Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Wafalme

2 Wafalme 22

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yosia alikuwa na umri wa miaka minane wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa mda wa miaka thelathini na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Yedida (Alikuwa binti wa Adaye wa Bozkathi).
2Alifanya yale yaliyo mema usoni mwa Yahwe. Alitembea kwenye njia zote za Daudi babu yake, na hakugeuka wala upande wa kulia au kushoto.
3Ikawa kwamba katika mwaka wa kumi na nane mfalme Yosia, akamtuma Shafani mwana wa Azalia mwana wa Meshulamu, mwandishi, kwenye nyumba ya Yahwe, akisema,
4“Panda juu kwa Hilkia yule kuhani mkuu na mwambie ahesabu pesa ambazo zilizokuwa zimeletwa kwenye nyumba ya Yahwe, ambazo walinzi wa hekalu wamezikusanya kutoka kwa watu.
5Zigawanywe kwenye mikono ya wafanyakazi ambao ni wasimamizi wa nyumba ya Yahwe, na waache wawapatie wafanya kazi ambao wako kwenye nyumba ya Yahwe, ili waweze kutengeneza pale palipoharibika.
6Wapewe pesa maseremala, wajenzi, na waashi, na pia kununua mbao na kukata jiwe kukarabati nyumba ya Yahwe.”
7Lakini zile pesa hazikutakiwa kuhesabiwa wakati walipokuwa wanapewa, kwa sababu waliimudu ile kazi kwa uaminifu.
8Hilkia kuhani mkuu akamwambia Shafani yule mwandishi, “Nimekipata kitabu cha sheria katika nyumba ya Yahwe.” Basi Hilkia akampatia kile kitabu Shafani, na kukisoma.
9Shafani akaenda na kuchukua kile kitabu kwa mfalme, na pia kumjulisha, akisema, “Watumishi wako wamezitumia zile pesa ambazo zilizokuwa zimepatikana kwenye hekalu na zimegawiwa kwenye mikono ya wafanya kazi ambao husimamia kuangalia nyumba ya Yahwe.”
10Kisha Shafani yule mwandishi akamwambia mfalme, “Hilkia yule kuhani amenipatia kitabu.” Kisha Shafani akakisoma mbele ya mfalme.
11Ikawa kwamba wakati mfalme aliposikia maneno ya sheria, alichana nguo zake.
12Kisha mfalme akamwamuru Hilkia yule kuhani, Ahikamu mwana wa Shafani, Akbori mwana wa Mikaya, Shafani mwandishi, na Asaya, mtumishi wake mwenyewe, akisema,
13Nenda na ukaongee pamoja na Yahwe kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu na kwa Yuda yote, kwa sababu ya maneno ya hiki kitabu ambacho kilichopatikana. Kwa hasira kubwa ya Yahwe ambayo ametukasirikia dhidi yetu kwa sababu babu zetu hawakusikiliza maneno ya hiki kitabu hivyo kama kutii yote ambayo yalikuwa yameandikwa kuhusiana na sisi.
14Basi Hilkia yule kuhani, Ahikamu, Akbori, Shafani, na Asaya wakaenda kwa Hulda nabii wa kike, mke wa Shalumu mwana wa Tikva mwana wa Harhasi, mtunza kabati la nguo (aliishi katika Yerusalemu katika mtaa wa pili), na wakaongea pamoja naye.
15Akawaambia, “Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Israeli, asemavyo: 'Mwambie huyu mtu aliyekutuma kwangu,
16“Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: 'Tazama, nitaleta janga kwenye hii sehemu na juu ya wakaao hapa, kulingana na kila kitu kilichoandikwa kwenye kitabu ambacho mfalme wa Yuda alichokisoma.
17Kwa sababu wamenitelekeza na kufukiza ubani kwa miungu mingine, hivyo basi wanaweza kunichochea hasira pamoja na matendo yote waliyoyafanya-kwa hiyo hasira yangu ilikuwa inawaka dhidi ya hii sehemu, na haitazimika.”'
18Lakini kwa mfalme wa Yuda, aliye watuma kuuliza mapenzi ya Yahwe, hivi ndivyo mtakavyo mwambia: “Yahwe, Mungu wa Israeli asema hivi: Kuhusu yale maneno uliyoyasikia,

19kwa sababu moyo wako ulikuwa mlaini, na kwa sababu umejinyenyekesha mwenyewe mbele za Yahwe, wakati uliposikia nilichokisema dhidi ya hii sehemu na wenyeji wake, kwamba wanaweza kuwa wakiwa na laana, na kwasaabu ulizozirarua nguo zako na kulia mbele yangu, Nami pia nimekusikia-hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
20Tazama, nitakukusanya na babu zako, nawe utawekwa kaburini kwako kwa amani. Macho yako hayataona maafa yote ambayo nitayaleta kwenye hii sehemu.”’” Hivyo watu wakachukua ujumbe huu kuurudisha kwa mfalme.