Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Wafalme

2 Wafalme 16

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Katika mwaka wa kumi na saba wa Peka mwana wa Pemalia, Ahazi mwana wa Yothamu mfalme wa Yuda, akaanza kutawala.
2Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala, na alitawala kwa muda wa miaka kumi na sita katika Yerusalemu. Alifanya yasiyo haki usoni mwa Yahwe Mungu wake, kama Daudi babu yake.
3Badala yake, akatembea katika njia ya wafalme wa Israeli; hasa, akamuweka mwanaye kwenye moto kama sadaka ya kuteketeza, kufuatana na machukizo ya mataifa, ambayo Yahwe aliwafukuza wana wa Israeli.
4Akatoa sadaka na kuchoma ubani mahali pa juu, juu ya milima, na chini ya kila mti mbichi.
5Kisha Riseni, mfalme wa Shamu na Peka mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, wakaja mpaka Yerusalemu kuteka. Wakamzunguka Ahazi, lakini hawakuweza kumshinda.
6Katika kipindi hicho, Resini mfalme wa Shamu akamponya Elathi kwa Shamu na kuwapeleka watu wa Yuda nje ya Elathi. Kisha Washami wakaja kwa Elathi ambapo waliishi hadi leo.
7Hivyo Ahazi akatuma wajumbe kwenda kwa Tiglath Pileseri mfalme wa Ashuru, akisema, “Mimi ni mtumishi wako na mwanao. Panda juu na uniokoe kutoka kwenye mikononi ya mfalme wa Shamu na kutoka kwenye mkono wa mfalme wa Israeli, ambao wameniteka.”
8Hivyo Ahazi akachukua fedha na dhahabu iliyokuwa imepatikana katika nyumba ya Yahwe na mingoni mwa waweka hazina wa nyumba ya mfalme na kuituma kama zawadi kwa mfalme wa Ashuru.
9Kisha mfalme wa Ashuru akamsikiliza, na mfalme wa Ashuru akaenda juu dhidi ya Damaski, akaishinda na kuwabeba watu wake kama wafungwa hadi Kiri. Akamuua Resini pia yule mfalme wa Shamu.
10Mfalme Ahazi akaenda Dameski kuonana na Tiglath Pileseri mfalme wa Ashuru. akaiona mdhabahu huko Damski. Akampelekea Uria kuhani mfano wa ile madhabahu na mpangilio wake na mchoro kwa ustadi wote ulikuwa umehitajika.
11Hivyo Uria yule kuhani akajenga madhabahu kuwa kama mipango ambayo Mfalme Ahazi atakaporudi kutoka Damaski. Akaimaliza kabla mfalme Ahazi hajarudi kutoka Dameski.
12Kisha mfalme akaja kuto Dameski akaiona ile madhabahu; mfalme akaikaribia ile madhabahu na kutoa sadaka juu yake.
13Akatengeneza sadaka yake ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka, na kunyunyiza damu ya washirika wake sadaka juu ya madhabahu.
14Madhabahu ya shaba ambayo ilikuwa mbele ya Yahwe-akaileta kutoka mbele ya hekalu, kutoka kati ya madhabahu yake na hekalu la Yahwe na kuiweka upande wa kaskazini wa madhabahu yake.
15Kisha mfalme Ahazi akamwiamuru Uria kuhani, akisema, “Juu ya madhabahu kubwa teketeza sadaka ya kutekezwa ya asubuhi na sadaka ya kuteketezwa ya nafaka ya jioni, pamoja na sadaka ya watu wote wa nchi, na matoleo ya sadaka ya mazao na sadaka zao za kinywaji. Nyunyiza juu ya hiyo damu yote ya sadaka ya kuteketeza, na damu yote ya kuteketeza. Lakini ile madhabahu ya shaba itakuwa kwa ajili yangu ili niulize ushauri.”
16Uria kuhani akafanya kile ambacho Ahazi aliamuru.
17Kisha mfalme Ahazi akaondoa jopo na mabeseni vitako vinavyobebeka; pia akachukua bahari kutoka juu ya ng'ombe wa shaba ambayo ilikuwa chini ya hiyo na kuiweka juu ya sakafu ya mawe.
18Aliondoa njia iliyokuwa kwa ajili ya kuingia kwenye Sabato ambayo walikuwa wamejenga kwenye hekalu, wote pamoja na mahali pa kuingilia mfalme kwenye hekalu la Yahwe, kwasababu ya mfalme wa Ashuru.

19Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Ahazi na yale aliyoyafanya, je yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
20Ahazi alilala pamoja na babu zake na kuzikwa pamoja babu zake katika mji wa Daudi. Hezekia mtoto wake akawa mfalme katika mahala pake.