Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Isaya

Isaya 48

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Sikiliza hili, nyumba ya Jakobo, mlioitwa kwa jina la Israeli, na mmetoka katika mbegu ya Yuda; yeye akirie kwa jina la Yahwe na kumuhusisha Mungu wa Israeli, lakini sio kweli wala kwa namna ya haki.
2Maana wanajiita wenyewewatu wa mji mtakatifu na kumuamini Mungu wa Israeli; Yahwe wa majeshi ndilo jina lake.
3''Nimetangaza vitu kutoka siku nyingi; Wamekuja nje kutoka mdomoni mwangu, na nimewafanya wajulikane; halafu gafla nimewafanyia, na yakatimia.
4Kwa sababu nilijua kwamba wewe ni mkaiidi, misuli ya shingo yako ni kama ya chuma, na paji la uso ni kama shaba,
5Hivyo basi nilitangaza vitu hivi kabla havijatokeo hivyo, nilikujulisha wewe, 'Sanamu yangu imefanya haya au sanamu yangu ya kuchonga na sanamu yangu ya kuyeyusha, yamekwishisha vitu.
6Umesikia kuhusu mambo haya; angalia ushahidi wote; na wewe, Je hautakubali kwamba ninacho kisema ni cha kweli? Kuanzia sasa na kuendelea Nitawaonyesha vitu vipya, mambo yaliyofichika ambayo hamkuyajua.
7Sasa, na sio yaliyopita, yamekuwa sasa, na kabla ya leo hamkusikia kuhusu wao, hivyo hautaweza kusema, 'Ndio, nilijua kuhusu wao.'
8Haukusikia; haukuelewa; haya mambo hayakufuniliwa katika masikio kabla ya. Maana nilijua kwamba umekuwa mdanganyifu, na kwamba umekuwa muasi kutoka kuzaliwa.
9Kwa niaba ya jina langu nitahairisha asira yangu, na kwa heshima yangu nitajizuia kutokumuharibu yeye.
10Tazama, Mimi niliwaandaa ninyi, lakini sio kama fedha; Nimekusafisha wewe katika tanuru la mateso.
11Kwa niaba yangu, kwa niaba yangu nitafanya; maana ni kwa jinsi gani niruhusu jina langu lisiheshimike? Sitampa utukufu wangu mtu yeyote.
12Nisikilize mimi, Yakobo, na Israeli niliyekuita: Mimi ndiye; Mimi ni wa kwanza, na pia wa mwisho.
13Ndio, mkono wangu umeweka msingi wa nchi, na mkono wangu wa kuume ulizitawanya mbingu, zimesimama juu kwa pamoja.
14Jikusanyeni wenyewe, nyinyi nyote, na sikilizeni; ni nani miongoni mwenu atangazaye mambo haya? Yahwe atakamilisha lengo lake dhidi ya Babeli. Atachukua mapenzi ya Yahwe dhidi ya wa Wakaldayo.
15Mimi, nimezungumza, ndio, nimemchagua yeye, nimemleta yeye, na yeye atafanikiwa.
16Sogea karibu na mimi, sikiliza hili; kutoka mwanzo sikuzungumza katika siri; lakini ilipotokea, Mimi niko hapa; na sasa Bwana Mungu amenituma mimi, na Roho wake.''
17Yahwe asema hivi, Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli anasema, ''Mimi ni Yahwe Mungu wenu, ninayewafundisha juu ya kufanikiwa, ninayewaonyesha njia mtakayoiptia.
18Ikiwa kama mtaheshimu amri zangu! Hivyo amani na maendeleo yatatiririka kama mto, na wokovu wenu ni kama mawimbi kwenye bahari.

19Watoto wako watakuwa wengi kama mchanga, na watoto kutoka kwenye tombo zenu watakuwa wengi kama nafaka kwenye mchanga; majina yao hayataondolewa wala kufutwa mbele yangu.
20Tokeni nje ya Babeli! wakimbieni Wakaldayo! kwa sauti ya kupiga kelele tangaza kwamba! hakikisha hili linajulikana, hakikisha hili linafika mpaka miisho ya nchi! sema 'Yahwe amemkomboa Yakobo mtumishi wake.
21Hawakupatwa na kiu alipowaongoza katika jangwa, alifanya maji kutokea kwenye mwamba kwa ajili yao; aliugawa na kufungua mwamba, na maji yakatoka nje.
22Hakuna amani kwa watenda makosa- amesema Yahwe.''