Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Torati

Torati 9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Sikiliza, Israeli; umekaribia kuvuka ng'ambo ya pili ya Yordani leo, kuyafukuza mataifa yenye nguvu na ushujaa kuliko ninyi, na miji ambayo ni mikuu na yenye boma iliyoenda juu,
2watu wakuu na warefu, wana wa Anakimu, ambaye mnamjua, na yule mliomsikia watu wakisema, 'Nani atasimama mbele ya wana wa Anak?
3Kwa hiyo tambua leo kwamba, Yahwe Mungu wenu ni yeye ambaye huenda mbele yenu kama moto uwalao; atawaharibu na kuwaangamiza mbele yenu, kwa hiyo mtawaondosha na kuwafanya kuwapoteza kwa haraka, kama Yahwe alivyosema kwenu.
4Msiseme kwenye mioyo yenu, baada ya Yahwe Mungu wenu kuwatupilia toka mbele yenu, “ilikuwa kwa sababu ya haki yangu kwamba Yahwe amenileta mimi kuimiliki nchi hii; kwa kuwa ilikuwa kwa sababu ya maovu ya mataifa haya kwamba Yahwe anawaondowa toka mbele yenu.
5Si kwa sababu ya uadilifu wenu au unyofu wa mioyo yenu ambayo mnaenda kuingia kumiliki nchi yao, lakini ni kwa sababu ya maovu ya mataifa haya ambayo Mungu anawaondowa kutoka mbele zenu, na kusudi alifanye kuwa kweli neno ambalo aliapa kwa mababu zenu, Ibrahimu, Isaka na Yakabo.
6Kwa hiyo tambua, kwamba Yahwe Mungu wenu awapi ninyi nchi hii nzuri kuimiliki kwa sababu ya uadilifu wenu kwa kuwa ni watu wakaidi.
7Kumbuka na msisahau jinsi mlivyomchochea Yahwe Mungu wenu katika hasira huko jangwani; kutoka siku hiyo ambayo mliacha nchi ya Misri mpaka mlipokuja kwenye eneo hili, mmekuwa waasi dhidi ya Yahwe.
8Pia huko Horebu mlimchochea Yahwe katika hasira, na Yahwe alikasirika vya kutosha kwenu kuwaangamiza.
9Wakati nilipoenda juu ya mlima kupokea mbao za mawe, mbao za agano ambalo Yahwe alifanya nanyi, Nilibaki kwenye mlima kwa siku arobaini na usiku arobaini; Wala sikula mkate wala kunywa maji.
10Yahwe alinipa mbao mbili za mawe zilizoandikwa kwa kidole chake; juu yake kuliandikwa kila kitu kama tu maneno yote ambayo Yahwe alitangaza kwenu juu ya mlima toka katikati mwa moto siku hiyo ya kusanyiko.
11Ilitokea mwishoni mwa siku hizo arobaini na usiku arobaini ya kwamba Yahwe alinipa mimi mbao mbili za mawe, mbao za agano.
12Yahwe alisema nami, 'Inuka, nenda chini haraka kutokea hapa, kwa kuwa watu wako, ambao uliwaleta toka Misri, wamekuwa wafisadi wenyewe. Kwa haraka wamegeuka toka kwenye njia ambayo niliwaamuru. Wamejifanyia wenyewe umbo la kutupwa.
13Zaidi ya hayo, Yahwe alizungumza na mimi na kusema, “Nimewaona watu hawa; ni watu wakaidi.
14Acha mimi peke yangu, ili kwamba niweze kuwaangamiza na kulifuta jina lao kutoka chini ya mbingu, na nitawafanya ninyi taifa lenye nguvu na kuu kuliko wao.”
15Kwa hiyo niligeuka nyuma na kushuka chini ya mlima, na mlima ulikuwa ukiwaka moto. Mbao mbili za agano zilikuwa kwenye mikono yangu.
16Nilitazama, na tazama, mlikuwa mmefanya dhambi dhidi ya Yahwe Mungu wenu. Mmejitengenezea wenyewe ndama. Kwa haraka mmegeuka toka njia ambayo Yahwe alikuwa amewaamuru.
17Nilizichukua mbao mbili na kuzitupa toka mikononi mwangu. Nilizivunja mbele ya macho yenu.
18Tena nilala kifudifudi mbele ya Yahwe kwa siku arobaini na usiku arobaini; wala sikula mkate wala kunywa maji, kwa sababu dhambi zenu zote ambazo mlikuwa mmefanya, kwa kufanya hivyo ambavyo ilikuwa ni mbaya machoni pa Yahwe, ili kwamba kumchochea yeye katika hasira.

19Kwa kuwa nilikuwa nimeogopa hasira na gadhabu kali ambayo Yahwe alikuwa amekasirika vya kutosha dhidi yenu kuwaangamiza. Lakini Yahwe alinisikiliza mimi kwa wakati huo pia.
20Yahwe alikuwa na hasira nyingi na Aaroni kwa kusudi la kumuangamiza; pia niliomba kwa ajili ya Aaroni kwa wakati huohuo.
21Nilichukua dhambi zenu, ndama mliyekuwa mmentengeza, na kumchoma, kumpiga, kumweka chini kuwa mdogo, mpaka ilipokuwa laini kama vumbi. Nilirusha vumbi lake katika mkondo ambao ulitiririka chini kutoka mlimani.
22Huko Taberah, Massah, na huko Kibrothi Hattaavah, mlimchochea Yahwe kwenye adhabu.
23Wakati Yahwe aliwatoa kutoka Kadeshi ya Barnea na kusema, 'Nenda juu na umiliki nchi ambayo nimekupa, 'ndipo mliasi dhidi ya agizo la Yahwe Mungu wenu, na hamkumwamini na kumsikiliza sauti yake.
24Mmekuwa waasi dhidi ya Yahwe toka siku ile nilipowajua.
25Kwa hiyo nilala kifudifudi mbele ya Yahwe siku zile arobaini na usiku arobaini, kwa sababu alikuwa amesema kwamba angewaangamiza.
26Niliomba kwa Yahwe na kusema, 'Oh Bwana Yahwe, usiwaangamize watu wako au warithi wako ambao uliwaokoa kwa ukuu wako, ambapo uwatoa toka Misri kwa mkono wa uweza.
27Akilini waite watumishi wenu Ibrahimu, Isaka, na Yakobo; msiangalie ukaidi wa watu hawa, wala maovu yao, dhambi zao,
28ili kwamba nchi ambayo ulitutoa iseme, “Kwa sababu Yahwe hakuweza kuwaleta katika nchi aliyowaahadia, na kwa sababu aliwachukia, amewaleta nje kuwauwa katika jangwa.
29Bado ni watu wa kwenu na urithi wenu, ambao uliwatoa kwa nguvu zako kuu na kwa kuonesha mamlaka yako,