Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Wafalme - 2 Wafalme 10

2 Wafalme 10:7-27

Help us?
Click on verse(s) to share them!
7Hivyo barua ilipokuja kwao, waliwachukua wana wa wafalme na kisha kuwaua, watu sabini, wakaweka vichwa vyao kwenye vikapu, na kuivituma kwa Yehu katika Yezreeli.
8Mjumbe mmoja akaja kwa Yehu, akisema, “Wamevileta vile vichwa vya watoto wa wafalme.” Hivyo akasema, viwekeni kwenye mafungu mawili kwenye lango hadi asubuhi.”
9Asubuhi Yehu akatoka nje na kusimama, na kusema kwa watu wote, “Ninyi hamna hatia. Tazameni, nimefanya fitina dhidi ya bwana wangu na kumuua, lakini ni nani aliyewaua hawa wote?
10Sasa hakika tafakarini kwamba hakuna sehemu ya neno la Yahwe, lile alilonena Yahwe kuhusu familia ya Ahabu, itaanguka kwenye aridhini, kwa kuwa Yahwe amefanya kile alichokiongea kupitia mtumishi wake Eliya.”
11Basi Yehu akawaua wote waliokuwa wamebakia wa familia ya Ahabu katika Yezreeli, na watu wake muhimu wote, marafiki zake wa karibu, na makuhani wake, hakuna hata mmoja wao alisalia.
12Kisha Yehu akainuka na kuondoka; akaenda Samaria. Kadiri alivyokuwa akikaribia Bethi Ekedi ya wachungaji,
13akamlaki na ndugu wa Ahazia mfalme wa Yuda. Yehu akawaambia, “Ninyi ni akina nani?” Wakajibu, “Sisi ni ndugu zake na Ahazia, na tunashuka chini kuwasalimia watoto wa mfalme na watoto wa Malkia Yezebeli.”
14Yehu akawaambia watu wake mwenyewe, “Wachukue wakiwa hai.” Hivyo wakawachukua wakiwa hai na kuwaua kwenye kisima cha Bethi Ekedi, watu wote arobaini na mbili. Hakumwacha hata mmoja wao akiwa hai.
15Baada ya Yehu kuondoka huko, akakutana na Yehonadabu mwana wa Rekabu anakuja kukutana naye. Yehu akamsalimia na kisha akamwambia, “Je moyo wako uko na mimi, kama moyo wangu ulivyo pamoja na wako?” Yehonadabu akajibu, Ndio.” Yehu akasema, “kama ni ndio, nipatie mkono wako.” Kisha Yehonadabu akampatia mkono wake, na Yehu akampandisha Yehonadabu juu kwenye magari ya farasi pamoja naye.
16Yehu akasema, “Fuatana pamoja nami na uone wivu wangu kwa Yahwe.” Hivyo alikuwa na Yehonadabu akiendesha gari la farasi.
17Wakati alipokuja Samaria, Yehu akawaua wote waliobakia kutoka uzao wa Ahabu katika Samaria, hata akawaangamiza ukoo wa kifalme wa Ahabu, kama walivyokuwa wameambiwa kabla ya neno la Yahwe, ambalo aliloambiwa Eliya.
18Kisha Yehu akawakusanya watu wote akwaambia, “Ahabu alimtumikia Baali kidogo, lakini Yehu atamtumikia sana.
19Basi niitieni manabii wote wa Baali, wote wamwabuduo, na makuhani wake wote. Asikosekane mtu hata mmoja, kwa kuwa nina dhabihu kubwa nataka kutoa kwa Baali. Yeyote atakayeshindwa kuja hataishi.” Lakini Yehu alifanya haya kwa udanganyifu, kwa dhamira ya kuwaua wanaomwabudu Baali.
20Yehu akasema, “Tengeni mda tuwe na mkutano kwa ajili ya Baali.” Hivyo wakalitangaza.
21Kisha Yehu akatuma Israeli yote na wamwabuduo Baali waje, hivyo basi hakuna mtu hata mmoja ambaye aliacha kuja. Walikuja kwenye hekalu la Baali, na ilijaa kutoka mwanzo hadi mwisho.
22Yehu akamwambia yule mtu aliyekuwa anatunza kabati la nguo za makuhani, “Uwatolee mavazi wote wamwabuduo Baali.” Basi yule mtu akawatolea nguo.
23Basi Yehu akaingia pamoja na Yohonadabu mwana wa Rekabu kwenye nyumba ya Baali, na kisha akawaambia wanaomwabudu Baali, “Tafuteni na muhahakishe kwamba hakuna mtu hapa pamoja na ninyi kutoka watumishi wa Yahwe, lakini wamwabuduo Baali peke yao.”
24Kisha wakaenda kutoa dhabihu na sadaka ya kutekeza. Basi Yehu alichagua watu themanini ambao walikuwa wamesimama nje, na aliwaambia, Kama mtu yeyote miongoni mwa hawa watu ambao nimewaleta kwenye mikono yenu atoroke, yeyote atakayemwacha huyo mtu atoroke, maisha yake yatachukuliwa kwa ajili ya yule aliyeokoka.”
25Hivyo kisha baada ya mda mfupi Yehu alipomaliza kutoa sadaka ya kutekezwa, akamwambia mlinzi na manahodha, “Ingieni na muwaue. Msimwache mtu yeyote atoke.” Basi waliwaua kwa makali ya upanga, na mlinzi na manahodha wakawatupa nje na kwenda kwenye chumba cha ndani cha nyumba ya Baali.
26Wakazitoa nguzo za mawe ambazo zilikuwa kwenye nyumba ya Baali, na kisha kuzichoma.
27Kisha wakazivunja zile nguzo za Baali, na kuiharibu nyumba ya Baali na kuifanya choo, ambacho kipo hadi leo.

Read 2 Wafalme 102 Wafalme 10
Compare 2 Wafalme 10:7-272 Wafalme 10:7-27