Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Isaya

Isaya 39

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Katika mda ule Merodaki mtoto wa Baladani, mfalme wa Babeli, alituma zawadi na barua kwa Hezekia; maana alisikia Hezekia alikuwa anaumwa na amepona.
2Hezekia alifurahishwa na hivi vitu; alimuonyesha mjumbe nyumba ya ghala la vitu vya thamani- vitu kama fedha, dhahabu, viungo, na mafuta ya thamani, ghala la kuwekea silaha zake, na vitu vyote vilivyopatikana kwenye stoo yake. Hapakuwa na kitu katika nyumba yake, wala ufalme wake wote, Hezekia hakuwaonyesha wao.
3Basi Isaya nabii alikuja kwa mfalme Hezekia na kumuuliza, ''Je watu hawa wamekuambia nini? wametoka wapi?, ''Wamekuja kwangu kutoka mbali nchi ya Babeli.''
4Isaya akamuuliza je ni vitu gani walivyoviona katika nyumba yako? Hezekia akajibu, ''Wameona kila kitu katika nyumba nyangu. Hakuna kitu miongoni mwa vitu vyangu vya thamani ambavyo sijawaonyesha.''
5Basi Isaya akamwambia Hezekia, ''Sikiliza neno la Yahwe wa majeshi:
6'Tazama siku inakaribia kuja pale kila kitu katika nyumba yako, vitu ambavyo mababu zako wamevihifadhi mbali mpaka mda huu wa sasa Vitapelekwa Babeli. Hakuna kitakachobakizwa, asema Yahwe.
7Na watoto watazaliwa kutoka kwako, ambao wewe mwenyewe utawazaa- watachukuliwa mbali, na watakuwa matoashi katika jumba la mfalme wa Babeli.''
8Basi Hezekia akamwambia Isaya, ''Neno la Yahwe alilolizunumza ni zuri.'' Maana alifikiria, ''Patakuwa na amani na utulivu katika siku zangu.''