Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Torati

Torati 12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Hizi ni amri na sheria ambazo mtazishika katika nchi ambayo, Yahwe Mungu wa baba zenu, amewapa kumiliki, siku zote mnazoishi kwenye ardhi.
2Hakika mtaharibu maeneo yote ambapo mataifa mtakayofukuza miungu yao walioabudu, kwenye milima mirefu, kwenye vilima, na chini ya kila mti wa kijani.
3Na mtazivunja madhabahu zao chini, mtaharibu kwa vipandepande nguzo zao za mawe, na kuchoma ncha za Asherahi, mtazikata sanaa za kuchongwa za miungu yao na kuangamiza jina lao nje ya eneo hilo.
4Hamtamwabudu Yahwe Mungu wenu kama hivyo.
5Lakini kwa eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua kutoka makabila yenu kuweka jina lake, hapo patakuwa ni eneo analoishi na huko ndiyo mtaenda.
6Ni huko ndiko mtaleta sadaka ya kutekeketezwa, dhabihu zenu, zaka zenu, na sadaka zinazotolewa kwa mkono wenu, sadaka zenu za viapo, sadaka za utayari na mzao wa kwanza wa mifugo na wanyama.
7Ni huko mtakula mbele za Yahwe Mungu wenu na kufurahi kuhusu kila kitu ambacho mmeweka mkono, nyie na jamaa zenu, ambapo Yahwe Mungu wenu amewabariki.
8Hamtafanya mambo yote ambayo tunafanya hapa leo; sasa kila moja anafanya chochote kile kizuri machoni pake,
9kwa kuwa bado hamjapumzika, kwa urithi ambao Yahwe Mungu wenu anawapa.
10Lakini pindi mnaenda ng'ambo ya pili ya Yordani na kuishi ndani ya nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anasababisha ninyi kurithi, na wakati awapa pumziko kutoka kwa maadui zenu wanaowazunga karibu, ili kusudi muishi kwa usalama,
11kisha itakuwa eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua kusababisha jina lake kuishi, huko mtaleta yote ninayowaamuru; sadaka za kuteketezwa, dhabihu zenu, zaka zenu, sadaka zilizotolewa kwa mkono wenu, na sadaka za chaguo lenu kwa ajili ya nadhiri mtakazotoa kwa Yahwe.
12Mtafurahi mbele za Yahwe Mungu wenu-nyie, watoto wenu, binti zenu, wajakazi wa kiume, wajakazi wa kike, na Walawi walio ndani ya lango lenu, kwa sababu hana sehemu au urithi miongoni mwenu.
13Uwe makini mwenyewe kwamba usitoe sadaka zako za kuteketezwa kila eneo unaloona;
14lakini ni katika eneo hilo ambalo Yahwe atawachagua miongoni moja kati ya makabila yenu ambalo litatoa sadaka ya kuteketezwa, na huko mtafanya kila kitu ninachokuamuru.
15Hata hivyo, mtaweza kuua na kula wanyama ndani ya malango yenu, kama mnavyotaka, kupokea baraka ya Yahwe Mungu wenu kwa ajili ya yote amewapa; na watu wasio safi na safi wote wanaweza kula, wanyama kama vile paa na kulungu.
16Lakini hamtakula damu, mtaimwaga kwenye ardhi kama maji.
17Mnaweza msile ndani ya malango kutoka kwenye zaka ya nafaka zenu, mvinyo wenu mpya, mafuta yenu au mzao wa kwanza wa mifugo au wanyama; na mnaweza msile nyama yoyote mnayoitoa dhabihu pamoja na viapo vyovyote vyenu mnafanya, wala sadaka yenu ya utayari, wala sadaka mnayotoa kwa mkono wenu.
18Badala yake, mtakula mbele ya Yahwe Mugu wenu katika eneo ambalo Yahwe Mungu atachagua- nyie, mtoto wenu, binti yenu, mjakazi wa kiume, mjakazi wa kike, na Mlawi aliye malangoni mwenu; mtafurahi mbele ya Yahwe Mungu wenu kuhusu kila kitu ambacho mnaweka mkono wenu.

19Muwe makini wenyewe ili kwamba msimwache Mlawi maadamu mnaishi kwenye nchi yenu.
20Wakati Yahwe Mungu wenu apanua mipaka yenu, kama alivyowaahidi, na kusema, “Nitakula nyama,” kwa sababu ya tamaa zenu mnakula nyama, mnaweza kula nyama, kama tanmaa za roho zenu.
21Kama eneo ambalo Yahwe Mungu wenu achagua kuliweka jina lake ni mbali kutoka kwenu, basi mtaua baadhi ya mifugo yenu na wanyama wenu ambao Yahwe amewapa, kama nilivyowaamuru: hivyo mnaweza kula ndani ya malango yenu, kama tamaa za roho zenu.
22Kama paa na Kulungu wanaliwa, hivyo mtakula watu wasio safi na wasafi wanaweze kula kadhalika.
23Lakini muwe na uhakika kwamba hamtumii damu, kwa kuwa damu ni uhai, hamtakula uhai pamoja na nyama.
24Hamtakula, mtaimwaga nje kwenye ardhi kama maji.
25Hamtakula, ili kwamba iweze kuwa vizur kwenu, na watoto wenu baada yenu, wakati mtafanya kile kilicho sahihi machoni pa Yahwe.
26Lakini mambo ambayo ni ya Yahwe ambayo mnayo na sadaka za viapo vyenu-mtachukua hizi na kwenda eneo ambalo Yahwe achagua.
27Hapo mtatoa sadaka ya kuteketekezwa, nyama na damu, kwenye madhabahu ya Yahwe Mungu wenu, damu ya dhabihu zenu itamwangwa nje kwenye madhabahu ya Yahwe Mungu wenu, na mtakula nyama.
28Mchunguze na msikilize haya maneno yote ambayo - ninawaamuru, ili iwe uzuri kwenu na watoto wenu baada yenu milele, wakati mnafanya kile kilicho kizuri na sawa machoni pa Yahwe Mungu wenu.
29Wakati Yahwe Mungu wenu anapunguza mataifa kutoka kwenu, wakati mnaingia kuwafukuza, na mnawafukuza na kuishi katika nchi yao,
30muwe makini wenyewe ili kwamba msinaswe kwa kuwafuata, baada ya kuangamizwa kutoka kwenu kunaswa katika kuchunguza miungu yao, katika kuuliza, “Kwa namna gani haya mataifa yanaabudu muingu yao? Nitafanya hivyo hivyo.
31Hautafanya hivyo katika kumheshimu Yahwe Mungu wako, kwa kuwa kila kitu ambacho ni chukizo kwa Yahwe, mambo ambayo anayachukia- wamefanya haya na miungu yao, hata mnateketeza vijana wao na binti zao kwenye moto kwa ajili ya miungu yao.
32Chochote ninakuamuru, chunguza. Usiongeze juu yake au kupunguza.