1Ninyi ni watu wa Yahwe Mungu wenu. Msijikate wenyewe, wala kunyoa sehemu za nyuso zenu kwa ajili ya wafu.
2Kwa kuwa mu taifa lilowekwa wakfu kwa Yahwe Mungu wenu, na Yahwe amewachagua kuwa watu kwa ajili ya urithi wake, zaidi kuliko watu wote walio juu ya uso wa dunia.
3Hampaswi kula kitu chochote kilicho chukizo.
4Hawa ni wanyama ambao mnaweza kula: ng'ombe, kondoo, mbuzi,
5kulungu, paa, kulungu wa kiume, mbuzi wa mwituni, paa mweupe na pofu na kondoo wa mlimani
6Mnaweza kula wanyama wowote ambao wamegawanyika kwato, ambaye ana kwato zilizogawanyika mara mbili, na utafuna macheuo.
7Hata hivyo, hampaswi kula baadhi ya wanyama ambao utafuna macheuo au ambao wana kwato zilizogawanyika mara mbili: ngamia, sungura, pomono, kwa sababu watafuna macheuo lakini hawajagawanyika kwato, ni najisi kwenu.
8Nguruwe ni najisi kwenu pia kwa sababu amegawanyika kwato lakini hatafuni macheuo; ni najisi kwenu. Msile nyama ya nguruwe, na msiguse mizoga yao.
9Haya yaliyo ndani ya maji mnaweza kula: chochote kilicho na mapesi na magamba;
10lakini chochote kisichokuwa na mapesi na magamba msile; ni najisi kwenu.
11Ndege wote safi mnaweza kula.
12Lakini hawa ni ndege ambao hampaswi kula: tai, tumbusi, kipungu,
13mwewe mwekundu na mweusi, aina yoyote ya kipanga.
14Hampaswi kula aina yoyote ya kunguru,
15na mbuzi na mwewe wa usiku, Lanes ndege wa baharini, aina yoyote ya mwewe,
16bundi mdogo, bundi mkubwa, na bundi mweupe,
17Mwari, nyamafu ya tai, mnandio.
18Hampaswi kula korongo, aina yoyote ya kongoti, hudihudi, na popo.
19Wote wenye mabawa; vitu vya utando ni najisi kwenu; havipaswi kuliwa.
20Mnaweza kula vitu vyote virukavyo.
21Hampaswi kula chochote kinachokufa chenyewe; mnaweza kumpa mgeni ambaye yuko katika mji wenu, kwamba anaweza kula au mnaweza kuuza kwa mgeni. Kwa kuwa mu taifa lilolowekwa wakfu kwa ajili ya Yahwe Mungu wenu. Hampaswi kumchemusha mbuzi kijana katika maziwa ya mama yake.
22Hakika mnapaswa kutoa fungu la kumi la mavuno ya mbegu zenu zote, ambazo huja kutoka kwenye shamba kila mwaka.
23Mnapaswa kula mbele ya Yahwe Mungu wenu, katika eneo ambalo atachagua kama patakatifu pake, fungu la kumi la nafaka zenu, za mvinyo mpya, na mafuta yenu, na mzaliwa wa kwanza wa wanyama na mifugo, kwamba mnaweza kujifunza daima kumheshimu Yahwe Mungu wenu.
24Kama safari ni ndefu kwenu na kwamba hamwezi kuibeba, kwa sababu eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua kama patakatifu pake ni mbali kwenu, basi, wakati Yahwe Mngu anawabariki,
25mtabadilisha sadaka katika pesa. Fungeni pesa kwenye mkono, na nendeni kwenye eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua.
26Huko mtatumia pesa kwa chochote mnatamani kwa ng'ombe au kondoo, au kwa mvinyo, au kwa kinywaji imara, au kwa chochote mnatamani; mtakula hapo mbele ya Yahwe Mungu wenu, na mtafurahi, nyie na nyumba zenu.
27Mlawi ambaye yuko malangoni mwenu- msimsahau, kwa kuwa hana sehemu wala urithi pamoja nanyi.
28Mwisho mwa kila miaka mitatu mtawasilisha mafungu yote ya kumi ya mazao kwa mwaka huo huo, na mtatunza katika malango yenu;
29na Mlawi, kwa sababu hana sehemu wala urithi pamoja nanyi, na mgeni, na yatima, na wajane walio ndani ya malango yenu, watakuja na kula na kurithika. Fanya hivyo kwa Yahwe Mungu wenu aweze kuwabariki katika kazi zote za mikono yenuo mnazofanya.