1Angalia Yahwe anakaribia kuifanya dunia kuwa utupu, kuhiharibu, kuharibu uso wake, na kuwatawanya wenyeji wake.
2Itakuwa kama ilivyo kwa watu itakuwa hivyo hivyo kwa kuhani; na kwa watumishi na kwa bwana wake, na kwa mfanyakazi wa ndani itakuwa hivyo na kwa tajiri yake, ndivyo itakavyokuwa kwa anayeuza na anayenunua; ndivyo itakavyokwa kwa wenye kupata faida na wenye madeni, na wale wennye kupokea faida itakuwa hivyo hivyo kwa wale wenye kutoa faida.
3Dunia itaharibiwa kabisa na kufanjwa ukiwa; maana Yahwe amenena maneno hayo. Dunia imekauka kabisa na kunyauka,
4Dunia inazimia n kudhohofika. Watu maarufu wa duniani watapotezwa.
5Dunia inavutwa na watu wakao ndani yake kwa sababu wamepindisha sheria, wameibadili amri na wamevunja agano la milele.
6Hivyo basi laana inaitafuna nchi, na wenyeji wake wamekutwa na makosa. Wakaao duniani wanateketea, na watu wachache wameachwa.
7Divai mpya imekauka, mizabibu imenyauka, na mioyo yote iliyochangamka inaugua.
8Sauti ya furha ya kigoma inasimama, na kelele za wenye furaha zimekwisha, na furaha ya kinubi imesitishwa.
9Hawatakunjwa mvinyo tena na kuimba, bia chungu kwa wale wanokunywa.
10Mji uliochafuka umeangushwa chini; kila nyumba imefungwa na hakuna kitu.
11Kuna kilio mtaani kwa sababu ya mvinyo; furaha yote imetiwa giza, furaha ya nchi imetoweka.
12Ndani ya mji kumebaki ukiwa, na lango limebolewa kwa uharibifu.
13Hivi ndivyo itakavyofanyika kwa dunia yote mwiongoni mwa mataifa, pale mti wa mzabibu utakapopigwa, na waokotapo zabibu baada mavuno yake kuwa tayari.
14Watanyanyua saut zao na kupiga keleleYahwe mwenye enzi, na utapaza sauti kutoka kwenye bahari.
15Hivyo basi mashariki mtukuze Yahwe, na katika kisiwa cha bahari tukuzeni jina la Yahwe, Mungu wa Israeli.
16Kutoka umbali wa sehemu ya dunia tumesika nyimbo, ''Utukufu kwa watu wenye haki! Lakini nikasema, ''Nimepita mbali, Ole juu wangu! Wasaliti walshulika na wenye hila; ndio, wasaliti walishuhulika na wenye hila.''
17Hofu, shimo, na mtego yako juu yako, wenyeji wa dunia.
18Amekimbia maana sauti ya hofu itaanguka kwenye shimo, na anayekuja juu katikati ya shimo atanaswa na mtego. Madirisha ya mbinguni yatafunguliwa, na misingi ya dunia itatikisika.
19Dunia itangamizwa kabisa, dunia itapasukia mbali; dunia itatatikisika vikali.
20Dunia itajikongoja kama mlevi na itachezacheza kurudi nyuma na mbele kama kibanda. Dhambi zao zitakuwa nzito juu yao na zitaanguka na hazitasimama tena.
21Itakuwa siku hiyo ambayo Yahwe ataliadhibu jeshi la aliye juu mahali pa juu, na falme za dunia katika dunia.
22Watakusanyika pamoja, wafungwa katika shimo, na watafungw gerezani; na baada ya siku nying watadhibiwa.
23Halafu Mwenzi utatiwa aibu na jua pia litatwa aibu, maana Yahwe wa majeshi atatawala katika mlima Sayuni na Yerusalemu, kabla ya wazee wake katika utukufu.