1Katika mwaka wa ishirini na tano wa kuhamishwa kwetu mwanzoni mwa mwaka siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya mji kuchukuliwa-katika siku hiyo hiyo, mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu na alinichukua huko.
2Katika maono ya Mungu akanileta hata nchi ya Israeli. Akanileta kupumzika juu ya kila mlima mrefu sana; upande wa kusini kulikuwa na monekano kana kwamba majengo ya mji.
3Kisha akanileta huko. Tazama, kulikuwa na mtu! Mwonekano wake ulikuwa kama mwonekano wa shaba. Alikuwa na uzi wa kitani na mwanzi wa kupimia mkononi mwake, na alisimama katika lango la mji.
4Huyo mtu akanambia, “Mwanadamu, tazama kwa macho yako na sikiliza kwa masikio yako, na elekeza moyo wako juu ya yote ninayokufunulia, kwa kuwa ulinileta hapa ili niweze kukufunulia haya wewe. Toa taarifa ya kila kitu utakachokiona kwa nyumba ya Israeli.
5Kulikuwa ukuta uliokuwa umezunguka eneo la hekalu. Urefu wa kipimo cha mwanzi katika mkono wa mtu ulikuwa dhiraa sita urefu, kila urefu wa dhiraa ulikuwa dhiraa moja na kipimo cha kiganja cha mkono urefu. Aliupima ukuta; ulikuwa kipimo cha mwanzi mmoja na ufito mmoja urefu.
6Kisha akaenda hata kwenye lango la hekalu lililokuwa limeelekea mashariki. Akapanda ngazi na kuipima kizingiti cha lango-mwanzi mmoja upana.
7Vyumba vya ulinzi vilikuwa kila mwanzi mmoja urefu na mwanzi mmoja upana; kulikuwa na dhiraa tano katika kila vyumba viwili, na kizingiti cha lango la hekalu karibu na tawa la hekalu kilikuwa mwanzi mmoja urefu.
8Akapima tawa la lango; ulikuwa mwanzi mmoja urefu.
9Akapima tawa la lango. Ilikuwa mwanzi mmoja kwenda chini. Mihimili ilikuwa dhiraa mbili upana. Hili lilikuwa tawa la lango kuelekea hekalu.
10Kulikuwa na vyumba vitatu vya ulinzi pande zote za lango la mashariki, na yote yalikuwa na kipimo kile kile, na kuta zilizokuwa zimezigawanya zilikuwa na kipimo kile kile.
11Kisha yule mtu akapima upana wa njia ya lango la kuingia-dhiraa kumi; na akapima urefu wa njia ya lango la kuingia-dhiraa kumi na tatu.
12Akaupima ukuta uliokuwa mpaka mbele ya vyumba-dhiraa moja urefu. Vyumba vilipimwa dhiraa sita kila upande.
13Kisha akapima lango la njia kutoka kwenye paa ya chumba kimoja kuelekea chumba kingine-dhiraa ishirini na tano, kutoka lango la kuingia chumba cha kwanza kuelekea kile cha pili.
14Kisha akapima ukuta uliokuwa umeenda kati ya vyumba vya ulinzi-dhiraa sitini urefu; alipima kwa mbali na tawa la lango.
15Lango la kuingia kutoka lango la mbele kuelekea lango jingine la tawa la mwisho lilikuwa dhiraa hamsini.
16Kulikuwa na madirisha yaliyokuwa yamefungwa kuelekea vyumba na kuelekea nguzo zake kati ya malango kuzunguka kote; na vivyo hivyo kwa mabaraza. Kulikuwa na madirisha pande zote za ndani, na kila mhimili ulikuwa umepambwa kwa mitende.
17Kisha huyo mtu akanileta hata ua wa nje mwa hekalu. Tazama, kulikuwa na vyumba, na kulikuwa na kibamba katika ua, pamoja na vyumba thelathini baada ya kibamba.
18Kibamba kilienda juu hata upande wa malango, na upana wake ulikuwa sawsawa na urefu wa malango. Hiki kilikuwa kibamba cha chini.
19Kisha huyo mtu akapima umbali kutoka mebele ya lango la chini hata mbele ya lango la ndani; ilikuwa dhiraa mia moja upande wa mashariki, na sawasawa na upande wa kaskazini.
20Kisha akapima urefu na upana wa lango lililokuwa upande wa kaskazini mwa ua wa nje.
21Kulikuwa na vyumba vitatu pande zote za lango, na lango na matawa yake yalipimwa sawa na lango kubwa-dhiraa hamsini upana wote na dhiraa ishirini na tano upana.
22Madirisha yake, tawa, vyumba, na mitende yake vilikabiliana na lango ambalo linaloelekea mashariki. Ngazi saba kuupandia juu hata kwenye tawa lake.
23Kulikuwa na lango kwenye ua wa ndani mbele kuelekea mashariki; huyo mtu alipima kutoka lango moja hadi lango jingine-dhiraa mia moja umbali.
24Kisha huyo mtu akanileta hata kwenye lango la kuingia la kusini, na kuta zake na tawa vilipimwa sawa kama malango mengine ya nje.
25Kulikuwa na madirisha yaliyofungwa katika lango la njia na tawa lake kama lile lango. Lango la kusini na tawa lake vilipimwa dhiraa hamsini urefu na dhiraa ishirini na tano upana.
26Kulikuwa na ngazi saba hadi kwenye lango na matawa yake, na kulikuwa na mitende iliyochongoka juu ya kuta pande zote.
27Kulikuwa na lango la ua wa ndani upande wa kusini, na yule mtu akapima kutoka hilo lango hata lango la kuingia upande wa kusini-dhiraa mia moja umbali.
28Kishi huyo mtu akanileta hata ua wa ndani karibu na lango lake la kusini, ambalo lilikuwa na vipimo vile vile kama malango mengine.
29Vyumba vyake, kuta, na matao vilipimwa sawa kama malango mengine; kulikuwa na madirisha kuzunguka matao yote. Lango la ndani na matao yake yalipimwa dhiraa hamsini urefu na dhiraa ishirini na tano upana.
30Pia kulikuwa na matao pande zote za kuta za ndani; haya yalikuwa dhiraa ishirini na tano urefu na dhiraa tano upana.
31Hili tawa lilielekea ua wa nje pamoja na mitende iliyochongwa juu ya kuta zake na ngazi nane kuupandia.
32Kisha yule mtu akanileta hata kwenye ua wa ndani karibu na njia ya kaskazini na kulipima lango, ambalo lilikuwa na vipimo sawa kama malango mengine.
33Vyumba vyake, kuta, na matawa yalikuwa na kipima sawa kama cha malango, na kulikuwa na madirisha pande zote. Laango la ndani na matawa yake yalikuwa dhiraa hamsini urefu na dhiraa ishirini na tano upana.
34Matawa yake yalielekea nje ya ua; ilikuwa na mitende pande zote za hiyo na ngazi nane za kuupandia.
35Kisha huyo mtu akanileta hata lango la kaskazini na kulipima; likapimwa vivyo hivyo kama malango mengine.
36Vyumba vyake, kuta, na ukumbi vilipimwa sawa na malango mengine, na kulikuwa na madirisha pande zote. Njia ya lango na matao yake yalipimwa dhiraa hamsini urefu na upana dhiraa ishirini na tano.
37Tatawa lake lilielekea ua wa nje; ilikuwa na mitende pande zote za huo na ngazi nane kuupandia.
38Kulikuwa na chumba pamoja na mlango karibu na kila lango la ndani. Hapa ndipo ambako walipooshea sadaka za kutekezwa.
39Kulikuwa na meza mbili kila upande wa kila ukumbi, ambako sadaka ya kuteketezwa ilipochinjiwa, na pia sadaka ya dhambi na sadaka ya hatia.
40Karibu na ukuta wa ua, kuelekea juu kwenye lango kuelekea kaskazini, kulikuwa na meza mbili. Pia kwa upande mwingine kulikuwa na meza mbili kwenye lango la ukumbi.
41Kulikuwa na meza nne pande zote karibu na lango; wakachinja wanyama juu ya meza nane.
42Kulikuwa na meza nne za mawe yaliyochongwa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, dhiraa moja na nusu urefu, dhiraa moja na nusu upana, na kimo dhiraa moja. Juu yake waliweka vyombo pamoja ambavyo walivichinjia sadaka za kuteketezwa kwa ajili ya sadaka.
43Kulabu mbili ujazo wa kiganja urefu uliokuwa umeunganishwa katika ua pande zote, na nyama ya matoleo ilikuwa imewekwa juu ya meza.
44Karibu na lango la ndani, katika ua wa ndani, kulikuwa na vyumba vya waimbaji. Moja ya hivi vyumba kilikuwa upande wa kaskazini, na kingine kusini.
45Kisha yule mtu akanambia, “Hiki chumba kinachoelekea kusini ni kwa ajili ya makuhani walio zamu katika hekalu.
46Chumba kilichoelekea kaskazini kilikuwa kwa ajili ya makuhani waliokuwa zamu kwenye madhabahu. Hawa ni wana wa Sadoki ambaye huja humkaribia Yahwe kumtumikia; ambao ni miongoni mwa wana wa Lawi.”
47Kisha akaupima ule ua-dhiraa mia moja urefu na dhiraa mia moja upana mraba, pamoja na madhabahu mbele ya nyumba.
48Kisha yule mtu akanileta hata kwenye varanda ya nyumba na kupima mwimo wa milango yake-ilikuwa dhiraa tano unene upande huu. Njia ya kuingilia yenyewe ilikuwa dhiraa kumi na nne, na kuta pande zote za huo zilikuwa dhraa tatu upana.
49Urefu wa ukumbi ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake ulikuwa dhiraa kumi na moja. Kulikuwa na ngazi zilizokuwa zimepanda juu na nguzo zilizokuwa zimesimama pande zote za huo.