hiki kikombe kimejaa kiasi kikubwa.
33Utajazwa kwa ulevi na huzuni, kikombe cha ushangao na uharibifu; kikombe cha dada yako Samaria.
34Utakinywea na kubakia kitupu; kisha utakivunja vunja na kuyararua maziwa yako kuwa vipande vipande. Kwa kuwa nimesema hivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.'
35Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi, 'Kwa sababu umenisahau na kunitupa mbali nyumba ya mgongo wako, basi pia utachukua matokeo ya tabia zako za aibu na matendo ya uasherati.”'
36Yahwe akanambia, “Mwanadamu, Je! utamhukumu Ohola na Oholiba? Basi waambie matendo yao ya machukizo,

37kwa kuwa wamefanya uzinzi, na kwa kuwa kuna damu juu ya vichwa vyao. Wamefanya uzinzi na sanamu zao, na wamewaweka hata wana wao kwenye moto, kama chakula cha sanamu zao.
38Kisha waliendelea kufanya hivi kwa ajili yangu: Wamepafanya patakatifu pangu unajisi, na katika siku hiyo hiyo wakainajisi Sabato zangu.
39Kwa kuwa walipokuwa wamewachinjia watoto wao kwa ajili ya sanamu zao, kisha wakaja hata patakatifu pangu siku hiyo hiyo kupanajisi! Hivyo tazama! Hivi ndivyo walivyofanya kati ya nyumba yangu.
40Mmewatuma watu kutoka mbali, ambao wajumbe waliwatuma-sasa tazama. Wakaja kweli, ambao uliojiosha kwa ajili yao, uliweka rangi macho yako, na kujipamba kwa mapambo ya vito.
41Huko ulikaa kwenye kitanda kizuri na kwenye meza iliyokuwa imepangwa mbele yake ulikuwa umeweka ubani na mafuta yangu.
42Hivyo sauti za watu zilikuwa zimemzunguka; pamoja na watu wa kila aina, hata walevi waliletwa kutoka jangwani, na wakawavalisha vikuku mikononi mwao na mataji mazuri juu ya vichwa vyao.
43Kisha nikasema juu yake aliyekuwa ameonywa kwa uzinzi, 'Sasa watazini pamoja naye, na yeye pamoja nao.'
44Wakamwingilia na kulala naye kama watu wamwingiliavyo kahaba. Katika njia hii walilala Ohola na Oholiba, waliokuwa wanawake wazinzi.
45Lakini watu wenye haki watapitisha hukumu na kuwaadhibu kama wazinzi, na watawaadhibu kwa hukumu kwa wale wamwagao damu, kwa sababu wao ni wazinzi na damu iko mikononi mwao.
46Hivyo Bwana Yahwe asema hivi: Nitainua kundi la watu juu yao na kuwatoa kuwa kitisho na kuteka nyara.
47Kisha hilo kundi la watu litawapiga kwa mawe na kuwakatilia chini kwa panga zao. Watawaua wana wao na binti na kuzichoma nyumba zao.
48Kwa kuwa nitaondoa tabia ya aibu kutoka kwenye nchi na nidhamu wanawake wote hivyo hawatatenda kama makahaba.
49Hivyo wataweka tabia yenu ya aibu juu yenu. Mtachukua hatia ya dhambi zenu pamoja na sanamu zenu, na kwa njia hii mtajua yakuwa mimi ni Bwana Yahwe.”