Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Wafalme

2 Wafalme 4

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ndipo mke wa mmoja wa watoto wa manbii alipokuja kwa Elisha akilia, akisema, “Mtumishi wako mme wangu amukufa, na unajua kwamba mtumishi wako alikuwa anamcha Yahwe. Basi aliyemuwia amekuja kuwachukua watoto wangu wawili kwenda kuwa watumwa.”
2Hivyo Elisha akamwambia, “Nikusaidie nini? Niambie una nini kwenye nyumba yako?” Akamwambia “Mtumishi wako hana kitu kwenye nyumba, isipokuwa chupa ya mafuta.”
3Kisha Elisha akasema, “Nenda kaazime vyombo kwa majirani zako, vyombo vitupu. Azima vyombo vingi uwezavyo.
4Kisha lazima uende ndani na kujifungia mlango wewe na watoto wako, na kumiminia mafuta vyombo vyote; vile vilivyojaa ukavitenge.”
5Basi akamuacha Elisha na kujifungia mlango yeye na watoto wake. Wakavileta vile vyombo kwake, na akivijaza kwa mafuta.
6Ikawa vyombo vilipojaa, akamwambia mtoto wake, “Niletee chombo kingine.” Ila akamwambia, “Hakuna vyombo vingine.” Kisha mafuta yakakoma kutoka.
7Ndipo akaja na kumwambia mtu wa Mungu. Akasema, “Nenda kauze mafuta; lipa deni lako, na yatakayobaki waachie watoto wako.”
8Siku moja Elisha alitembea Shunemu ambapo mwanamke muhimu aliishi; alimsihi ale chakula pamoja naye. Ikawa alipopita mara nyingi, angeweza kusimama pale na kula.
9Huyo mwanamke akamwambia mme wake, “Ona, sasa nadhani kwamba huyu ni mtu mtakatifu wa Mungu ambaye hupita siku zote.
10Ngoja tutengeneze chumba kidogo kwenye paa kwa ajili ya Elisha, na tuweke kitanda juu ya hicho chumba, meza, na taa. Kisha atakapokuwa anakuja kwetu, atakuwa anakaa hapo.”
11Ikawa siku moja akaja tena kwamba Elisha akasimama pale, akakaa kwenye hicho chumba na kupumzika hapo.
12Elisha akamwambia Gehazi mtumishi wake, “Mwite huyu Mshunami.” Wakati alipomuita, alisimama mbele yake.
13Elisha akamwambia, “Mwambie, 'Umetusumbukia kwa kutujali. Nini kifanyike kwa ajili yako? Tunaweza kukuombea kwa mfalme au amri jeshi?”” Akajibu, “Ninaishi miongoni mwa watu wangu.”
14Kisha Elisha akajibu, “Tumfanyie nini kwa ajili yake, sasa?” Gehazi akajibu, “Kweli hana mtoto, na mume wake ni
15mzee.” Hivyo Elisha akajibu, “Mwite.” Wakati alipomuita, akasimama kwenye mlango.
16Elisha akasema, “Katika kipindi kama hiki mwakani, katika kipindi cha mwaka mmoja, utakuwa ukimkumbatia mtoto.” Akasema “Hapana, bwana wangu na mtu wa Mungu, usidanganye kwa mtumishi wako.”
17Lakini yule mwanamke akabeba mimba na kujifungua mtoto wakume kipindi hicho hicho katika mwaka uliofuata, kama Elisha alivyokuwa amemwambia.
18Wakati mtoto alipokuwa mkubwa, akaenda kwa baba yake siku moja, ambaye alikuwa na watu wanaovuna.

19Akamwambia baba yake, “Kichwa changu, kichwa changu.” Baba yake akamwambia mtumishi wake, “Mbebe mpeleke kwa mama yake.”
20Wakati mtumishi alipombeba kumrudisha kwa mama yake, yule mtoto alikaa kwenye magoti yake hadi mchana na baada ya hapo mtoto alikufa.
21Hivyo yule mwanamke akambeba na kumlaza kwenye kile kitanda cha mtu wa Mungu, akafunga mlango, na kutoka nje.
22Akamwita mume wake, na kusema, “Tafadhali nitumie mmoja wa watumishi wako na moja ya punda wako ili niweze kuwahi kwa mtu wa Mungu ili niweze kurudi.”
23Mume wake akasema, “Kwa nini unataka kwenda kwake leo? Sio mwezi mpya wala Sabato.” alijibu, “Itakuwa sawa.”
24Ndipo akatandika kwenye punda na kumwambia mtumishi wake, “Mwendeshe haraka; usinipunguzie mwendo hadi nitakapokwambia ufanye hivyo.”
25Hivyo alienda na kuja na mtu wa Mungu katika mlima Karmeli. Basi wakati mtu wa Mungu alipomuona kwa mbali, akamwambia Gehazi mtumishi wake, “Tazama, mwanamke Mshunami anakuja.
26Tafadhali mkimbilie na umwambie, 'Hamjambo kwako pamoja na mume wako na mtoto wako?” Akajibu, “Hawajambo.”
27Baada ya kufika kwa huyo mtu wa Mungu katika mlima, alimkumbatia miguu yake. Gehazi akaja karibu ili kumuondoa lakini mtu wa Mungu akasema, “Muache, kwa kuwa amefadhaika sana. na Yahwe amenificha tatizo kwangu, na hajanambia kitu.”
28Ndipo aksema, “Nilikuuliza mtoto wako, bwana wangu? Sikusema, 'Usinifiche'?
29Ndipo Elisha akamwambia Geahazi, “Vaa kwa ajili ya safari na uchukue fimbo yangu mkononi mwako. Nenda kwake. Kama ukimkuta mtu yeyote, usimsalimie, na kama mtu yeyote akikusalimia, usimjibu. Laza fimbo yangu kwenye uso wa mtoto.
30Lakini mama yake na huyo mtoto akasema, “Kama Yahwe aishivyo, na kama uishivyo, sintokuacha.” Hivyo Elisha akainuka na kumfuata.
31Gehazi akawatangulia na kulaza ile fimbo kwneye uso wa yule mtoto, lakini yule mtoto hakuongea wala kusikia. Hivyo baada ya hapo Gehazi akarudi kuonana na Elisha na kumwambia akisema, “Mtoto hakuamka.”
32Ndipo Elisha alipofika kwenye ile nyumba, yule mtoto alikuwa amekufa na alikuwa bado yupo kwenye kitanda.
33Hivyo Elisha aliingia ndani na kufunga malango yeye mwenyewe na yule mtoto na kuomba kwa Yahwe.
34Alipanda juu na kulala juu ya yule mtoto; aliweka mdomo wake kwenye mdomo wake, macho yake kweneye macho yake, na mikono yake kwenye mikono yake. Akajinyoosha yeye mwenyewe kwa yule kijna, na mwili wa yule mtoto ukaanza kupata joto.
35Baada ya hapo Elisha aliinuka na kuanza kutembea kuzunguka kile chumba na kurudi tena juu na kujinyoosha mwenyewe kwa yule kijana. Yule kijana alipiga chafya mara saba na kisha akafungua macho yake!
36Hivyo Elisha akamwita Gehazi na kumwambia, “Mwite yule Mshunami!” Hivyo akamwita, na wakati alipofika kwenye kile chumba, Elisha akasema, “Mchukue mtoto wako.”

37Kisha akainamisha uso wake chini kwenye miguu yake na kusujudu, na kisha kumchukua mtoto wake na kuondoka.
38Kisha Elisha akarudi tena Gilgali. Kulikuwa na njaa katika nchi, na wana wa manabii walikuwa wamekaa mbele yake. Akamwambia mtumishi wake, “Weka sufuria kubwa kwenye moto na pika kwa ajili ya watoto wa manabii.”
39Mmoja wao akaenda kwenye shamba kukusanya mboga mboga. Alikuta matango ya porini na kukusanya ya kutosha hadi alipojaza kwenye nguo yake. Walizikata na kuziweka kwenye sufuria, lakini hakujua zilikuwa za aina gani.
40Basi, wakawapakulia na kusambaziwa kwa watu kwa ajili ya kula. Baadae, kadiri walivyokuwa wakiendelea kula, walipiga kelele na kusema, “Mtu wa Mungu, kuna kifo kwenye sufuria!” Hivyo wasingeweza kula tena.
41Lakini Elisha akasema, “Late unga.” Alitupia kwenye sufuria na kusema, “Pakua kwa watu kwa ajili ya kula, kwa hiyo wanaweza kula.” Kisha hapakuwa kitu chochote kibaya kwenye ile sufuria.
42Akaja mtu kutoka Baal Shalisha kwa mtu wa Mungu na kumletea chakula cha kwanza cha mavuno yake mikate shirirni ya shayiri, na masuke mabichi kwenye gunia. Akasema, “Wape haya watu ili waweze kula.”
43Mtumishi wake akasema, “Je, niandae hii mbele ya watu mia moja?” Lakini Elisha akasema, “Wapeni hawa watu, ili waweze kula, kwa sabau Yahwe anasema, 'Watakula na kingine kitabaki.”'
44Basi mtumishi wake akawaandalia mbele yao; wakala, na kuacha kingine kimebaki, kama neno la Yahwe lilivyokuwa limesema.