Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Nyakati

2 Nyakati 4

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Vivile akatengeneza madhabahu ya shaba; urefu wake ulikuwa mikono ishirini, na upana wake ulikuwa mikono ishirini.
2Pia akatengeneza bahari ya mduara ya chuma cha kuyeyushwa, mikono kumi kutoka ukingo hadi ukingo. Urefu wake kwenda juu ulikuwa mikono mitano, na bahari ilikuwa na mzunguko wa mikono thelatinini.
3Chini ya kingo kuzunguka bahari kulikuwapo ng'ombe dume, kumi kila mkono,
4Bahari ilisimama juu ya ng'ombe wa kulima kumi na wawili, watatu wakiangalia kaskazini, watatu wakiangalia magharibi, na watatu wakiangalia kusini, na watatu wakiangalia mashariki. Bahari iliwekwa juu yao, na robo ya sehemu zao za nyuma zote zilikuwa ndani.
5Bahari ilikuwa nene kama upana wa mkono, na ukingo wake ulikuwa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi. Bahari ilikuwa na mabafu elfu tatu ya maji.
6Pia akatengeneza birika kumi kwa ajili ya kuoshea vitu; tano akaziweka mkono wa kulia, na tano akaziweka kushoto; vifaa vilivyotumika katika kufanayia sadaka za kuteketezwa zilipaswa kuoshwa ndani ya hizo birika. Bahari, vilevile ilikuwa kwa ajili ya makauhani kuoga humo.
7Akatengeza vinara vya taa kumi vya dhahabu ambavyo vilitengenezwa kutokana na maelekezo ya jinsi vilivyopaswa kuwa; akaviweka hekaluni, vitanao mkno wa kulia, na vitano mkono wa kushoto.
8Akatengeneza meza kumi na kuziweka hekaluni, tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto. Akatengeneza birika mia moja za dhahabu.
9Zaidi ya hayo akatengeneza mahakama ya makuhani na mahakama kuu, na milangu kwa ajili ya mahakama, akaifunika milango yake kwa shaba.
10Akaiweka bahari upande wa kulia wa nyumba, masharika, ikielekea upande wa kusini.
11Huramu akayatengeza masufuria, majembe, na mabakuli ya kunyunyizia. Hivyo Huramu akamaliza kazi aliyofanya kwa ajili ya mfalme Selemani katika nyumba ya Mungu:
12zile nguzo mbili, taji mfano wa upinde zilizo kuwa juu ya zile nguzo mbili, na nyavu mbili za za mapambo zilizofunika zile taji mbili mfano wa upinde zilizokuwa juu ya zile nguzo.
13Alikuwa ametengeneza makomamanga mia nne kwa ajili ya zile nyavu za mapambo: safu mbili za makomamanga kwa kila wavu ili kufunika vimbe mbili zilizo kuwa juu ya nguzo.
14Pia akavitengeneza vitako na mabirika juu ya kitako,
15bahari moja na wale ng'ombe kumi na wawili chini yake,
16pia masufuria, majembe, nyuma za nyama, na vyombo vingine vyote. Huramu mtaalamu akavifanya kwa ajili ya Mfalme Selemani, kwa ajili ya nyumba ya Yahwe, vya shaba iliyong'arishwa.
17Mfalme alikuwa amevisubu katika uwanda wa Yordani, katika udongo wa mfinyanzi kati kati ya Sukothi na Sereda.
18Hivyo ndivyo Selemani alivyovitengeneza vyombo vyote kwa wingi; kwa kweli, uzito wa shaba haukuweza kujulikana.

19Selemani akazitengeza samani zote ambazo zilikuwa kwenye nyumba ya Mungu, pia madhabahu ya dhahabu, na meza ambazo juu yake mkate wa uwepo ulipaswa kuwekwa;
20vinara pamoja na taa zake, ambazo zilitengezwa ili kumulika mbele ya chumba cha ndani—hivi vilitengenezwa kwa dhahabu halisi;
21na maua, taa, na makoleo, ya dhahabu, dhahabu safi.
22Pia mikasi ya taa, na mabakuli, vijiko, na vikaango vya sadaka za kuteketezwa vyote vilitengenezwa kwa dhahabu safi. Kuhusu mlanago wa kuingilia kwenye nyumba, milango yake ya ndani kwenye patakatifu pa patakatifu na milango ya nyumba, ambayo ni, ya hekalu, ilitengenezwa kwa dhahabu.