Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 13

Yohana 13:4-14

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Basi, Yesu aliondoka mezani, akaweka kando vazi lake, akachukua kitambaa na kujifunga kiunoni.
5Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwaosha wanafunzi wake miguu na kuipangusa kwa kile kitambaa alichojifungia.
6Basi, akamfikia Simoni Petro; naye Petro akasema, “Bwana, wewe utaniosha miguu mimi?”
7Yesu akamjibu, “Huelewi sasa ninachofanya lakini utaelewa baadaye.”
8Petro akamwambia, “Wewe hutaniosha miguu kamwe!” Yesu akamjibu, “Nisipokuosha hutakuwa na uhusiano nami tena.”
9Simoni Petro akamwambia, “Bwana, nioshe, si miguu tu, bali na mikono yangu na kichwa pia.”
10Yesu akamwambia, “Aliyekwisha oga hana lazima ya kunawa isipokuwa miguu, maana amekwisha takata mwili wote. Ninyi mmetakata, lakini si nyote.”
11(Yesu alimjua yule ambaye atamsaliti, ndiyo maana alisema: “Ninyi mmetakata, lakini si nyote.”)
12Alipokwisha waosha miguu na kuvaa tena vazi lake, aliketi mezani, akawaambia, “Je, mmeelewa hayo niliyowatendeeni?
13Ninyi mwaniita Mwalimu na Bwana, nanyi mwasema vyema, kwa kuwa ndimi.
14Basi, ikiwa mimi niliye Bwana na Mwalimu, nimewaosha ninyi miguu, nanyi pia mnapaswa kuoshana miguu.

Read Yohana 13Yohana 13
Compare Yohana 13:4-14Yohana 13:4-14