Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Torati

Torati 7

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Wakati Yahwe Mungu wenu atuleta katika nchi ambayo mnaenda kuimiliki na kuwaondoa mataifa mengi mbele zenu- Mhiti, Mgirgashi na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, Mhivi, Myebusi- mataifa saba makubwa na yenye nguvu kuliko wewe.
2Na wakati Yahwe Mungu wenu awapa ninyi ushindi juu yao pindi mnakutana nao katika vita, mtawashambulia, basi mnapaswa kuwateketeza kabisa. Hamtafanya agano nao, wala kuonesha huruma kwao.
3Wala hamtapanga ndoa zozote pamoja nao, hamtawatoa binti zenu kwa vijana wao, na hamtawachukua binti zao kwa vijana wenu.
4Kwa kuwa watawabadilisha vijana wenu kutonifuata mimi, ili kwamba waweze kuabudu miungu yao. Kwa hiyo hasira ya Yahwe itawashwa dhidi yenu na atawaangamiza haraka.
5Hivi ndivyo mtakavyo washughulikia nao; mtavunja madhabahu zao, vunja nguzo zao za mawe katika vipande, kata chini ncha za Asherahi, na kuzichoma sanamu za kutupwa.
6Kwa kuwa wewe ni taifa uliyetengwa kwa Yahwe Mungu wako. Amekuchagua wewe kuwa watu kwa ajili yake kumiliki, zaidi ya watu wengine wote ambao wako katika uso wa dunia.
7Yahwe hakuweka upendo wake juu yenu au kuwachagua kwa sababu mlikuwa zaidi katika idadi kuliko watu wowote, kwa kuwa mlikuwa wachache kuliko watu wote-
8Lakini kwa sababu anawapenda ninyi, anataka kushika kiapo alichoapa kwa baba zenu. Huyu ni Yahwe aliyewatoa kwa mkono wa uweza na kuwakomboa kutoka nyumba ya utumwa, kutoka mkono wa Farao, mfalme wa Misri.
9Kwa hiyo tambua ya kuwa Yahwe Mungu wako-ni Mungu, Mungu mwaminifu, anayetunza maagano na uaminifu kwa vizazi elfu kwa wale wanaompenda na kuyashika maagizo yake,
10lakini huwalipa wale wanaomchukia kwa sura zao, kuwaangamiza, hatakuwa na huruma kwa yeyote anayemchukia; atamlipa kwa uso wake.
11Kwa hiyo utashika maagizo, amri, na sheria ninazokuamuru leo, ili kwamba uzifanye.
12Kama mtasikiliza maagizo haya, kuyashika na kuyafanya, itakuwa Yahwe Mungu wenu atawashika pamoja na agano na uaminifu ambao aliapa kwa baba zenu.
13Atawapenda, atawabariki, na kuwazidisha, pia atabariki tunda la miili yenu na tunda la ardhi yenu, nafaka zenu, divai mpya, mafuta yenu, atazidisha mifugo na kundi lako la mifugo michanga, katika nchi ambayo aliapa kwa baba zenu kuwapa.
14Mtabarikiwa zaidi kuliko watu wengine wote; hapatakuwa na mwanaume asiyekuwa na mtoto au mwanamke tasa miongoni mwenu au miongoni mwa mifugo.
15Yahwe atawaondolea magonjwa yote; hakuna magonjwa mabaya ya Misri ambayo mnayajua yatawekwa juu yenu, Lakini atayaweka kwa wote wanaowachukia ninyi.
16Mtayaondoa makundi ya watu wote ambayo Yahwe Mungu wenu awapa ushindi, na jicho lenu halitawaonea huruma. Na hamtaabudu miungu yao, kwa kuwa huo utakuwa mtego kwenu.
17Kama mtasema kwenye mioyo, Haya mataifa ni mengi zaidi kuliko mimi; nitawezaje kuwafukuza?
18Usiwaogope; utakumbuka akilini Yahwe nini Mungu wenu alifanya kwa Farao na Misri yote?

19Mateso makuu ambayo macho yenu yaliona, ishara, maajabu, mkono wa uweza, mkono ulionyoshwa ambao Yahwe Mungu wenu alivyowatoa. Yahwe Mungu wenu atafanya kile kile kwa watu wote ambao mnawaogopa.
20Zaidi ya yote, Yahwe Mungu wenu atatuma nyigu miongoni mwao, mpaka wale waliobaki na wale wanaojificha wenyewe mbele yenu waangamizwa mbele ya uwepo wenu.
21Hamtatishikeni nao, kwa kuwa Yahwe Mungu wenu yuko miongoni mwenu, Mungu mkuu na wa kuogofya.
22Yahwe Mungu wenu atayaondoa mataifa mbele zenu kidogo kidogo. Hamtayashinda yote kwa wakati mmoja, au wanyama wa mwitu watakuwa wengi karibu yenu.
23Lakini Yahwe Mungu wenu atawapa ninyi ushindi dhidi yao wakati mkutanapo vitani; atawachanganya kwa kiasi kikubwa mpaka wameangamizwa.
24Atawaweka wafalme wao chini ya utawala wenu, na mtafanya jina lao kuangamia toka chini ya mbingu. Hakuna atakayeweza kusimama mbele yenu, mpaka muwaangamize.
25Utazichoma sanamu za kuchonga za miungu yao- usitamani madini ya fedha au dhahabu yanayofunika na kuichukua kwa ajili yenu, kwa sababu mkifanya, mtanaswa nayo-kwa kuwa ni chukizo kwa Yahwe Mungu wenu.
26Hamtaleta chukizo lolote ndani ya nyumba zenu na kuanza kuiabudu. Mtachukizwa kabisa na kuchukia kwa kuwa imetengwa kwa ajili ya uharibifu.