Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Samweli

2 Samweli 8

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1ikawa baada ya haya Daudi aliwashambulia Wafilisti na kuwashinda. Hivyo Daudi akaichukua Gathi na vijiji vyake kutoka katika mamlaka ya wafilisti.
2Kisha akaishinda Moabu na akawapima watu wake kwa mstari kwa kuwafanya walale chini juu ya ardhi. Alipima mistari miwili ya kuua, na mstari mmoja kamili kuwahifadhi hai. Hivyo Wamoabu wakawa watumishi wa Daudi na wakaanza kumlipa kodi.
3Kisha Daudi akamshinda Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba, Hadadezeri aliposafiri kuurudisha ufalme wake katika mto Frati.
4Daudi aliteka magari 1, 700 ya farasi na askari ishirini elfu waendao kwa miguu. Daudi akawakata miguu farasi wa magari, lakini akahifadhi wakutosha magari mia moja.
5Wakati Washami wa Dameski walipokuja kumsaidia Hadadeziri mfalme wa Soba, Daudi akaua katika Washami watu ishirini na mbili elfu.
6Daudi akaweka ngome huko Shamu ya Dameski, na Washami wakawa watumishi wake na wakaleta kodi. Yahwe akampa Daudi ushindi kila alikokwenda.
7Daudi akachukua ngao za dhahabu walizokuwa nazo watumishi wa Hadadezeri naye akazileta Yerusalemu.
8Mfalme Daudi akachukua shaba nyingi kutoka Beta na Berosai, miji ya Hadadezeri.
9Wakati Tou, mfalme wa Hamathi, aliposikia kwamba Daudi amelishinda jeshi lote la Hadadezeri,
10Tou akamtuma Hadoramu mwanawe kwa mfalme Daudi kumpa salamu na kumbariki, kwa kuwa Daudi alikuwa amepigana na Hadadezeri na kumshinda, maana Hadadezeri alikuwa amepiga vita dhidi ya Tou. Hadoramu akaja pamoja na vitu vya fedha, dhahabu, na shaba.
11Mfalme Daudi akaviweka wakfu vitu hivi kwa ajili ya Yahwe, pamoja na fedha na dhahabu kutoka katika mataifa yote aliyokuwa ameyashinda-
12kutoka Shamu, Moabu, Waamoni, Wafilist, Waamaleki, pamoja na nyara zote alizoziteka kutoka kwa Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba.
13Jina la Daudi likajulikana sana alipowashinda washami katika bonde la Chumvi, pamoja na watu wao wapatao elfu kumi na nane.
14Akaweka ngome katika Edomu yote, na Waedomu wote wakawa watumishi wake. Yahwe akampa Daudi ushindi kila alipokwenda.
15Daudi akatawala juu ya Israeli yote, naye akatenda kwa haki na usawa kwa watu wote.
16Yoabu mwana wa Seruya alikuwa mkuu wa jeshi, na Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mwenye kuandika taarifa.
17Sadoki mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani, na Seraya alikuwa mwandishi.
18Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi, na wana wa Daudi walikuwa washauri wa mfalme.