Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Nyakati

2 Nyakati 2

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Sasa Selemani akaamuru kulijengea nyumba jina la Yahwe na nyumamba kwa ajili ya ikulu ya ufalme wake.
2Selemeni akateua wanaume elfu sabini wabebe mizigo, na wanaume elfu themanini wa kukata mbao katika mlima, na wanaume 3, 600 kwa ajili ya kusimamia.
3Selemani akatuma ujumbe kwa Hiramu, mfalme wa Tiro, ukisema, “Kama ulivyofanya na Daudi baba yangu, ulivyomtumia magogo ya mierezi ili ajenge nyumba ya kuishi, fanya hivyo hivyo na mimi.
4Tazama, niko karibu kujenga nyumba kwa ajili ya jina la Yahwe Mungu wangu, kuiweka wakifu kwake, kwa ajili ya kumtolea sadaka za kuteketezwa zenye viungo vitamu mbele zake, kwa ajili ya mkate wa uwepo, na kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa asubuhi na jioni, katika siku za Sabato na za mwezi mpya, na katika sikukuu zilizoteuliwa kwa ajili ya Yahwe Mungu wetu. Hii itakuwa milele, kwa Israeli.
5Nyumba nitakayoijenga itakuwa kubwa sana, maana Mungu wetu ni mkuu kuliko miungu mingine yote.
6Lakini ni nani anayeweza kumjengea Mungu nyumba, kama dunia yote na hata mbigu yenyewe haviwezi kumtosha? Mimi ni nani hata nimjengee nyumba, ispokuwa sadaka kwa ajili ya sadaka za kufukiza mbele zake?
7Kwa hiyo nileteeni mtu mwenye ujuzi wa kazi katika kazi ya dhahabu, fedha, shaba, na chuma, na ya dhambarau, na nyekundu, na sufu ya samawati, mtu anayejua kutengeza aina zote za mapambo ya mbao. Atakuwa na watu wenye ustadi waliopamoja nami katika Yuda na Yerusalemu, ambao Daudi baba yangu aliwaweka.
8Nitumieni pia mierezi, miberoshi, na miti ya msandali kutoka Lebanoni, maana najua ya kuwa watumishi wako wanajua jinsi ya kukata mbao katika Lebanoni. Angalia, watumishi wangu watakuwa na watumishi wako,
9ili kwamba watayarishe mbao nyingi kwa ajili yangu, maana nyumba ninayotaka kuijenga itakuwa kubwa na ya ajabu.
10Angalia, nitawapa watumishi wako, watu watakaozikata mbao, kori ishirini elfu za ngano ya aridhini, kori ishirini elfu za shayiri, bathi ishirini elfu za mvinyo, na bathi ishirini elfu za mafuta.” (Maandishsi ya kale yanasema: “kori ishirini elfu za ngano kama chakula”).
11Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akajibu kwa maandishi, ambayo alimtumia Selemani: “Kwa kuwa Yahwe anawapenda watu wake, amekufanya kuwa mfalme juu yao.”
12Zaidi ya hayo, Hiramu akasema, “Abarikiwe Yahwe, Mungu wa Israeli, aliyeziumba mbingu na dunia, amempa Daudi mwana mwenye hekima, mwenye karama ya busara na uelewa, ambaye atajenga nyumba kwa aajili ya Yahwe, na nyumba kwa ajili ya ufalme wake.
13Sasa nimemtum mtu mwenye ujuzi, mwenye karama ya uelewa, Hiramu, mtaalamu wangu.
14Ni mwana wa mwanamke wa binti za Dani. Baba yake alikuwa mtu kutoka Tiro. Ana ujuzi katika kazi za dhahabu, fedha, shaba, chuma, mawe, na katika mbao, na katika dhambarau, samawati, na sufu yenkundu, na kitani safi. Pia ana ujuzi katika kutengeneza michoro ya aina yoyote na katika kubuni kitu chochote. Apatiwe nafsi miongoni mwa watumishi wako wenye ujuzi, na pamoja na wale wa bwana wangu, Daudi, baba yako.
15Sasa, ngano na shayiri, mafuta na mvinyo, ambayo bwana wangu aliisema, na apeleke sasa vitu hivi kwa watumishi wake.
16Tutakata mbao kutoka Lebanoni, mbao nyingi kadri unavyohitaji. Tutazileta kwako kama mitumbwi kupitia bahari kwenda Yafa, na utazibeba hadi Yerusalemu.”
17Selemani akawahesabu watu wageni waliokuwa katika nchi ya Israeli, kwa kutumia njia ya Daudi, baba yake, aliyoitumia kuwahesabu. Walikutwa wako 153, 600.
18Miongoni mwao aliwateua sabini elfu ili wabebe mizigo, themanini elfu kuwa wakataji wa mbao katika milima, na 3, 600 kuwa wasimamizi wa kuwasimamia watu wafanye kazi.