Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Nyakati

2 Nyakati 20

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ikawa baada ya hayo, kwamba watu wa Moabu na Amoni, na pamoja na baadhi ya Wameuni wakaja juu ya Yehoshafati ili kupigana vita. (Mandishi, “baadhi ya Wameuni” yanatoa masahihisho kwa ajili ya maandishi ya Kiebrania, ambayo yanasomeka, “baadhi ya Waamoni”. Inadhaniwa kwamba “Wameuni” ndilo neno la asili, na wenye kunukuu walilibadili kuwa “baadhi ya Waamoni”. Lakaini jina hili la mwisho halileti maana, kwa sababu Waamoni tayari wamekwisha tajwa katika mstri huu. Vile vile, matoleo tofauti tofauti yanajihusha na tatizo hili katika namna mabli mbali)
2Kisha baadhi ya watu wakaja wakamwambia Yehoshafati, wakisema, “Umati mkubwa wanakuja juu yako ng'ambo ya Bahari iliyokufa, kutoka Edomu. Ona, wako Hason- tamari”, ambayo ndiyo En-gedi. (Badala ya “Edomu” baadhi ya matoleo ya zamani na ya kisasa yanasomeka, “Aramu.”
3Yehoshafati akaogopa na akajipanga kumtafuta Yahwe. Akatangaza haraka katika Yuda yote.
4Yuda wakakakusanyika pamoja kwa ajili ya kumtafuta Yahwe; wakaja kutoka miji yote ya Yuda kwa ajili ya kumtafauta Yahwe.
5Yehoshafati akasimama katika kusanyiko la Yuda na Yerusalemu, kwenye nyumba ya Yahwe, mbele ya kibaraza kipya.
6Akasema, “Yahwe, Mungu wa babau zetu, hauko mbinguni? Wewe siyo mtawala juu ya falame zote za mataiafa? Nguvu na uweza viko mkononi mwako, kwa hiyao hakuna anayeweza akukupinga wewe.
7Munagu wetu, Hukuwafuaakuja nje wakaaji wa nchi hii mbe ya watau watau wakop Israeli, na kuitoa milele kwa ajili ya uzaoa wa Abrahamu?
8Wakaishi ndani yake na kujenga sehemu takatifu kwa ajili ya jina lako, wakisema,
9'Ikiwa janga litakuja juu yetu —upanga, hukumu, au ugonjwa, au njaa—tutasimama mbele ya nyumba hii, na mbele zako (kwa maana jina lako limo ndani ya nyumba hii), na tutakulilia wewe katika mateso yetu, na utatusikia na kutuokoa.' (Badala ya “hukumu” baadhi ya maandiko ya zamani yanasema “mafuriko”).
10Tazama sasa, hapa kuna watu wa Amoni, Moabu, na wa Mlima Seiri ambao hukuwaacha Israeli wawapige waalipotoka nchi ya Misri; badala yake, Israeli waliwageukia mbali na hawakuwaangamiza.
11Ona jinsi wanavyotuzawadia; wanakuja kutotoa nje ya nchi yako mbayo umetupa kuirithi.
12Mungu wetu, hutawahukumu? Kwa maana hatuna nguvu dhidi ya hili jeshi kubwa ambalo linakuja juu yetu. hatujui cha kufanya, lakini macho yetu yako kwako.
13Yuda wote wakasimama mbele ya Yahwe, pamoja na wadogo wao, wake, na watoto.
14Kisha kati kati ya kusanyiko, roho ya Yahwe ikaja juu ya Yahazieli, mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, mwana, Mlawi, mmoja wa wana wa Asafu.
15Yahazieli akasema, “Sikilizeni, Yuda wote na ninyi wakaaji wa Yerusalemu, na Mfalme Yehoshafati. Hivi ndivyo Yahwe asemavyao kwenu, 'Msiogope: msivunjike moyo kwa sababu ya hili jeshsi kubwa, kwa maana vita siyo yenu, bali ni ya Mungu.
16Lazima muende chini juu ya yao kesho, Ona, wanakuja wakipanda kupia njia ya Sisi. Mtawakuta mwishono mwa bondo, mbele ya jangwa la Yerueli.
17Hamtahitaji kupigana katika vita hii. Simameni katika nafasi zenu, simameni wima, na muone wokovu wa Yahwe pamoja nanyi, Yuda na Yerusalemu. Msiogope wala kukata tamaa. Tokeni nje juu yao kesho, kwa maana yuko pamoja nanyi.”
18Yehoshafati akainamisha kichwa chake pamaoja na uso wake chini. Yuda wote na wakaaji wa Yerusalemu wakaanguka chini mbele za Yahwe, wakimwabudu yeye.

19Walawi, wale wa uzao wa Wakohathi na wa uzao wa Wakorahi, wakasimama juu kumsifu Yahwe, Mungu wa Israeli, kwa sauti kubwa sana.
20Asubuhi mapema wakasimama na kwenda nje kwenye bonde la Tekoa. Walipokuwa wakienda nje, Yehoshafati akasimama na kusema, “Nisikilizeni, Yuda, na nnyi wakaaji wa Yerusalemu! Aminini katika Yahwe Mungu wenu, na mtasaidiwa. Aminini katika manabii zake, na mtafanikiwa.
21Alipokuwa ameshauriana na watu, akawachagaua wale ambao wangemwimbia Yahwe na kumpa sifa kwa ajili ya utukufu wake mtakatifu, walipokuwa wakienda wakilitangulia jeshi, na kusema, “Mshukuruni Yahwe, kwa maana uaminifu wa aganao lake unadumu milele.”
22Walipoanza kuimba na kusifu, Yahwe akapanga wanaume katika mavamizi juu ya watu wa Amoni, Moabu, na wa Mlima Seiri, ambao walikuwa wanakauja dhidi ya Yuda. Walishindwa.
23Kwa maana watu wa Aamoni na Moabu walisimama kupigana na wakaaji wa Mlima Seiri, ili kuwaua kabisa na kuwangamiza. Waliapokuwa wamemaliza kuwaangamiza wakaaji wa Mlima Seiri, wote wakasaidiana kuangamizana kila mmoja.
24Yuda walipokuwa katika sehemu hiyo wakiangalia jangwani, waliangalia nje juu ya jeshi. Tazama, walikuwa wamekufa, wameanguka chini; hakuna aliyekuwa amepona.
25Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara kutoka kwa hao watu, walikuta miongoni mwao bidhaa nyingi, nguo, na johari za thamani, ambazo walizichukua kwa ajili yao wenyewe, nyingi kuliko uwezo wao wa kubeba. Iliwachukua siku tatu kusomba nyara hizo, zilikuwa nyingi sana. (Badala ya “miongoni mwao”, baadhi ya maandishi ya zamani na ya kisasa yanasema, “ng'ombe.” badala ya “nguo” baadhi ya maandiko ya kale na ya kisasa yanasema, “miili iliyokufa”).
26Katika siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka, Huko wakamsifu Yaahwe, kwa hiyo jina la sehemu hiyo hata leo ni “Bonde la Baraka”.
27Kisha, wakarudi, kila mtu wa Yuda na Yerusalemu, na Yehoshafati katika uongozi wao, kwenda tena Yerusalemu kwa furaha, kwa maana Yahwe alikuwa amewafanya wafurahie juu ya adui zao.
28Wakaja Yerusalemu na kwenye nyumba ya Yahwe kwa vinanda, vinubi na matarumbeta.
29Hofu ya Yahwe ikawa juu ya falme zote za mataifa waliposikia kwamba Yahwe amepigana dhidi ya adui wa Israeli.
30Kwa hiyo ufaleme wa Yehoshafati ulikuwa mtivu, kwa maana Mungu wake alimpa amani kuzungunga pande zake zote.
31Yehoshafati akatawala juu ya Yuda: Alikuwa na umri wa miaka thelathini na mitano alipoanza kutawala. Jina la mama yke aliitwa Azubahi, binti wa Shilhi.
32Akatembea katika njia za Asa, baba yake; hakugeka popote kuziacha; akafanya yaliyo mema katika macaho ya Yahwe.
33Vile vile, sehemu za juu hazikuwa zimeondoshwa mbali. Watu walikuwa bado hawajaelekeza mioyo yao kwa Mungu wa babu zao.
34Kwa mambo mengine kuhusu Yehoshafati, mwanzo na mwisho, tazama, yameandikwa katika historia ya kitabu cha wafalme wa Israeli.
35Baada ya hayo, Yehoshafati, mfalme wa Yuda, akapatana na Ahazia, mfalme wa Israeli, ambaye alitenda uovu mwingi.
36Akapatana naye kujenga meli za kwenda Tarshishi; Wakazijenga meli hizo huko Esion-geberi.

37Kisha Eliezeli, mwana wa Dadavahu wa Maresha, akatoa unabii juu ya Yehoshafati; akasema, “kwa sababu umepatana na Ahazia, Yahwe ameiharibu miradi yako.” Meli zilivunjika ili kwamba zisiweze kusafiri.