1Katika mwaka wa kumi na moja wa Ahazi mfalme Yuda, utawala wa Hoshea mwana wa Elahi ulianza. Alitawala katika Samaria juu ya Israeli kwa muda wa miaka minane.
2Alifanya yaliyo maovu usoni pa Yahwe, ila sio kama waflme wa Israeli ambao ulikuwa kabla yake.
3Shalmanesa mfalme wa Ashuru akamshambulia, na Hoshea akawa mtumishi na kumletea kodi.
4Kisha mfalme wa Ashuru akaona kwamba Hoshea alikuwa na njama dhidi ya yake, kwa kuwa Hoshea aliwatuma wajumbe kwa So mfalme wa Misri; pia, hakumpatia kodi mfalme wa Ashuru, kama alivyofanya mwaka hadi mwaka.
5Basi mfalme wa Ashuru akamfunga akamtia kifungoni. Kisha mfalme wa Ashuru akaishambulia nchi yote, akaishambulia Samaria na kuizunguka kwa miaka mitatu.
6Katika mwaka wa tisa wa Hoshea, mfalme wa Ashuru akaichukua Samaria na akawapeleka Israeli hadi Ashuru. Akawaweka kwenye Hala, kwenye Habori Mto wa Gozani, na katika mji wa Wamedi.
7Utekwaji huu ulitokea kwa sababu wana wa Israeli walifanya dhambi dhidi ya Yahwe Mungu wao, ambaye aliwaleta kutoka nchi ya Misri, kutoka chini ya mkono wa Farao mfalme wa Misri. Watu walikuwa wakiabudu miungu mingine
8na kutembea katika matendo ya wamataifa ambao Yahwe aliwafukuza mbele ya watu wa Israeli, na katika matendo ya wafalme wa Israeli ambayo waliyokuwa wameyafanya.
9Wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo mabaya dhidi ya Yahwe Mungu wao. Wakajijengea mahala pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hadi mji wenye boma.
10Pia wakasimamisha nguzo za mawe na Ashera juu ya kila mlima chini ya kila mti mbichi.
11Huko wakafukiza ubani katika mahali pa juu pote, kama mataifa walivyokuwa wamefanya, ambao Yahwe aliwafukuza mbele yao. Waisraeli wakafanya mambo maovu ili kuchochea hasira ya Yahwe,
12wakaabudu sanamu, ambazo Yahwe alizokuwa amewaambia, “Msifanye jambo hili.”
13Bado Yahwe aliwashuhudia Israeli na Yuda kwa kila nabii na kila muonaji, kusema, “Geukeni kutoka nija zenu mbaya na kuzishika amri zangu na hukumu zangu, na kuwa makini kufuata ile sheria yote niliyowaamuru baba zenu, na ambayo niliwapelekea kwa watumishi wangu manabii.”
14Lakini hawakuweza kusikia; badala yake walikuwa wakaidi kama baba zao ambao hawakumwamini Yahwe Mungu wao.
15Walizikataa sheria zake na lile agano ambalo alilifanya pamoja na babu zao, na hilo agano wakakubaliana wapewe. Wakafuata mambo yao yasiyofaa na wakawa hawafai. Wakawafuata mataifa ya kipagani ambao waliwazunguka, ambao Yahwe alikuwa amewaamuru wasiige.
16Wakazipuuza amri zote za Yahwe Mungu wao. Wakatengeneza sanamu za kusubu za ndama wawili kuziabudu. Wakatengeza nguzo ya Ashera, na wakaziabudu nyota zote za mbinguni na Baali.
17Wakawatupia watoto wao wakike kwa wakiume kwenye moto, wakapiga ramli na uchawi, wakajiuza wenyewe kufanya yale ambayo yalikuwa maovu usoni pa Yahwe, na kuichochea hasira yake.
18Kwa hiyo Yahwe alikuwa na hasira na Israeli na kuwaondoa usoni mwake. Hakubakia mtu hata mmoja isipokuwa kabila la Yuda peke yake.
19Hata watu wa Yuda hawakushika amri za Yahwe Mungu wao, lakini badala yake walifuata mambo hayo hayo ya kipagani ambayo Israeli walifuata.
20Hivyo Yahwe akawakataa vizazi vyote vya Israeli; akawatesa na kuwatia kwenye mkono wa wale wenye kuwateka nyara, hadi atakapokuwa amewatupa usoni mwake.
21Akawatoa Israeli kutoka kwenye mstari wa kifalme wa Daudi, na wakamfanya Yeroboamu mwana wa Nabeti mfalme. Yeroboamu akawapeleka Israeli mbali kutoka kumfuata Yahwe na kuwafanya wafanye dhambi kubwa.
22Wana wa Israeli wakafuata dhambi zote za Yeroboamu na hawakujiepusha nazo,
23basi Yahwe akawaondoa Israeli kutoka usoni pake, kama alivyokuwa amesema kupitia watumishi wake wote manabii kwamba angeweza kufanya. Hivyo Israeli walichukuliwa kutoka nchi yao kwenda Ashuru, na iko hivyo hata leo.
24Mfalme wa Ashuru akawaleta watu kutoka Babeli na kutoka Kutha, na kutoka Ava, na kutoka Hamathi na Sefarvaimu, na kuwaweka katika mji wa Samaria na kuishi katika huo mji wake.
25Ikatokea wakati walipoanza kuishi huko hawakumcha Yahwe. Hivyo Yahwe akatuma simba miongoni mwao ambao waliwaua baadhi yao.
26Basi wakaongea na mfalme wa Ashuru, wakisema, “Wale mataifa uliowaamisha na kuwaweka kwenye miji ya Samaria hawayajui mambo wanayotakiwa kuyafanya kutokana na mungu wa nchi. Hivyo alikuwa amewatuma simba kwenda kwao, na, tazama, wale simba walikuwa wakiwauua watu huko kwa sababu hawakufahamu yale mambo waliyokuwa wanatakiwa kuyafanya kwa mungu wa nchi.”
27Kisha mfalme wa Ashuru akatoa amri, akisema, “Mchukueni mmoja wa makuhani hapo ambaye mmemleta kutoka huko, na mumwache aende na kuishi huko, na mumwache awafundishe mambo yanayotakiwa kwa mungu wa nchi.”
28Hivyo mmoja wa makuhani ambaye walimchukua kutoka Samaria akaja na kuishi katika Betheli; akawafundisha jinsi wavyotakiwa mcha Yahwe.
29Watu wa kila kabila wakajifanyia miungu yao wenyewe, na kuiweka mahala pa juu ambapo Wasamaria walifanya kila kabila katika mji ambako walipoishi.
30Watu wa Babeli wakatengeneza Sakoth Benithi; watu wa Sakoth wakatengeneza Nergali; watu wa Hamathi wakatengeza Ashima;
31Waavi wakatengeneza Nibhazi na Tartaki. Nao Wasefarvi wakwachoma watoto wao kwenye moto kwa Adrameleki na Anameleki, wale miungu wa Sefarvaimu.
32Pia wakamcha Yahwe, na kuwateua kutoka miongoni mwao makuhani wa mahali pa juu, ambao waliteketeza kwa ajili yao kwenye hekalun mahali pa juu.
33Wakamcha Yahwe na pia kuabudu miungu yao wenyewe, sawa sawa na tamaduni za mataifa kutoka miongoni mwao waliokuwa wamewachukua.
34Hadi siku hii ya leo wameshikilia tamaduni zao za zamani. Wala hawamwogopi Yahwe, wala hawazifuati sheria zake, torati, au amri ambazo Yahwe aliwapa watu wa Yakobo ambaye alemwita jina Israeli
35pamoja na ambao Yahwe alifanya agano nao na kuwaamuru, “Msiiche miungu mingine, wala kuisujudia, wala kuiabudu, wala kuitolea sadaka.
36Lakini Yahwe, ambaye aliwatoa kutoka nchi ya Misri kwa nguvu kubwa na mkono ulionyooshwa, yeye ndiye mnayetakiwa kumwabudu, yeye ndiye manayetakiwa kumsujudia, na yeye ndiye mnayetakiwa kumtolea sadaka.
37Na sheria na hukumu, na torati na amri ambazo alizoziandika kwa ajili yenu, mtazishika milele. Hivyo msiiche miungu mingine,
38na agano ambalo nimelifanya pamoja nanyi, hamtalisahau; wala kuicha miungu mingine.
39Lakini Yahwe Mungu wenu, ndiye ambaye mtakayemcha. Atawalinda mbali na nguvu ya maadui zenu,”
40Hawatasikia, kwasababu waliendelea kufanya yale waliyokuwa wameyafanya nyuma.
41Hivyo haya mataifa wakamcha Yahwe na pia wakaabudu sanamu zao za kuchonga, na watoto wao wakafanya hivyo hivyo na watoto wa watoto wao. Wakaendelea kufanya yale ambayo babu zao waliyoyafanya, hata leo.