5Usiogope, maana Mimi niko pamoja na wewe; Nitawarudisha watoto wako kutoka mashariki, na kuwakusanya nyie kutoka magharibi.
6Nitasema na kaskazini, 'Wakabidhini wao; na kwa kusini, Usiangalie ya nyuma; Leteni vijana wangu kutoka mbali na binti zangu kutoka vijiji vya mikoani katika nchi,
7yeyote aitwe kw jina langu, niliyemuumba kwa utukufu wangu mwenyewe, Niliyemuumba, ndio, Mimi niliyemfanya.
8Waleteni nje watu ambao ni vipofu, hata kama wana macho, na viziwi, hata kama wana masikio.
9Mataifa yote yatakusanyika kwa pamoja na watu watakusanyika. Ni nani miongoni mwenu atakaye tamka na kutangaza kutumia mambo ya mwanzo? Waache walete mashahidi kuwashuhudia wao kama wako sahihi, waache wasikilize na kuthibitisha, 'kama ni kweli'.
10Ninyi ni mashahidi wangu, ametangaza Yahwe, ''na watumishi wangu niliowachagua, ili uweze kujua na kuniamini mimi, na kuelewa kwamba mimi ndiye. Kabla yangu hapana mungu mwingine aliyeumbwa, na wala hatatoke baada yangu.
11Mimi, Mimi Yahwe, na hakuna Mkombozi zaidi yangu.