Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Nyakati

2 Nyakati 33

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili alipoanza kutawala, alitawala miaka hamsini na tano katika Yerusalemu.
2Akafanya yalikuwa uovu katika macho ya Yahwe, kama yalivyo mambo ya machukizo ya mataifa ambao Yahwe alikuwa amewafukuza mbele ya watu wa Israeli.
3Kwa maana alizijenga tena sehemu za juu ambazo baba yake Hezekia alikuwa amezibomoa, na akajenga madhabahu kwa ajili ya mabaali, akatengeneza sanaamu za Maashera, na akaziinamia chini nyota zote za mbinguni na kuziabudu.
4Manase akajenga madhbahu za kipagani katika nyumba ya Yahwe, ingawa Yahwe alikuwa amemwamuru, “Ni katika Yerusalemu ambamo jina langu litawekwa milele”.
5Alijenga madhabahu kwa ajili ya nyota zote za mbinguni katika vile viwanja viwili vya nyumba ya Yahwe.
6Katika bonde la Beni Hinomu akawaweka wanaye katika moto. Akafanya misemo ya ubashiri, na uchawi, akassoma utabiri; akashauriana na wale waliozungumza na wafu na wale waliozungumza na na roho. Akafanaya maaovu mengi katika mcho ya Yahwe na alimfanya Mungu akasirike.
7Ile sanamu ya Maashera aliyokuwa amefanya, akaipeleka katika nyumba ya Mungu. Ni kuhusu nyumba hii ambayo Mungu alikuwa amesema kwa Daudi na Selemani mwanaye; alikuwa amesema, “Ni katika nyumba hii na katika Yerusalemu, ambao nimeuchangua kutoka makabila yote ya Israeli, kwamba nitaliweka jina langu milele.
8Sitawaondoa tena watu wa Israeli katina nchi hii ambayo niliitoa kwa babu zao, ikiwa tu watakuwa makini katika kuyashika yote niliyowaamuru, kuzishika sheria zangu, amri zangu, na sheria zangu nilizowapa kupitia Musa.”
9Manase akawaongoza Yuda na wakaaji wa Yerusalemu hata kufanya uovu zaidi kuliko hata watu wa mataifa ambao Yahwe alikuwa amewateketeza mbele za Israeli.
10Yahwe akasema kwa Manase, na kwa watu wake wote, lakini hawakumsikiliza.
11Kwa hiyo Yahwe akaleta juu yao maamri jeshsi wa jeshi la Ashuru, ambao walimchukua Manase katika minyonyoro, wakamfunga kwa pingu, na wakampeleka Babeli.
12Manase alipokuwa katika dhika, alimuomba Yahwe, Mungu wake, na akajinyenyekesha sana mbele za Mungu wa babu zake.
13Akaomba kwake; na Mungu akamsikiliza, na Mungu akasikia kuomba kwake na akamrudisha Yerusalemu, katika ufalme wake. Kisha Manase akafahamu kwamba Yahwe alikuwa Mungu.
14Baada ya hayo, manase akajenga ukuta wa nje ya mji wa Daudi, upande wa magharibi wa Gihoni, katika bonde, hadi kwenye lango la Samaki. Akauzungushia mlima wa Ofeli na akaupandisha ukuta hadi usawa mrefu sana. Akaweka maamri jeshi jasiri katika ngome zote za miji ya Yuda.
15Akaipeleka mbali miungu yote ya kigeni, akaondoa sanamu zote kwenye nyumba ya Yahwe, na madhabahu zote ambazo alikuwa amejenga juu ya mlima wa nyumba ya Yahwe na katika Yerusalemu, na kuvitupa nje ya mji.
16Akaijenga tena madhabahu ya Yahwe na juu yake akatoa sadaka za amani na sadaka za shukrani; akamwamuru Yuda amtumikie Yahwe, Mungu wa Israeli.
17Hata hivyo watu bado walitoa sadaka mahali pa sehemu za juu, lakini kwa Yahwe, Mungu wao pekee.
18Katika mambo mengine kuhusu Manase, maombi yake kwa Mungu wake, na maneno ya waonaji ambao walisema kwake katika jina la Yahwe, Mungu wa Israeli, tazama, yameandikwa miongoni mwa matendo ya wafalme wa Israeli.

19Katika matukio hayo kuna historia ya maombi yake, na jinsi Mungu alivyoguswa na maomabi hayo. Pia kuna kumbu kumbu ya dhambi zake zote na makosa yake, na sehemu ambako alikuwa amejenga sehemu za juu na kuzisimamisha Maashera na sanamu za kuchonga, kambla ya kujinyenyekesha mwenyewe — na imeandikwa kuhusu hayo katika tarehe ya waonaji. (Maandishi ya kale yanasema hivi, “tarehe ya Hozai,” ambayo ni maandishi ya kifungu asili. Lakini matoleo mengi ya kisasa yamesahihisha na kusomeka “tarehe ya waonaj” Pia, matoleo machache ya kisasa yanasema “tarehe ya waonaji”.).
20Kwa hiyo Manase akalala na babu zake, na wakamzika katika nyumba yake mwenyewe. Amoni, mwaye, akawa mfalme katika nafasi yake.
21Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na mbili alipoanza kutawala; alitawala miaka miwili katika Yerusalemu.
22Akafanya yaliyokuwa uovu katika macho ya Yaahwe, kama Manase, baba yake, alivyofanya. Amoni alitoa sadaka katika sanamau zote za kuchonga ambazo alitengeneza Manase baba yake, na aliziabudu.
23Hakujinyenyekesha mbele za Yahwe, kama baba yake Manase alivyokuwa amefanya. Badala yake, Amoni huyu huyu alifanya makosa zaidi na zaidi.
24Watumishi wake wakapanga njama wa zidi yake na wakamua katika nyumba yake mwenyewe.
25Lakini watu wa nchi wakawaua wote waliofanya njama zidi ya Mfalme Amoni, na wakamfanya Yosia, mwanaye, mfalme katika nafasi yake.