Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Torati

Torati 30

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Vitu hivi vitakavyokuja juu yako, baraka na laana nilizoziweka mbele yako, na utakapozirejea akilini miongoni mwa mataifa mengine ambapo Yahwe Mungu wako kawapeleka,
2na utakapomrudia Yahwe Mungu wako na kutii sauti yake, na kufuata yote ambayo nayokuamuru leo – wewe na watoto wako – kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote,
3kisha Yahwe Mungu wako atageuza kutekwa kwako na kukuhurumia; atawarudisha na kuwakusanya kutoka kwa watu wote ambapo Yahwe Mungu wako aliwatawanya.
4Iwapo yeyote ya watu walio uhamishoni wapo katika sehemu za mbali sana chini ya mbingu, kutoka huko Yawhe Mungu wako atawakusanya, na kutoka huko atawarejesha.
5Yahwe Mungu wako atawaleta katika nchi ambayo mababu zenu walimiliki, nanyi mtaimiliki tena; atawatendea mema na kuwazidisha zaidi ya alivyofanya kwa mababu zenu.
6Yahwe Mungu wako atatahiri moyo wako na moyo wa uzao wako, ili umpende Yahwe Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote, ili kwamba uweze kuishi.
7Yahwe Mungu wako ataweka laana hizi zote kwa maadui zako na kwa wote wakuchukiayo, wale waliokutesa.
8Utarudi na kutii sauti ya Yahwe, nawe utatenda amri zake zote ambazo ninakuamuru leo.
9Yahwe Mungu wako atakufanikisha katika kazi yote ya mkono wako, katika matunda ya mwili wako, katika matunda ya mifugo yako, na katika matunda ya nchi yako, kwa mafanikio; kwa maana Yahwe atafurahia tena mafanikio yako, kama alivyofurahia kwa baba zako.
10Atafanya hivi iwapo utatii sauti ya Yahwe Mungu wako, ili kuzishika amri zake na kanuni zake zilizoandikwa katika kitabu hiki cha sheria, iwapo utamgeukia Yahwe Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote.
11Kwa maana amri hii nayokuamuru leo sio ngumu sana, wala haipo nje ya uwezo wako kufikia.
12Haipo mbinguni, ili usije ukasema, “Nani atayekwenda kwa ajili yetu mbinguni na kutuletea kwetu na kutufanya tuisikie, ili tuweze kutekeleza?”
13Wala haipo ng’ambo ya bahari, ili usije ukasema, “Nani atakwenda ng’ambo ya pili ya bahari kwa ajili yetu na kutuletea kwetu na kutufanya tuisikie, ili tuweze kuifanya?”
14Lakini neno lipo karibu sana kwako, katika kinywa chako na moyo wako, ili uweze kutekeleza.
15Tazama, leo nimeweka mbele yako uzima na wema, mauti na uovu.
16Iwapo utatii maagizo ya Yahwe Mungu wako, ambayo ninakuamuru leo kumpenda Yahwe Mungu wako, kutembea katika njia zake, na kushikilia amri zake, kanuni zake, na sheria zake, utaishi na kuongezeka, na Yahwe Mungu wako atakubariki katika nchi ambayo unaingia kumiliki.
17Lakini moyo wako ukigeuka, na usisikilize na badala yake unavutwa na kusujudia miungu mingine na kuwaabudu,
18basi leo nakutangazia kwako ya kwamba hakika utaangamia; siku zako hazitaongezeka katika nchi unayoipita juu ya Yordani kuingia na kumiliki.

19Naziita mbingu na nchi kushuhudia dhidi yako ya kuwa nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; kwa hiyo chagua uzima ili kwamba uweze kuishi, wewe na uzao wako.
20Fanya hivi ili umpende Yahwe Mungu wako, kutii sauti yake, na kung’ang’ania kwake. Kwa maana yeye ni uzima wako na urefu wa siku zako; fanya hivi ili kwamba uweze kuishi katika nchi ambayo Yahwe aliapa kwa mababu zako, kwa Abrahamu, kwa Isaka, na kwa Yakobo, kuwapatia.