Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Isaya

Isaya 57

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Wenye waki watatoweka, lakini hakuna mtu atakayelitia maanani, na watu wa agano la kuaminika wamekusanyika mbali, lakini hakuna mtu anayefahamu kuwa wenye haki wamekusanyika mbali na maovu,.
2Wameingia katika amani; wamepumzika katika vitanda vyao, wale wanotembea katika haki.
3Lakini njooni hapa, enyi watoto wa wachawi, watoto wa wazinifu na mwanamke anayefanya ukahaba.
4Ni nani mnayemfanyia mzaha? dhidi ya wale wanofungua midomo yao na kutoa nje ndimi zao? Je ninyi sio watoto wa uaasi, watoto wa uongo?
5Enyi unaowasha wenywe kwa kulala pamoja chini ya mualoni, kila chini ya mti mbichi, ewe unaeua watoto wako katika mabonde yaliyokauka, chini ya miamba inayoning'inia.
6Miongoni mwa vitu vilaini katika bonde la mto ni mambo uliyopewa uyafanyie kazi. Ni vitu vya ibada yako. Umemwaga nje kinywaji chako kwao na kutoa sadaka ya mazao. Katika haya mambo Je ninaweza kuwa radhi na mambo haya?
7Umeandaa kitanda chako juu ya mlima mrefu; pia umeeda pale juu kutoa sadaka.
8Nyuma ya mlango na mihimili ya milango umeweka ishara zako; umeniweka mimi furagha, umejifunua wewe mwenywe, na kwenda juu; umekifanya kitanda changu kuwa kikubwa. Umefanya agano na wao; ulipenda vitanda vyao; uliona sehemu zao za siri.
9Ulienda kwa Moleki pamoja na mafuta; umeongeza marashi. Ulimtuma balozi wako mbali sana; Alikwenda chini kuzimu.
10Ulichoka kwa safari yako ndefu, lakini haukusema, ''Haina matumaini.'' Umeyatafuta maisha katika mkono wako; Hivyo basi haukudhoofika.
11Ni uliyemuogopa? Ni nani uliye muhofia zaidi ambaye aliyekufanya wewe kutenda udanganyifu, kwa wingi namna hiyo ambapo hauwezi kunikumbuka mimi au kufikiria kuhusu mimi? Maana nilikuwa kimya kwa mda mrefu, hauniogopi mimi tena.
12Nitatangaza matendo haki yako na nitawaambia kila kitu ulichokifanya, lakini hawatakusaidia.
13Utakapolia nje, wacha sanamu ulizozikusnya zikusaidie wewe. Badala yake upepo utavipeperusha vyote, punzi itavipeperusha mbali. Lakini yeye anayenikimbilia mimi atairithi aridhi na atachukua umiliki katika mlima wangu mtakatifu.
14Atasema, 'Jenga, jenga! safisha njia! ondoeni vizuizi vyote katika njia ya watu wangu!''
15Maana yeye allye juu palipoinuka, anayeishi katika uzima wa milele, ambaye jina lake ni mtakatifu, asema hivi, ''Ninaishi mahali pa juu na mahali patakatifu pamoja na yeye pia aliyemnyenyekevu na moyo uliopondeka, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu na kufufua mioyo ya wanaojutia.
16Maana sitawahukumu milele, wala sitakuwa na hasira milele, Kisha roho ya mtu itazimia mbele yangu, maisha niliyowafanyia.
17Kwa sababu ya dhambi ya mapato ya vurugu zake, Nilipatwa na hasira, na nikamuadhibu yeye; niliuficha uso wangu, nilikuwa na hasira, lakini alirudi nyuma katika njia za moyo wake mwenyewe.
18Nimeziona njia zake, lakini nitamoponya yeye. Nitamuongoza yeye na kumfariji na kuwashauri wale wanomliliia yeye,

19na natengeneza tunda la midomo. Amani, amani, kwa wale walio mbali sana na wale walio karibu-asema Yahwe nitawaponya ninyi.
20Lakini waovu ni kama bahari iliyochafuka, haiwezi kutulia, na maji yake yametanda juu ya matope.
21Hakuna amani kwa wakosaji asema Mungu.''