1Vitu ambavyo Isaya mtoto Amozi alivijua katika maono, kuhusu Yuda na Yerusalemu.
2Na itakuwa katika siku za mwisho, ule mlima wa nyumba ya Yahwe itaanzishwa kama mlima mrefu zaidi, na utanyanyuliwa juu ya vilima, na mataifa yote yatakusanyika pale.
3Watu wengi watakuja na kusema, ''Njooni, twendeni juu ya mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo, kwa hiyo anaweza kutufundisha baadhi ya njia zake na tunaweza kutembea katika njia zake.'' Nje ya Sayuni itaenda sheria na neno la Yahwe litatoka Yerualemu.
4Atahukumu kati ya mataifa na atatoa maamuzi kwa watu wote; watayapiga nyungo mapanga yao kuwa majembe, na mikiku yao kama ya kukatia ndoano; taifa halitanyanyua upanga juu ya taifa lingine, na wala hawata jiandaa kwa vita tena.
5Nyumba ya Yakobo, njooni, na tutembee katika mwanga wa Yahwe.
6Kwa maana mmewatekeleza watu wenu, nyumba ya Yakobo, wamejazwa na desturi kutoka mashariki na dalili kutokea kama mfilisti, na watasalimiana kwa mikono na wana wa wageni.
7Nchi yao imejaa fedha na dhahabu, na hakuna mipaka katika utajiri wao; nchi yao pia imejaa farasi, wala hakuna mipika ya magari.
8Nchi yao pia imejaa sanamu; wanaabu utengenezaji wa mikono yao wenyewe, vitu aambavyo vidole vyao vimetengeneza.
9Watu watainama chini, na kila mmoja atanguka chini; hivyo basi msiwanyanyue juu.
10Nendeni maeneo yenye miamba na mjifiche kwenye aridhi kwa hofu ya Yahwe na kwa utukufu wa enzi yake.
11Mtu anaye tazama kwa kujivuna atashushw chini, na kiburi cha watu kitashushwa chini, na Yahwe mwenyewe atainuliwa siku hiyo.
12Maana kutakuwa na siku ya Yahwe wa majeshi juu ya yeyote anayejigamba na kujiinua juu, na dhidi ya yeyote mwenye kiburi na atashushwa chini-
13na dhidi ya mierezi ya Lebanoni iliyo juu na kupandishwa juu, na dhidi ya mialoni ya Bashani.
14Siku hiyo ya Yahwe wa majeshi itakuwa dhidi ya milima yote mirefu, na dhidi ya vilima vyote vilivyonyanyuliwa juu,
15na dhidi ya minara mirefu, na dhidi ya kila ukutaunaojitokeza,
16na dhidi ya merikebu zote za Tarshishi, na dhidi ya vyombo vizuri vya meli.
17Kiburi cha mwanaume kitashushwa chini, na kiburi cha wanaume kitaanguka; Yahwe mwenyewe atainuliwa siku hiyo.
18Sanamu zote zitaondolewa.
19Wanaume wataingia kwenye mapango ya miamba na mashimo ya aridhi, kwa hofu ya Yahwe, na kwa utukufu wa enzi yake, atakapo nyanyuka na kuitisha nchi.
20Siku hiyo watu watatupa sanamu zao za fedha na dhahabu ambazo wametengeneza wenyewe kwa ajili ya kuabudia - watazitupa mbali kwa fuko na popo.
21Watu wataingia kwenye miamba kupitia mwanya itakuwa miamba chakavu, kwa hofu ya Yahwe na utukufu wa enzi yake,
22usimwaminia mtu, ambae pumzi yake inatokea katika pua yake, ni kwa kiasi gan?