Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Samweli

2 Samweli 3

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kulikuwa na vita ya mda mrefu kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi. Daudi akaendelea kupata nguvu zaidi, lakini nyumba ya Sauli iliendelea kudhoofika na kuthoofika.
2Wana wakazaliwa kwa Daudi huko Hebron. Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Amnoni, kwa Ahinoamu wa Yezreeli.
3Mwanawe wa pili, Kileabu, alizaliwa kwa Abigaili, mjane wa Nabali wa Karmeli. Wa tatu, Absalomu, alikuwa mwana wa Maaka, binti Talmai, mfalme wa Geshuri.
4Mwana wa nne wa Daudi, Adoniya, alikuwa mwana wa Hagithi. Mwanawe wa tano alikuwa Shefatia mwana wa Abitali,
5na wa sita, Ithreamu, alikuwa mwana wa Egla mkewe Daudi. Hawa wote walizaliwa kwa Daudi huko Hebroni.
6Ikawa wakati wa vita kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi Abneri akajifanya mwenye nguvu katika nyumba ya Sauli.
7Sauli alikuwa na suria jina lake Rispa, binti Aiya. Ishboshethi akamuuliza Abneri, “Kwa nini umelala na suria wa baba yangu?”
8Hata ikawa Abneri akakasirika sana kutokana na maneno ya Ishboshethi naye akasema, “Je mimi ni kichwa cha mbwa wa Yuda? Ninaonesha uaminifu kwa nyumba ya Sauli, baba yako, kwa jamaa yake, na rafiki zake, kwa kutokukuweka katika mkono wa Daudi. Na bado leo unanishutumu kuhusu mwanamke.
9Mungu na anifanyie hivyo, Abneri, na kuzidi, ikiwa sitafanya kwa Daudi kama Yahwe alivyomwapia,
10kuuhamisha ufalme kutoka nyumba ya Sauli na kukisimika kiti cha enzi cha Daudi juu ya Israeli na juu ya Yuda, kutoka Dani hadi Beersheba.”
11Ishboshethi hakuweza kumjibu Abneri neno tena, kwani alimuogopa.
12Kisha Abneri akatuma wajumbe kwa Daudi kusema, “Nchi hii ni ya nani? Fanya agano nami, nawe utaona kwamba mkono wangu uko nawe, kuiIeta Israeli yote kwako.”
13Daudi akajibu, “Vema, nitafanya agano nawe. Lakini neno moja ninalolitaka kutoka kwako ni kwamba hautauona uso wangu usipomuleta kwanza Mikali, binti Sauli, unapokuja kuonana nami.”
14Kisha Daudi akatuma wajumbe kwa Ishboshethi, mwana wa Sauli, kusema, “Nipe Mikali, mke wangu niliyetoa kwa ajili yake govi mia moja za Wafilisti.”
15Hivyo Ishboshethi akatuma kwa Mikali na kumchukua kutoka kwa mme wake, Paltieli mwana wa Laishi.
16Mme wake akafuatana naye, huku akilia, akaendelea hadi Bahurimu. Kisha Abneri akamwambia, “basi sasa rudi nyumbani.” Hivyo akarudi.
17Abneri akaongea na wazee wa Israeli kusema, “Zamani mlitaka Daudi awe mfalme wenu.
18Basi sasa fanyeni hivyo. Kwa maana Yahwe alisema kuhusu Daudi kusema, “Kwa mkono wa Daudi mtumishi wangu nitawaokoa watu wangu Israeli kutoka katika mkono wa Wafilisti na kutoka katika mkono wa adui zao wote.”

19Pia Abneri akasema na watu wa Benjamini ana kwa ana. Kisha Abneri akaenda kuongea na Daudi huko Hebroni akaeleza kila jambo ambalo Israeli na nyumba yote ya Benjamini walitamani kulitimiza.
20Wakati Abneri na watu ishirini kati ya watu wake walifika Hebroni kumuona Daudi, Daudi akaandaa sherehe kwa ajili yao.
21Abneri akamweleza Daudi, “Nitainuka na kukukusanyia Israeli wote, bwana wangu mfalme, ili kwamba wafanye agano nawe, kwamba utawale juu ya yote unayotaka.” Hivyo Daudi akamruhusu Abneri kuondoka, Abneri akaondoka kwa amani.
22Kisha askari wa Daudi na Yoabu wakarudi kutoka katika kuteka nyara na wakaja na nyara nyingi. Lakini Abneri hakuwepo Hebroni pamoja na Daudi. Daudi alikuwa amemruhusu kuondoka, na alikuwa ameondoka kwa amani.
23Wakati Yoabu na Jeshi lote walipofika, Yoabu aliambiwa, “Abneri mwana wa Neri alikuja kwa mfalme, na mfalme amemruhusu kuondoka, naye Abneri ameondoka kwa amani.”
24Kisha Yoabu akaja kwa mfalme na kusema, “Umefanya nini? Tazama, Abneri alikuja kwako! Kwa nini umemruhusu kuondoka, naye amenda?
25Haujui kwamba Abneri mwana wa Neri alikuja kukudanganya na kupeleleza hali yako na kuangalia kila unalofanya?”
26Yoabu alipoondoka kwa Daudi, alituma wajumbe kumfuatia Abneri, nao wakamrudisha kutoka katika kisima cha Sirah, lakini Daudi hakulijua hili.
27Abneri aliporudi Hebroni, Yoabu alimchukua kando kati ya lango ili aongee naye faraghani. Hapohapo Yoabu alimchoka tumboni na kumuua. Hivyo, akalipa kisasi cha damu ya Asaheli nduguye.
28Daudi alipolisikia jambo hili akasema, “Mimi na ufalme wangu hatuna hatia mbele za Yahwe daima, kuhusiana na damu ya Abneri mwana wa Neri.
29Hatia ya damu ya Abneri na iwe juu ya Yoabu na nyumba yote ya baba yake. Na asikosekane katika familia ya Yoabu mtu mwenye vidonda, au mwenye ukoma, au kirema atembeaye kwa fimbo au aliyeuawa kwa upanga au mwenye kukosa chakula.”
30Hivyo Yoabu na Abishai nduguye wakamwua Abneri, kwa sababu alimwua Asaheli ndugu yao vitani huko Gibeoni.
31Daudi akamwambia Yoabu na wote waliokuwa pamoja naye, “Rarueni mavazi yenu, jivikeni nguo za magunia, na muomboleze mbele ya mwili wa Abneri.” Na mfalme Daudi akaufuata mwili wa Abneri wakati wa mazishi.
32Wakamzika Abneri huko Hebroni. Mfalme akalia kwa sauti katika kaburi la Abneri, na watu wote pia wakalia.
33Mfalme akamwombolea Abneri naye akaimbo, “Je ilipasa Abneri afe kama afavyo mpumbavu?
34Mikono yako haikufungwa. Miguu yako hakuwa imefungwa minyororo. Kama mtu aangukavyo mbele ya wana wa uovu, ndivyo ulivyoanguka.” Watu wote wakamlilia zaidi.
35Watu wote wakaja kumtaka Daudi ale wakati kungali mchana, lakini Daudi akaapa, “Mungu na anifanyie hivyo, na kuzidi, ikiwa nitaonja mkate au chochote kabla jua halijazama.”
36Watu wote wakaiona huzuni ya Daudi, na ikawapendeza, hivyo kila alichokifanya mfalme kikawapendeza.

37Hivyo watu wote na Israeli wote wakatambua siku hiyo kwamba haikuwa nia ya mfalme Abneri mwana wa Neri afe.
38Mfalme akawaambia watumishi wake, “je hamjui kuwa mtu mkuu ameanguka leo hii katika Israeli?
39Nami leo nimedhoofika, japokuwa nimetiwa mafuta kuwa mfalme. Watu hawa, wana wa Seruya ni hatari sana kwangu. Yahwe na amrudishie mwovu kwa kumlipa kwa ajili ya uovu wake kama anavyostahili.