Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Wafalme

2 Wafalme 14

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Katika mwaka wa pili wa Yehoashi mwana wa Yehoazi, mfalme wa Israeli, Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, alianza kutawala.
2Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tanao wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa mda wa miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu.
3Mama yake alikuwa anaitwa Yehoyadani, wa Yerusalemu. Alifanya yale yaliyo mema usoni mwa macho ya Yahwe, sio kama baba yake Daudi. Alifanya kila kitu ambacho Yoashi, baba yake, alichukuwa amekifanya.
4Lakini sehemu ya juu haikuondolewa. Watu wakaendelea kutoa dhabihu na kufukiza ubani katika sehemu mahala pa juu.
5Ikawa mara utawala wake ulipokuwa imara, aliwaua watumishi ambao waliokuwa wamemuua baba yake, mfalme.
6Ila hakuwaweka watoto wa wale wauaji kwenye kifo; isipokuwa, alifanya kutokana na kile kilichokuwa kimeandikwa kwenye sheria, kwenye kitabu cha Musa, kama Yahwe alivyokuwa ameamuru, akisema, “Wababa wasife kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasife kwa ajili ya makosa ya wazazi wao. Isipokuwa, kila mtu atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.”
7Aliua maaskari elfu kumi wa Edomi kwenye bonde la chumvi; pia alimchukua Sela kwenye vita na kuiita Yoktheeli, ndivyo paitwavyo hadi leo.
8Kisha Amazia akatuma wajumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu mfalme wa Israeli, akisema, “Njoo, tuonane kila mmoja macho kwa macho kwenye mashinadano.”
9Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akawatuma wajumbe kurudi kwa Amazia mfalme wa Yuda, akisema, “Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma kwa mwerezi katika Lebanuni, kusema, 'Mpatie mwanangu binti yako amuoe; lakini hayawani aliyekuwako Lebanoni akaukanyaga chini ule mbaruti.
10Umempiga sana Edomu, na moyo wako umekuinua. Jisifu katika ushindi wako, lakini kaa nyumbani, kwa nini unataka kujisababishia mataizo na kuanguka, wote wewe na Yuda pamoja nawe?”
11Lakini Amazia hakutaka kusikia. Hivyo Yehoashi mfalme wa Israeli akakwea yeye na Amazia mfalme wa Yuda wakakutana uso kwa uso huko Beth Shemeshi, ambayo ilikuwa ya Yuda.
12Yuda walishindwa mbele ya Israeli, na kila mtu akakimbia nyumbani.
13Yehoashi mfalme wa Israeli, akamchukua Amazia, mfalme wa Yuda mwana wa Yehoashi mwana wa Ahazia, huko Beth Shemeshi. Akaja Yerusalemu na kuuangusha chini ukuta wa Yerusalemu kutoka lango la Efraimu mpaka kwenye pembe ya lango, urefu wa mbali wa dhiraa mia nne.
14Akachukua dhahabu na fedha zote, na vitu vyote ambavyo vilipatikana katika nyumba ya Yahwe, na vitu vya thamani kwenye nyumba ya mfalme, pamoja na mateka pia, na kurudi samaria.
15Kama ilivyo kwa mambo mengine yamhusuyo Yehoashi, yote aliyoyafanya, ushujaa wake, na jinsi alivyopigana na Amazia mfalme wa Yuda, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Israeli?
16Kisha Yehoashi akalala na wazee wake na ailizikwa katika Samaria pamoja na wafalme wa Israeli, na Yeroboamu, mwanaye, akawa mfalme katika eneo lake.
17Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, akaishi miaka kumi na tano baada ya Yehoashi mwana wa Yehoahazi, mfalme wa Israeli.
18Kama ilivyo kwa mambo mengine yanayomhusu Amazia, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Yuda?

19Wakafanya njama dhidi ya Amazia katika Yerusalimu, akakimbilia Lakishi. Akakimbia hadi Lakishi, lakini wakawatuma watu kumfuata hadi Lakishi na kumuua huko.
20Wakamrudisha kwa farasi, na alizikwa pamoja na wazee wake katika mji wa Saudi.
21Watu wote wa Yuda wakamchukua Uzaria, ambaye alikuwa na umri wa miaka kumi na minne, na walimfanya kuwa mfalme katika nyumba ya kifalme wa baba yake Uzaria.
22Alikuwa Uzaria ambaye alijenga Elathi na kuirudisha kwa Yuda, baada ya mfalme Uzaria akalala pamoja na mababu zake.
23Katika mwaka wa kumi na tano wa Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda, Yeroboamu mwana wa Yoashi mfalme wa Israeli alianza kutawala katika Samaria; alitawala kwa muda wa miaka arobaini na moja.
24Akafanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe. Hakuziacha dhambi zake za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye aliisababisha Israeli kuasi.
25Akairudisha mipaka ya Israeli kutoka Lebo Hamathi mpaka kwenye Bahari ya Araba, kufuata amri ya neno la Yahwe, Mungu wa Israeli, ambalo aliongea kupitia mtumishi wake Yona mwana wa Amitai, yule nabii, ambaye alitokea Gathi Heferi.
26Kwa kuwa Yahwe aliyaona mateso ya Israeli, ambayo yalikuwa makali kwa kila mmoja, wote mtumwa na asyemtumwa, na kwamba hapakuwa na ulinzi kwa ajili ya Israeli.
27Basi Yahwe akasema kwamba hatoweza kulifuta jina la Israeli chini ya mbingu; badala yake, aliwaokoa kwa mkono wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi.
28Kama ilivyo kwa mambo mengine yamhusuyo Yeroboamu, yote aliyoyafanya, ushujaa wake, jinsi alivyo pigana vita na kuipata tena Damaskasi na Hamathi, ambayo ilikuwa ya Yuda, kwa Israeli, je hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
29Yeroboamu akalala na mababu zake, pamoja na mfalme wa Israeli, na Zekaria mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.