Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Nyakati

2 Nyakati 15

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Roho ya Mungu ikaja juu ya Azaria mwana wa Odedi.
2Akaenda nje kukutana na Asa na akamwambia, “Nisikilize, Asa, na Yuda wote na Benyamini: Yahwe yuko pamoja nanyi, pale mnapokuwa naye. Kama mtamtafuta, mtampata; lakini kama mtamsahau, atawasahau ninyi.
3Sasa kwa muda mrefu, Israeli hawakuwa na Mungu wa kweli, bila kuhani wa kufundisha, na bila sheria.
4Lakini katika dhiki yao wakamrudia Yahwe, Mungu wa Israeli, na wakamtafuta, wakamta.
5Katika nyakati hizo hapakuwa na amani kwake aliyesafiri kwend mbali, wala kwake aliyesafiri kuja hapa; badala yake shsida kubwa zilikuwa juu ya wenyeji wote wa wanchi.
6Waligawanyika vikundi vikundi, taifa dhidi ya taifa, na mji dhidi ya mji, kwa maana Mungu aliwapa shsida za kila aina ya kila mateso.
7Lakini muwe hodari, na msiuache mkono wenu kuwa dhaifu, kwa maana kazi yen itapewa thawabu.”
8Asa aliposikia maneno haya, unabii wa odedi nabii, akajipa ujasiri na kuviondosha mbali vitu vya kuchukiza kutoka nchi yote ya Yuda na Benyamini, na kutoka miji yote aliyokuwa ameiteka kuanzia kilima cha nchi ya Efraimu, na akaijenga tena madhabahu ya Yahwe, ambayo ilikuwa mbele ya ukumbi wa nyumba ya Yahwe.
9Akawakusanya Yuda wote na Benyamini, na wae waliokaa pamoja nao—watu wa kutoka Efraimu na Manase, na kutoka Simeoni. Kwa maana walikuja kwake katika hesabu kubwa kutoka Israeli, walipoona kwamba Yahwe Mungu wake alikuwa pamoja naye.
10Kwa hiyo wakakusanyika katika Yerusalemu katika mwezzi wa tatu, katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Asa.
11Katika siku hiyo walimtolea Yahwe dhabihu baadhi ya nyara ambazo walikuwa wameleta; ng'mbe wa kulima mia saba na kondoo na mbuzi elfu saba.
12Wakaingia kataika agano kwa ajili ya kumtafuta Yahwe, Mungu wa babau zao, kwa moyo wao wote na roho yao yote.
13Wakakubaliana kwamba yeyote atakepuuzia kumtafuta Yahwe, Mungu wa Israeli, atapaswa kuuawa, iwe mdogo ama mkubwa, iwe mwanaume ama mwanamke.
14Wakaapa kwa Yahwe kwa sauti kubwa, kwa kelele, na kwa sauti za tarumbeta na baragumu.
15Yuda wote wakakifurahia kile kiaapo. kwa maana walikuwa wameapa kwa moyo wao wote, na walimtafuta Mungu kwa nia yao yote, na walimuona. Yahwe akawapa amani pande zote.
16Pia akamwondoa Maaka, asiwe malikia, kwa sababu alikuwa amefanya sanamu ya kuchukiza ya Maashera. Asa akaivunja vunja sanamu ya kuchukiza, akaiweka kwenye mavumbi akaichoma moto huko kijitoni Kidroni.
17Lakini sehemu za juu hazikuwa zimeondolewa nje ya Israeli. Vile vile, Moyo wa Asa ulijitoa kikamilifu siku zake zote.
18Akaleta kwenye nyumba ya Mungu vitu vya baba yake na vitu vyake mwenyewe vilivyokuwa vya Yahwe: vitu vya fedha na dhahabu.

19Hapakuwa na vita zaidi hadi miaka thelathini na mitano ya utawala wa Asa.