Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Nyakati

2 Nyakati 18

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Sasa Yehoshafati alikauwa na utajiri mwingi na heshima kubwa; alifanya undugu na Ahabu mmoja wa watu wa familia yake akamuo binti yake.
2Baada ya miaka kadhaa, akashsuka chini kwa Ahabu huko Samaria. Ahabu akachinja kondoo na ngo'mbe wengi kwa ajili ya yake na watu waliokuwa pamoja naye. Ahabu pia akamshawishi kuivamia Ramothi-gileadi pamoja naye.
3Ahabu, mfalme wa Israeli, akamwambia Yehoshafati, mfalme wa Yuda, “Utakwenda Ramothi-gileadi pamoja nami?” Yehoshafati akamjibu, “Mimi ni kama wewe, na watu wangu ni kama watu wako; tutakuwa pamoja nawe katika vita.”
4Yehoshafati akamwambia mfalme wa Israeli, Tafadhali litafute neno la Yahwe kwanza kwa ajili ya jibu lako”
5Kisha mfale wa Israeli akawakusanya manabii pamoja, wanauame mia nne, na akasema akwao, Tutaenda vitani Ramothi-gileadi, au nisiende?” Wakasema, “Vamia, kwa maana Mungu ataitia mkononi mwa mfalme.”
6Lakini Yehoshafati akasema, “Hakuna nabii mwingine hapa wa Yahwe ambaye kwake tunapaswa kutafuta ushauri?”
7Mfale wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Bado kuna mtu mmoja amabaye kwake lazima tuutafute ushauri wa Yahwe, Mikaya mwana wa Imla, lakini namchukia kwa sababu yeye huwa hatabiri mema kamwe kuhusu mimi, bali kila mara maovu,” Lakini Yehoshafati akasema, “Mfalme hapaswi kusema hivyo.”
8Kisha mfalme wa Israeli akamwita akida na kusema, Haraka mlete Mikaya mwana wa Imla.”
9Sasa Ahabu mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wamekaa kila mmoja katika kiti cha enzi, wamevalia kanzu zao, katika sehemu ya uwazi katika maingilia ya lango la Samaria, na manabii wote walikuwa wakitabairi mbele zao.
10Zedekia mwana wa Kenaani akajitengenezea pembe za chuma na kusema, Yahwe anasema hivi: Kwa kutumia hizi pembe mtawasukuma Waaramu hadi waangamie.”
11Manabii wote wakatabiri kitu kile kile, wakisema, “Vamia Raamothi-gleadi na shinda. kwa maana Yahwe ameutia kwenye mkono wa mfalme.”
12Mjumbe aliyeenda kumuita Mikaya akasema kwake, akisema, “Sasa angalia, maneno ya manabii yanatangaza mambo mema kwa ajili ya mfalme kwa kinywa kimoja. Tafadhali maneno yako yawe kama maneno ya mmoja wao na sema mambo mema.”
13Mikaya akajibu, “Kama Yahwe aishivyo, mimi nitasema kile mbacho Mungu anasema.”
14Alipokuja kwa mfalme, mfamle akamwambaia, “Mikaya, tutaenda Ramothi -gileadi kwa ajili ya vita, au la?” Mikaya akamjibu, “Vamia na utashinda! kwa maana utakuwa ushinda mkuu.”
15Kisha mfalme akasema kwake, “Ni mara ngapi ninapaswa kukutaka kuapa kutoniambia kitu chochote sispokuwa kweli katika jina la Yahwe?
16Kwa hiyo Mikaya akasema, “Niliwaoana Israeli wametawanyika ktika mlima, kama kondoo wasio na mchungaji, na Yahwe akasema, hawa hawana mchungaji. Ebu kila mtu arudi nyumbani kwake kwa amani.”
17Kwa hiyo mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Sikukuambia kwamba asingeweza kutabiri mema juu yangu, bali majanga tu?
18Kisha Mikaya akasema, “Kwa hiyo ninyi nyote mnapashwa kulisikia neno la Yahwe: Nilimuon Yahwe amekaa juu ya kiti chake cha enzi, na majeshi yote ya mbinguni yalikauwa yamekaa mkono wake wa kulia na mkono wake wa kushoto.

19Yahwe akasema, Ni nani atakayemrubuni Ahabu, mfalme wa Israeli, ili kwamba aende na kuanguka huko Ramothi-gileadi?' Mmoja alisema hivi na mwingine hivi.
20Kisha roho ikaja moja kwa maja na kusimama mbele ya Yahwe na kusema, 'Nitamrubuni.' Yahwe akamwambia, 'Kivipi?'
21Roho ikajibu, “nitatoka nje na nitakuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.' Yahwe akajibu, 'utamrubuni, na pia utafanikiwa. nenda sasa na fanya hivyo.'
22Sasa ona, Yahwe ameweka roho ya uongo katika midomo ya manabii wako hawa, na Yahwe ametangaza majanga kwa ajili yako.”
23Kisha Zedekia mwana wa Kenaana, akaja, akampiga kofi mika juu ya shavu, na kusema, “Kwa njia gani Roho wa Yahwe alitoka kwangu ili aseme nawe?”
24Mika akasema, Angalia, utalijua hilo katika siku hiyo, mtakapokimbia katika baadhi ya vyumba vya ndani kwa ajili ya kujificha.”
25Mfalme wa Israeli akasema kwa baadhi ya watumishi, “Enyi watu mkamateni Mikaya na mmpeleke hadi Amoni, mkuu wa mji na, na kwa Yoashi, mwanangu.
26Nanyi mtamwambia, 'Mfalme anasema: Mweke gerezanai huyu mtu na umlishe kwa mkate kiogo tu na maji kidogo tu, mpaka nitakaporudi salama.”
27Kisha Mikaya akasema, “Kama utarudi salama, Yahwe hajasema nami.” Kisha akaongeza, “Sikiliza haya, enyi watu wote.”
28Kwa hiyo Ahabu, mfalme wa Israeli, na Yehoshafati, mfalme wa Yuda, wakaenda juu ya Ramothi-giledi.
29Mfalme wa Israeli akamwamabia Yehoshafati, “Nitajibadilisha mwenyewe na kwenda vitani, lakini wewe vaa mavazi yako ya kifalme.” Kwa hiyo mfalame wa Israeli akajibalisha, na wakaenda vitani.
30Sasa mfalme wa Aramu alikuwa amewaamuru maakida wa magari yake, akisema, Msiwavamie wanajeshsi wasio wa muhimu wala wanajeshsi muhimu. Badala yake, mvamieni mfalme wa Israeli pekee,”
31Ikawa kwamba maakida wa magari walipomuona Yehoshafati wakasema, “Yule ni mfalme wa Israeli.” Wakageka kumzunguka wamvamie, lakini Yehoshafati akalia, na Yahwe akamsaidia. Mungu akawageza nyuma kutoka kwake.
32Ikawa kwamba maakida wa magari walipoona ya kuwa hakuwa mfalme wa Israeli, wakarudi nyuma wasimfukuze.
33Lakini mtu mmoja akauvuta upinde wake kwa kubahatisha na kumpiga mfalme wa Israeli kati kati ya maungio ya mavazi yake. Kisha Ahabu akamwambia dereva wa gari lake, “Geuza nyuma na nitoe nje ya mapigano, kwa maana nimejeruhiwa vibaya sana.”
34Mapigano yakazidi kuwa makali siku hiyo, na mfalme wa israeli akashikiliwa katika gari lake kuwaelekea Waaramu hadi jioni. Muda jua lilipokaria kwenda chini, akafa.