Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Isaya

Isaya 64

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1''Oh, ikiwa umeigawa kwa kuifungua mbingu na kushuka chini! Milima inetikisika mbele yako,
2ni kama vile moto uunguzao vichaka, moto uchemshao maji. Oh, jina lako lingejulikana kwa maadui wako, na ya kwamba mataifa yangetetemeka mbele yako!
3Awali, ulipofanya mambo ya ajabu ambayo hatukuyategemea, ulishuka chini, milima ikatetemeka mbele zako.
4Tangu nyakati za kale hakuna hata mmoja aliyesikia au kujua, wala jicho kuona Mungu yeyote karibu yake, ni nani afanyae mambo haya kwake anayemsubiri yeye.
5Umekuja kuwasidia wale wanaofurahia kutenda yaliyo ya haki, wale wanaowaita kuwakumbusha njia zake na kumheshimu yeye. Ulipatwa na hasira tulipotenda dhambi. Katika njia zako daima tutakombolewa.
6Maana sote tumekuwa kama mmoja aliye na unajisi, na matendo yetu ya haki yamekuwa kama hedhi kali. Sote tumenyauka kama majani; maovu yetu, ni kama upepo, unaotupeperusha sisi mbali.
7Hakuna hata mmoja anayeita jina lako, hakuna anayefanya jitihada za kukushika wewe; maana umeuficha uso wako mbali na sisi na kutufanya sisi kuwa takataka katika mkono wa maovu yetu.
8Na lakini, Yahwe, wewe ni baba yetu; sisi ni udongo. Wewe ni mfinyanzi wetu; sisi ni kazi ya mkono wako.
9Usiwe na hasira kubwa, Yahwe, wala daima usikumbuke maovu dhidi yetu, tafadhali sisi sote, watu wako.
10Miji yenu mitakatifu imekuwa jangwa; Sayuni imekuwa jangwa, Yerusalemu imekuwa ukiwa.
11Hekalu letu takatifu na zuri. mahali ambapo baba zetu walikusifu wewe, limeangamizwa kwa moto, na kila kilichokuwa karibu kiliharibiwa.
12Je unawezaje kuendelea kumshika, Yahwe? Unawezaje kutulia kimya na kuendelea kutufedhehesha sisi?''