Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ezekieli

Ezekieli 35

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
2“Mwanadamu, weka uso wako juu ya Mlima Seiri na tabiri dhidi yake.
3Uiambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! ni juu yako, Mlima Seiri, nitakupiga kwa mkono wangu na kukufanya ukiwa na tishio.
4Nitaiharibu miji yenu, na wewe mwenyewe utakuwa ukiwa; kisha utajua kuwa mimi ni Yahwe.
5Kwa sababu umekuwa adui kwa watu wangu Israeli siku zote, na kwa sababu umewatoa kwenye mikono ya upanga wakati wa mateso yao, wakati adhabu yao itakapokuwa katika ukubwa wake.
6Kwa hiyo, kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-nitaandaa kwa ajili ya damu, na damu na kukufutilia! Kwa kuwa hukuchukia damu, damu itakufuatilia.
7Nitaufanya Mlima Seiri mkamilifu na ukiwa wakati nitakapoukatilia mbali kutoka huo yeyote apitaye na arudiye tena.
8Kisha nitaijaza milima kwa watu wao waliokufa. Milima yako na mabonde na mifereji-wale walioawa kwa upanga wataanguka kati yao.
9Nitakufanya mkiwa daima. Miji yako haitakaliwa na watu, lakini mtajua kwamba mimi ni Yahwe.
10Umesema, “Haya mataifa mawili na hizi nchi mbili zitakuwa zangu, na tutazimiliki,” hata wakati Yahwe alipokuwa pamoja nao.
11Kwa hiyo, kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-hivyo nitafanya kulingana na hasira yako na kulingana na wivu wako ambao uliousikia katika chuki yako ya Israeli, na nitajidhihirisha kwao nitakapokuhukumu.
12Hivyo utajua kwamba mimi ni Yahwe. Nimeyasikia matukano yako yote uliyasema dhidi ya milima ya Israeli, uliposema, “Wameharibiwa; wametolewa kwetu tuwale.
13“Nanyi mmejitukuza juu yangu kwa kile mlichokisema, na mmeongeza maneno juu yangu; na kuyasikia yote.
14Bwana Yahwe asema hivi: Nitakufanya ukiwa, wakati dunia nzima itakapofurahi.
15Kama vile unavyofurahi juu ya urithi wa watu wa Israeli kwa sababu ukiwa ya wake, ndivyo nitakavyokutenda wewe. Utakuwa ukiwa, Mlima Seiri, na Edomu yote! Kisha watajua kwamba mimi ni Yahwe.”'