Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Samweli

2 Samweli 5

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisha kabila zote za Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni nao wakasema, “Tazama, sisi ni nyama na mifupa yako.
2Kipindi kilichopita, Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, ni wewe uliyeliongoza jeshi la Waisraeli. Yahwe akakwambia, 'Utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala juu ya Israeli.”
3Hivyo wazee wote wa Israeli wakaja kwa mfalme huko Hebron na mfalme Daudi akafanya nao agano mbele ya Yahweh. Wakamtawaza Daudi kuwa mfalme wa Israeli.
4Daudi alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza kutawala, naye akatawala miaka arobaini.
5Alitawala juu ya Yuda miaka saba na miezi sit a huko Hebroni, na huko Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu juu ya Israeli yote na Yuda.
6Mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu kupigana na wayebusi, waliokuwa wenyeji wa nchi. Wakamwambia Daudi, “Hautaweza kuja hapa kwani hata wipofu na vilema waweza kukudhuia kuingia. Daudi haweze kuja hapa.”
7Lakini, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, ambayo sasa ni mji wa Daudi.
8Wakati huo Daudi akasema, “Waliowashambulia wayebusi watapaswa kupita katika mfereji wa maji ili wawafikie virema na vipofu ambao ni adui wa Daudi.” Hii ndiyo maana watu husema, “Vipofu na virema wasingie katika kasri.”
9Hivyo Daudi akaishi ngemeni naye akaiita mji wa Daudi. Akaizungushia ukuta, kuanzia barazani kuelekea ndani.
10Daudi akawa na nguvu sana kwa maana Yahwe, Mungu wa utukufu, alikuwa pamoja naye.
11Kisha Hiramu mfalme wa Tiro akatuma wajumbe kwa Daudi, na miti ya mierezi, mafundi seremala na wajenzi. Wakamjengea Daudi nyumba.
12Daudi akatambua kuwa Yahwe alikuwa amemweka ili awe mfalme juu ya Israeli, na kwamba alikuwa ameutukuza ufalme wake kwa ajili ya Israeli watu wake.
13Baada ya Daudi kuondoka Hebroni na kwenda Yerusalemu, akajitwalia wake na masuria wengi huko Yerusalemu, na wana na binti wengi walizaliwa kwake.
14Haya ndiyo majina ya wanawe waliozaliwa kwake huko Yerusalemu: Shamua, Shobabu, Nathani, Selemani,
15Ibhari, Elishua, Nefegi, Yafia,
16Elishama, Eliada na Elifeleti.
17Basi wafilisti waliposikia kwamba Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme juu ya Israeli, wakaenda wote kumtafuta. Daudi aliposikia hilo akashuka ngomeni.
18Basi Wafilisiti walikuwa wamekuja na kuenea katika bonde la Mrefai.

19Kisha Daudi akaomba msaada kutoka kwa Yahwe. Akasema, “Je niwashambulie wafilisti? Je utanipa ushindi juu yao?” Yahwe akamwambia Daudi, “Washambulia, kwa hakika nitakupa ushindi juu ya wafilisti.”
20Hivyo Daudi akawashambulia huko Baali Perasimu, naye akawashinda. Akasema, Yahwe amewafurikia adui zangu mbele yangu kama mafuriko ya maji. Kwa hiyo jina la mahali pale likawa Baali Perasimu.
21Wafilisiti wakaacha vinyago vyao pale, na Daudi na watu wake wakaviondoa.
22Kisha wafilisiti wakaja kwa mara nyingine tena na kujieneza zaidi katika bonde la Mrefai.
23Hivyo Daudi akatafuta msaada tena kutoka kwa Yahweh, naye Yahweh akamwambia, “Usiwashambulie kwa mbele, lakini uwazunguke kwa nyuma na uwaendee kupitia miti ya miforosadi.
24Wakati utakaposikia sauti za mwendo katika upepo uvumao juu ya miti ya miforosadi, hapo ushambulie kwa nguvu. Fanya hivi kwa kuwa Yahwe atatangulia mbele yako kulishambulia jeshi la Wafilisiti.”
25Hivyo Daudi akafanya kama Yahwe alivyomwamuru. Akawaua wafilisti njiani mwote toka Geba hadi Gezeri.