Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Torati

Torati 33

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Hii ni baraka ambayo Musa mtu wa Mungu aliwabariki watu wa Israeli kabla ya kifo chake.
2Alisema: Yahwe alikuja kutoka Sinai na akainuka kutoka Seiri juu yao. Aling'ara kutoka mlima wa Paramu, na akaja na elfu kumi ya watakatifu. Katika mkono wake wa kuume radi zilimulika.
3Kweli, anawapenda watu; watakatifu wake wote wapo mikononi mwako, na walimsujudu mguuni mwake; walipokea maneno yako.
4Musa alituamuru sheria, urithi kwa kusanyiko la Yakobo.
5Kisha pakawa na mfalme Yeshurumu, pale ambapo wakuu wa watu walipokusanyika, makabila yote ya Israeli pamoja.
6Acha Rubeni aishi na asife, lakini wanaume wake wawe wachache.
7Hii ni baraka ya Yuda. Musa akasema: Sikiliza sauti ya Yuda, Yahwe, na umlete kwa watu wake tena. Mpiganie; kuwa msaada dhidi ya maadui wake.
8Kuhusu Lawi, Musa akasema: Thumimu yako na Urimu yako ni ya mtakatifu wako, yule uliyemjaribu kule Masa, ambaye ulishindana naye katika maji ya Meriba.
9Mtu aliyesema juu ya baba na mama yake, “Sijawaona.” Wala hakuwatambua kaka zake, wala hakuzingatia juu ya watoto wake wenyewe. Kwa maana alilinda neno lako na kushika agano lako.
10Anafundisha Yakobo maagizo yako na Israeli sheria yako. Ataweka ubani mbele yako na sadaka kamili ya kuteketezwa juu ya dhabahu lako.
11Bariki mali zake, Yahwe, na kubali kazi ya mikono yake. Vunja viuno vya wale wanaoinuka dhidi yake, na wale watu wanaomchukia, ili wasiinuke tena.
12Kuhusu Benyamini, Musa akasema: Yule anayependwa na Yahwe anaishi kwa usalama kando yake; Yahwe anamkinga siku nzima, naye huishi katikati ya mikono ya Yahwe.
13Kuhusu Yusufu, Musa akasema: Nchi yake na ibarikiwe na Yahwe na vitu vya thamani vya mbinguni, na umande, na kina kilalacho chini.
14Nchi yake na ibarikiwe na vitu vya thamani mavuno ya jua, na vitu vya thamani mazao ya miezi,
15kwa vitu vizuri vya milima ya zamani, na kwa vitu vya thamani vya milima ya milele.
16Nchi yake ibarikiwe na vitu vya thamani vya ardhi na wingi wake, na kwa mapenzi mema ya yule aliyekuwa kichakani. Baraka na ifike juu ya kichwa cha Yusufu, na juu ya kichwa cha yule aliyekuwa mwana wa mfalme kwa kaka zake.
17Mzawa wa kwanza wa ng’ombe, katika utukufu wake, na pembe zake ni pembe za ng’ombe mwitu. Kwa hawa atawasukuma watu, wote, hadi mwisho wa ulimwengu. Hawa ni maelfu makumi ya Efraimu; hawa ni maelfu wa Manase.
18Kuhusu Zabuloni, Musa alisema: Furahi, Zabuloni, katika kutoka kwako, na wewe, Isakari, katika mahema yako.

19Watawaita watu hadi milimani. Huko watatoa sadaka za utakatifu. Maana watanyonya wingi wa bahari, na mchanga wa ufukweni.
20Kuhusu Gadi, Musa alisema: Abarikiwe yule amkuzaye Gadi. Ataishi pale kama simba jike, naye atanyakua mkono au kichwa.
21Alitoa sehemu nzuri kwake mwenyewe, maana kulikuwa na fungu la ardhi la kiongozi lililohifadhiwa. Alikuja na vichwa vya watu. Alitekeleza haki ya Yahwe na maagizo yake pamoja na Israeli.
22Kuhusu Dani, Musa alisema: Dani ni mwana wa simba arukaye kutoka Bashani.
23Kuhusu Naftali, Musa alisema: Naftali, aliyeridhika na fadhila, na kujaa kwa baraka za Yahwe, miliki nchi iliyopo magharibi na kusini.
24Kuhusu Asheri, Musa alisema: Abarakiwe Asheri Zaidi ya watoto wengine wa kiume; naye akubalike kwa kaka zake, na achovye mguu wake ndani ya mafuta ya zeituni.
25Vyuma vya mji wako na viwe chuma na shaba; kama vile siku zako zitakavyokuwa, ndivyo usalama wako utakavyokuwa.
26Hakuna aliye kama Mungu, Yeshurumu – aliyekamili, anayeendesha katika mbingu kukusaidia, na katika utukufu wake juu ya mawingu.
27Mungu wa milele ni kimbilio, na chini yake kuna mikono ya milele. Husukuma adui mbele yako, naye alisema, “Angamiza!”
28Israeli waliishi katika usalama. Wana wa Yakobo walikuwa salama katika nchi ya nafaka na divai mpya; hakika, mbingu na idondoshe umande juu yake.
29Baraka zako ni nyingi, Israeli! Nani kama wewe, watu waliokombolewa na Yahwe, ngao ya msaada wako, na upanga wa utukufu wako? Maadui zako watakuja kwako kwa kutetemeka; utakanyanga sehemu zao zilizoinuka.