Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Isaya

Isaya 63

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ni nani ajaye kutoka Edomu, aliyevaa mavazi rangi nyekundu kutoka Bozra? Ni nani aliye katika mavazi ya kifahari, anayetembea kwa kujiamini kwa sababu ya ukuu wa nguvu zake? Ndiye mimi, nizungumzae haki na uwezo mkubwa wa kuokoa.
2Kwa nini umevaa mavazi ya rangi nyekundu, na kwan nini wanaonekana kama akanyagae mizabibu katika vyombo vyake.
3Nimekanyaga zabibu lililoko katika vyombo vyenyewe, na hakuna hata mmoja kutoka mataifa aliyeungana na mimi. Niliwakanyaga kwa hasira yangu na niliwakanyaga wao kwa hasira yangu. Damu zao zimeruka katika nguo zangu na kuweka madoa nguo zangu zote.
4Maana niliangalia mbele katika siku ya kisasi, na mwaka wa ukombozi ulikwishawadia.
5Mimi nilitazama, na hapo hapakuwa na mtu mmoja hata wa kutoa msaada, lakini mkono wangu mwenywe uliniletea ushindi mimi, na hasira yangu kubwa iliniongoza mimi.
6Niliwakanyaga watu wangu chini kwa hasira yangu na kuwafanya wao wanywe laana yangu, na nilimwaga damu zao juu ya nchi.
7Nitakusimulia matendo ya agano la Yahwe lenye kuaminika, matendo ya kusifu ya Yahwe. Nitawasimulia yote ambayo Yahwe ametutendea sisi, na ukuu wa uzuri wake katika nyumba ya Israeli. Huruma hii aliyetuonyesha sisi kwa sababu ya rehema zake na matendo ya agano lake la kuaminika.
8Maana alisema, ''Baadhi yao ni watu wangu, watoto ambao sio waaminifu.'' Amekuwa mwokozi wao.
9Kupitia mateso yao yote, aliteseka pia, na malaika kutoka mbele yake aliwaokoa wao. Katika upendo wake na rehema aliwakomboa wao, na aliwanyanyua juu na aliwabeba wote katika kipindi chote cha kale.
10Lakini walimuasi na kumuuzunisha roho mtakatifu. Hivyo basi akkawa adui wao na kupigana dhidi yao.
11Watu wake walifikiri kuhushu nyakati za kale za Musa. Walisema, ''Yuko wapi Mungu, aliyewaleta juu nje ya bahari pamoja na mchungaji wa kundi lake? Yuko wapi Mungu, ambaye aliyeweka roho mtakatifu mwiongoni mwenu?
12Yuko wapi Mungu, aliyeufanya wingi wa utukufu wake kwenda katika mkono wa kuume wa Musa, na ukaganya maji mbele yao, kulifanya jina lake milele yeye mwenyewe?
13Yuko wapi Mungu, aliyewaongoza katika maji mengi? Kama farasi anayekimbia kwenye aridhi ambayo ni tambarare, hawakua na mashaka.
14Kama ng'ombe anayeshuka chini kwenye bonde, Roho ya Yahwe imewapa punziko. Hivyo umewaongoza watu wako, kufanya wewe mwenyewe jina la kusifu.
15Tazama chini kutoka mbinguni na pata taarifa kutoka kwenye makao ya utukufu wako. Iko wapi bidii yenu na matendo makuu? Uruatendo yako ya uruma yamezuiliwaa kutoka kwetu.
16Maana wewe n baba yetu, Japokuwa Ibrahimu hatujui sisi, na Israeli haitutambui sisi, wewe, Yahwe, wewe ni baba yetu. Mkombozi wetu limekuwa jina lako kutoka nyakati za kale.
17Yahwe, kwa nini unatufanya tangetange na kuifanya mioyo yetu kuwa migumu, hivyo hatukukuheshimu wewe? Rudi kwa niaba ya watumishi wako, kabila la urithi wako.
18Watu wako walirithi mahali patakatifu kwa mda mfupi, halafu maadui zetu waliwakanyaga.

19Tumekuwa kama juu ya wale ambao hawajawai kuongoza, kama wale ambao hawajaitwa kwa jina lako.