Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Isaya

Isaya 12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Siku hiyo utasema, ''Nitakushukuru wewe, Yahwe. Japo ulikuwa na hasira na mimi, laana yako imeondoka mbali, na umenifariji mimi,
2Ona Bwana ni wokovu wangu; nitamwamini na sitakuwa na hofu, kwa Yahwe, ndio, Yahwe ni nguvu yangu na wimbo wangu. Amekuwa wokovu wangu.''
3Kwa furaha utachota maji kwenye kisima cha wokovu.
4Siku hiyo utasema, ''Mshukuru Yahwe na ita jina lake; tangaza matendo yake miongoni mwa watu, tangaza jina lake limeinuliwa.
5Mwiimbie Yahwe, maana ametenda matendo yaliotukuka; acha hili lijulikane dunia nzima.
6Lia kwa nguvu na piga kelele kwa furaha, enyi wakazi wa Sayuni, maana katikati yenu ni mtakatifu wa Israeli.