Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Isaya

Isaya 43

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Lakini sasa haya ndio Yahwe asemayo, yeye aliyekuumba ewe, Yakobo, na yeye aliyekuumba ewe, Israeli: ''Usiogope, kwa maana nimekukomboa wewe; nmeikuita kwa jina lako, wewe ni wangu.
2Utakapopita katika maji, Nitakuwa pamoja na wewe; na katika mito, hayatakuzuru wewe. Utakapotembea katika moto hautaungua, na moto hautakuharibu wewe.
3Maana mimi Yahwe Mungu wako, Mtakatifu wa Israeli Mkombozi wenu. Nimewapa Misri kama fidia yenu, Ethiopia na Seba watabadilishana kwako.
4Kwa maana ulikuwa wa thamani na maalumu katika macho yangu, Ninakupenda; kwa sababu hiyo Nitatoa watu kwa ajili yako, na watu wengine kwa ajili ya maisha yako.
5Usiogope, maana Mimi niko pamoja na wewe; Nitawarudisha watoto wako kutoka mashariki, na kuwakusanya nyie kutoka magharibi.
6Nitasema na kaskazini, 'Wakabidhini wao; na kwa kusini, Usiangalie ya nyuma; Leteni vijana wangu kutoka mbali na binti zangu kutoka vijiji vya mikoani katika nchi,
7yeyote aitwe kw jina langu, niliyemuumba kwa utukufu wangu mwenyewe, Niliyemuumba, ndio, Mimi niliyemfanya.
8Waleteni nje watu ambao ni vipofu, hata kama wana macho, na viziwi, hata kama wana masikio.
9Mataifa yote yatakusanyika kwa pamoja na watu watakusanyika. Ni nani miongoni mwenu atakaye tamka na kutangaza kutumia mambo ya mwanzo? Waache walete mashahidi kuwashuhudia wao kama wako sahihi, waache wasikilize na kuthibitisha, 'kama ni kweli'.
10Ninyi ni mashahidi wangu, ametangaza Yahwe, ''na watumishi wangu niliowachagua, ili uweze kujua na kuniamini mimi, na kuelewa kwamba mimi ndiye. Kabla yangu hapana mungu mwingine aliyeumbwa, na wala hatatoke baada yangu.
11Mimi, Mimi Yahwe, na hakuna Mkombozi zaidi yangu.
12Nimetangaza, nimeokoa, na kutangaza, na hakuna Mungu mwingine miongoni mwenu, Ninyi ni mashahidi wangu asema Yahwe, ''Mimi ni Mungu.
13Kuanzia leo na kuendelea mimi ndiye, na hakuna hata mmoja atakayewakomboa kwenye mkono wangu. Nitafanya, na nani awezae kunizuia?''
14Yahwe asema hivi, Mkombozi wenu, yeye Mtakatifu wa Israeli: ''Kwa niaba yenu nimemtuma mjumbe kwenda Babeli na kuwaongoza wao wote chini kama watuhumiwa, kubadilisha kelele za furaha za watu wa Babeli' kuwa wimbo wa maombolezo.
15Mimi ni Yahwe, niliye Mtakatifu, Muumbaji wa Israeli, Mfalme wenu.
16Yahwe asema hivi, Ni nani aliyefungua njia katika bahari, na njia katika maji yenye nguvu,
17ni nani anayeongoza gari na farasi, majeshi na jeshi kuu. Walianguka chini kwa pamoja; hawakunyanyuka tena; wamezimwa, kama utambi unaoungua.
18Msifikirie hayo mambo yaliyopita, wala kuyafikiria mambo ya zamani.

19Tazama ninakaribia kufanya mambo mapya; sasa yanakaribia kutokea; Je humyajui haya? Nitafanya njia jangani na na mikondo ya maji katika jangwa
20Wanyama pori wa shambani wataniheshimu mimi, Mbweha na mbuni, kwa sababu ninatoa maji jangwani, na mito jangwani, ili watu wangu niliowachuga wapate kunjwa,
21Watu hawa niliowaumba mwenyewe, kwamba wahesabu tena sifa zangu.
22Lakini hamjanita mimi, Yakobo; umechoka na mimi, Israeli.
23Haujaniletea hata kondoo wako kama sadaka ya kuteketeza; na wala haujaniheshimu mimi kwa sadaka yako Sijakutumisha wewe kwa sadaka ya mazao, wala sijawachosha kwa sadaka yenu ya ubani.
24Hamkuninunulia mimi manukato mazuri kwa fedha, hakumwagia mimi mafuta ya sadaka zenu; Lakini mnanichosha mimi na dhambi zenu na mnanichosha mimi kwa matendo yenu mabaya.
25Mimi, ndio, Mimi, ndiye niliyafaye maovu yenu kwa niaba yangu mmi mwenyewe; na Sitawaita na kuwakumbusha dhambi zenu tena.
26Nikumbusheni mimi kilichotokea. Njooni tusemezane pamoja; leta hoja zako, ili kusudi uthibitishe kuwa hauna hatia.
27Baba yako wa kwanza alitenda dhambi, na viongozi wenu walitenda dhambi dhidi yangu.
28Hivyo basi Nitawatia unajisi viongozi watakatifu; Nitamkabidhi Yakobo kuwaharibu kabisa, na Israeli kulaani udhalilishaji.