Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Nyakati

2 Nyakati 5

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Wakati ilipomalizika kazi aliyofanya Selemani kwa ajili ya Yahwe, Selemani akapeleka vitu ndani, ambavyo Daudi, baba yake, aliviweka wakifu kwa kusudi hilo, pamoja na zile fedha, dhahabu, na vyombo vyote akavileta ndani ya hazina ya nyumba ya Mungu.
2Kisha Selemanai akawakusanya wazee wa Israeli, wakuu wa makabila yote, na viongozi wa familia za watu wa Israeli, katika Yerusalemu, ili walilete sanduku la agano la Yahwe kutoka mji wa Daudi, ambao ni Sayuni.
3Wanaume wote wa Israeli wakakusanyika mbele za mfalme katika sikukuu, ambayo ilikuwa katika mwezi wa saba.
4Wazee wote wa Israeli wakaja, na Walawi wakalichukua sanduku.
5Wakalileta sanduku, hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote ambavyo vilikuwa ndani ya hema. Makuhani waliokuwa wa kabila la Lawi wakavileta vtu hivyo.
6Mfalme Selemanai na kusanyiko lote la Israeli wakaja pamoja, mbele ya sanduku, wakitoa sadaka za kondoo na maksai ambao hawakuweza kuhesabika.
7Makuhani wakalileta sanduku la anago la Yahwe ndani mahali pake, katika chumba cha ndani cha nyumba, kwenye patakatifu pa patakatifu, chini ya mabawa ya makerubi.
8Kwa kuwa makerubi walitandaza mabawa yao juu ya mahali pa sanduku, na walilifunika sanduku na na miti yake ya kulibebea.
9Miti ilikuwa mirefu sana kwamba ncha zake zlionekana kutoka ile sehemu takatifu mbele ya chumba cha andani, lakini hazikuweza kuonekana kutoka nje. Zipo hapo hadi leo.
10Hapakuwa na kitu katika sanaduku isipokuwa zile meza mbili ambazo Musa aliziweka humo huko Horebu, wakati Mungu alipofanya agano na watu wa Israeli, walipotoka nje ya Misri.
11Ilikuwa makuhani walipotoka nje ya sehemu takatifu. Makuhanai wote wliokuwepo wakajiweka wakifu wenyewe kwa Yahwe, bila kujiamuru wenyewe kulingana na sehemu zao.
12Pia makuhani waliokuwa waimbaji, wote kwa ujumla wao, pamoja na Asafu, Hemani, Yeduthuni, na wana wao na ndugu zao, wakiwa wamevalia kitani safi na wakipiga matoazi, vinanda, na vinubi, wakaasimama upande wa mashariki wa mwisho wa madhabahu. Pamoja nao palikuwa na makuhuni 120 wakipuliza tarumbeta.
13Ikawa kwamba wapuruza tarumbeta na waimbaji wakafanya mziki pamoja, wakifanya sauti moja isikike kwa ajili ya kumsifu na kumshukuru Yahwe. Walipaza sauti zao kwa tarumbeta, toazi na vyombo vingine, na wakamsifu Yahwe. Wakaimba, “Kwa maana Yeye ni mwema, kwa kuwa uaminifu wa agano lake wadumu milele.” Kisha nyumba, ile nyumba ya Yahwe, ikajawa na wingu.
14Makuhani hawakuweza kusimama ili wahudumu kwa sababu ya lile wingu, kwa maana utukufu wa Yahwe uliijaza nyumba yake.