Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Samweli

2 Samweli 1

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Baada ya kifo cha Sauli, Daud alirudi kutoka kuwashambulia Waamaleki na akakaa Siklagi kwa siku mbili.
2Siku ya tatu, mtu mmoja alikuja kutoka kambi ya Sauli nguo zake zikiwa zimeraruliwa na akiwa na vumbi juu ya kichwa chake. Alipofika kwa Daudi alinamisha uso wake chini akajifanya yeye mwenyewe kuwa si kitu.
3Daudi akamuliza, “Unatoka wapi?” Yeye akajibu, “Nimeponyoka kutoka kambi ya Israeli.”
4Daudi akamwambia, “Tafadhari nieleze jinsi mambo yalivyokuwa.” Akajibu, “Watu walikimbia kutoka vitani. Wengi wameanguka, na wengi wao wameuawa. Sauli na Yonathani mwanawe pia wameuawa.”
5Daudi akamwuliza kijana, “unajuaje kuwa Sauli na Yonathani mwanawe wameuawa?”
6Yule kijana akajibu, “Kwa bahati nilikuwa juu ya Mlima Gilboa, na pale alikuwepo Sauli ameegemea mkuki wake, na magari ya farasi na waongozaji walikuwa karibu kumkamata.
7Sauli alipogeuka aliniona na akaniita. Nikajibu, 'Mimi hapa.'
8Akaniuliza, 'Wewe ni nani?' Nikamjibu, 'Mimi ni Mwamaleki,'
9Akaniambia, Tafadhari simama juu yangu uniuwe, kwa kuwa shida kubwa imenipata, lakini uhai ungalimo ndani yangu.'
10Hivyo nilisimama juu yake nikamuuwa, kwa maana nilijua kwamba asingeweza kuishi baada ya kuwa ameanguka. Ndipo nikachukuwa taji iliyokuwa juu ya kichwa chake na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, na nimevileta hapa kwako, bwana wangu.”
11Kisha Daudi akararua mavazi yake, na watu wote waliokuwa pamoja naye wakafanya vilevile.
12Walilia, wakaomboleza na kufunga mpaka jioni kwa ajili ya Sauli, Yonathani mwanawe, watu wa Yahwe, na kwa ajili ya nyumba ya Israeli kwa maana wameanguka kwa upanga.
13Daudi akamwambia yule kijana, “Unatokea wapi?” Akajibu, mimi ni kijana wa mgeni Mwamaleki.”
14Daudi akamwambia, “Kwa nini haukuogopa kumwua mfalme, mtiwa mafuta wa Yahwe kwa mkono wako?”
15Daudi akamwita mmojawapo wa vijana na akamwambia, “Nenda ukamuue.” Hivyo kijana huyo akaenda na kumpiga hata ata chini, Mwamaleki akafa.
16Ndipo Daudi akamwambia Mwamaleke aliyekufa, “Damu yako iwe juu ya kichwa chako kwa kuwa kinywa chako kimeshuhudia dhidi yako kusema, Nimemuua mfalme mtiwa mafuta wa Yahwe.
17Ndipo Daudi akaimba wimbo wa maombolezo juu ya Sauli na Yonathani mwanawe.
18Akawaamuru watu kuufundisha wimbo wa Bow kwa wana wa Yuda, ambao umeandikwa katika Kitabu cha Yashari.

19“Utukufu wako, Israel, umeondolewa, umeondolewa juu ya mahali pako pa juu! Jinsi mwenye nguvu alivyoanguka!
20Msiiseme katika Gathi, msiitangaze katika mitaa ya Ashikeloni, ili binti za wafilisti wasifurahi, ili binti za wasiotailiwa wasisherehekee.
21Milima ya Gilboa, kusiwe na umande au mvua juu yenu. wala mashamba yasitoe nafaka kwa ajili ya sadaka, kwa maana hapo ngao ya mwenye nguvu imeharibiwa. Ngao ya Sauli haiwezi tena kutiwa mafuta.
22Kutoka katika damu ya waliouawa, kutoka katika miili ya wenye nguvu, upinde wa Yonathani haukurudi nyuma, na upanga wa Sauli haukurudi patupu.
23Sauli na Yonathani walikuwa wakipendwa na walikuwa wenye neema maishani, hata wakati wa mauti yao walikuwa pamoja. Walikuwa na kasi kuliko tai, walikuwa na nguvu kuliko simba.
24Enyi binti wa Israeli lieni juu ya Sauli, aliyewavika mavazi ya thamani pamoja na vito vya thamani, na aliyetia mapambo ya dhahabu katika mavazi yenu.
25Jinsi wenye nguvu walivyoanguka vitani! Yonathani ameuawa juu ya mahali pako pa juu.
26Nimesikitishwa sana kwa ajili yako, Yonathani ndugu yangu. Ulikuwa mpendwa wangu sana. Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, ukipita upendo wa wanawake.
27Jinsi wenye nguvu walivyoanguka na silaha za vita zimeteketea!”