Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Nyakati

2 Nyakati 1

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Selemani mwana wa Daudi, aliimariswa katika utawala wake, na Yahwe Mungu wake alikuwa pamoja naye na alimpa nguvu nyingi sana.
2Sulemani akasema kwa Israleli wote, na maakida wa maelfu na wa mamia, na kwa waamuzi, na kwa kila mfalme kiongozi katika Israeli yote, wakuu wa kaya.
3Hivyo Sulemani na kusanyiko lote wakaenda pamoja naye sehemu ya juu iliyokuwa Gibeoni, maana ndipo palikuwepo hema ya kukutania ya Mungu, ambayo Musa mtumishi wa Yahwe, alikuwa ameitengeneza jangwani.
4Lakini Daudi alikuwa ameleta pale sanduku la Mungu kutoka Kiriath yeriam hadi sehemu ambayo alikuwa ametayarisha, maana alikuwa ameliandalia hema huko katika Yerusalemu.
5Zaidi ya hayo, madhabahu ya shaba iliyotengenezwa na Bezaleli mwana wa uri mwana wa Huri ilikuwepo huko kabla ya mbele ya madhabahu ya Yahwe; Sulemani na kusanyiko wakaenda ilikokuwa. (Maandiko ya zamani yanasema
6Selemani akaenda huko kwenye kwenye madhabahu ya shaba mbele za Yahwe, ambayo ilikuwepo mahali pa hema ya kukutamia, na akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu yake.
7Mungu akamtokea Selemani usiku huo na akasema kwake, “Omba! Nikupe nini?”
8Selemani akasema kwa Mungu, “Umeonesha agano la uaminifu mkuu kwa Daudi baba yangu, na umenifanya mfalme katika nafasi yaye.
9Sasa, Yahwe Mungu, ahadi yako kwa Daudi baba yangu itimie, maana umenifanya mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya dunia.
10Sasa nipe hekima na maarifa, ili niweze kuwaongoza watu hawa, maana ni nani anayeweza kuwaamua watu wako, ambao ni wengi sana kwa idadi?”
11Mungu akasema kwa Selemani, “Kwa kuwa hili lilikuwa kwenye moyo wako, na kwa kuwa hujaomba mali, utajiri, au heshima, wala maisha ya wale wanaokuchukia, wala maish marefu kwa jili yako binafsi, lakini umeomba hekima na maarifa kwa ajili yako, ili uwatawale watu wangu, ambao juu yao nimekufanya mfame, na hivi ndivyo nitafanya.
12Sasa nitakupa hekima na maarifa, pia nitakupa mali na utajiri, na heshima, kuliko wafalme wote waliokuwepo kabla yako walivyokuwa, na baada yako hakuna yeyote atakayekuwa navyo.”
13Kwa hiyo Selemani akaenda Yerusalemu kutoka sehemu ya juu iliyokuwepo Gibeoni, kutoka mbele ya hema ya kukutania; akatawala juu ya Israeli.
14Selemani akakusanya magari na wanaume waendesha farasi, naye alikuwa na magari 1, 400 na waendesha farasi kumi na mbili elfu ambao aliwaweka katika miji ya magari, pamoja naye, mfalme katika Yerusalemu.
15Mfalme akatengeneza fedha na dhahabu kuwa vitu vya kawaida kama mawe katika Yerusalemu, na mbao za mierezi kuwa kama miti ya mikuyu iliyomo katika nyanda za chini.
16Selemani katika uagizaji wa farasi kutoka Misiri, wafanya biashara wake walinunua farasi kutoka Misiri kwa bei stahiki.
17Waliagiza gari kutoka Misiri kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi mmoja kwa shekeli 150. Pia walinunua kutoka kwa wafalme wa Wahiti na wafalme wa Washamu.