Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Nyakati

2 Nyakati 36

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kisha watu wa nchi wakamchukua Yehoazi mwana wa Yosia, na wakamfanya mfalme katika nafasi ya baba yake katika Yerusalemu.
2Yehoazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala, na akatawala miezi mitatu katita Yerusalemu.
3Mfalme wa Misiri akamwondoa katika Yerusalemu, na akaitoza nchi faini ya talanta za fedha mia moja na talanta moja ya dhahabu.
4Mfalme wa Misiri akamfanya Eliakimu, ndugu yake, mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu, na akambadili jina lake kuwa Yehoakimu. Kisha akamchukua ndugu yake Eliakimu - Yeahazi na kumpeleka Misiri.
5Yehoakimu alikuwa na umri wa miaka ishini na tano alipoanza kutawala, na akatawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Akafanya ambayao yalikuwa uovu katika macho ya Yahwe Mungu wake.
6Kisha Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akamvamia na kumfunga katika minyororo kumuongoza kwenda mbali Babeli.
7Nebukadreza pia akabeba baadhi ya vitu katika nyumba ya Yahwe kwenda Babeli, na akaviweka katika ikulu yake huko Babeli.
8Kwa mambo mengine kuhusu Yehoyakimu, mambo mabaya aliyofanya, na yaliyopatikana zidi yake, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. Basi Yehoyakimu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
9Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala; alitawala miezi mitatu na siku kumi katika Yerusalemu. Akafanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe.
10Katika kipindi cha mwisho wa mwaka, mfalme Nebukadreza akatuma watu na wakampelekea Babeli, vitu vya thamani kutoka katika anyumba ya Yahwe, na kumfanya Sedekia ndugu yake, mfalame juu ya Yuda na Yerusalemu.
11Sedekia alikuwa na umri wa miaka isshirini na moja alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Akafanya yaliokuwa uovu katika macho ya Yahwe Mungu wake.
12Hakujinyenyekesha mwenyewe mbele za Yeremia nabii, ambaye alisema kutoka kwenye kinywa cha Yahwe.
13Sedekia pia akaasi zidi ya Mfalme Nebukadreza, ambaye alikuwa amemfanya aape uaminifu kwake kupitia Mungu. Lakini Sedekia aliishupaza shingo yake na kuufanya moyo wake mgumu usigeuke kwa Yahwe, Mungu wa Israeli.
14Vilevile, viongozi wote wa makauhanai na wa watu hawakuwa waaminifu, na waliufuata uovu wa mataiafa. Waliigoshi nyumba ya Yahwe ambayo alikuwa ameitakasa katika Yerusalemu.
15Yahwe, Mungu wa babu zao, akatuma maneno kwao tena na tena kupitia wajumbe wake, kwa sababu alikuwa na huruma juu ya watu wake na juu ya sehemu anayoishi.
16Lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, wakayadharau maneno yake, na kuwackeka manabii wake, hadi hasira ya Yahwe ilipoinuka zidi ya watu wake, hadi pailipokosekana msaada.
17Hivyo Mungu alimpeleka juu yao mfalme wa Wakaldayo, ambaye aliwaua vijana wao kwa upanga ndani ya patakatifu, na hakuwa na huruma juu ya vijana au mabikra, watu wazee au wenye mvi. Mungu akawatoa wote mikononi mwake.
18Vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, vikubwa na vidogo, hazina za nyumba ya Yahwe, na hazina za mfalme na watumishi wake—vyote hivi akavipeleka Babeli.

19Wakaichoma moto nyumba ya Mungu, wakauangusha chini ukuta wa Yerusalemu, wakachoma ikulu zake zote, na wakaharibu vitu vizuri vyote ndani yake.
20Mfalme akawapeleka mbali Babeli wale waliokuwa wameoka na upanga. Wakawa watumishi kwa ajili yake na wanawe hadi utawala wa Waajemi.
21Hili lilitokea ili kulitimiza neno la Yahwe kwa kinywa cha Yeremia, hadi nchi itakapokuwa imefurahia mapumziko ya Sabato yake. Iliishika Sabato kwa muda mrefu hadi kukataliwa kwake, ili miaka sabini itimie katika namna hii.
22Sasa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Yahwe kwa kinywa cha Yeremia liweze kutimizwa, Yahwe akaipa hamasa roho ya Koreshi, mfalme wa Uajemi, kwamba akafanya tangazo katika uflme wake wote, na akaliweka pia katika maandishi. Akasema,
23“Hivi ndivyo Koreshi, mfalme wa Uajemi, anasema: Yahwe, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia. Ameniagiza nijenge nyumbaa kwa ajili yake katika Yerusalemu, ambao upo Yuda. Yeyote aliyemiongoni mwenu kutoma katika watu wake wote, Yahwe Mungu wenu, awe naye. Aende kwenye ile nchi.”