Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Wafalme

2 Wafalme 15

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Katika mwaka wa ishirini na saba wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Azaria mwana wa Amazia mfalme wa Yuda akaanza kutawala.
2Azaria alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, na alitawala kwa mda wa miaka hamsini na mbili katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Yekolia, na alikuwa anatokea Yerusalemu.
3Alifanya yaliyo mema machoni pa Yahwe, kama baba yake Amazia alivyofanya.
4Lakini, mahali pa juu hapakuwa pameondolewa. Watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza ubani katika mahala pa juu.
5Yhawe akampiga mfalme hivyo basi akawa na ukoma mpaka siku ya kifo chake na alikaa kwenye nyumba ya pekee. Yothamu, mtoto wa mfalme, alikuwa juu ya watu na kuwaongoza watu wa nchi.
6Kama kwa mambo mengine yanayomhusu Azaria, yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
7Hivyo Azaria alilala pamoja na babu zake katika mji wa Daudi. Yothamu, mtoto wake, akawa mfalme katika mahala pake.
8Katika mwaka wa thelathini na nane mwaka wa Azaria mfalme wa Yuda, Zekaria mwana wa Yeroboamu akatawala juu ya Israeli katika Samaria kwa miezi sita.
9Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe, kama baba zake waliyoyafanya. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye alisababisha Israeli kuasi
10Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya njama dhidi ya Zekaria, akamshambulia katika Ibleamu, na kumuua. Kisha akawa mfalme katika mahala pake.
11Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Zekaria, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.
12Hili ndilo lililokuwa neno la Yahwe ambalo aliongea na Yehu, kusema, “Kizazi chako kitakaa katika kiti cha Israeli mpaka kizazi cha nne.” Hiyo ikatokea.
13Shalumu mwana wa Yabeshi akaanza kutawala katika mwaka wa thelathini na tisa wa Azaria mfalme wa Yuda, na kutawala kwa mwezi mmoja tu katika Samaria.
14Menahemu mwana wa Gadi akapanda kutoka Tirza kwenda Samaria. Akamshambulia Shalumu mwana wa Yabeshi hapo, katika Samria. Akamuua na kuwa mfalme katika mahali pake.
15Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Shalumu na njama aliyoifanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafle wa Israeli.
16Ndipo Menahemu akamshambulia Tifsa na wote waliokuwa pale, na mipaka yote kuzunguka Tizra, kwasababu hawakufungua kwenye mji. Hivyo akaushambulia, na akawapasua wanawake wajawazito wote katika hicho kijiji.
17Katika mwaka wa thelathini na tisa wa Ahazia mfalme wa Yuda, Menahemu mwana wa Gadi akaanza kutawala; alitawala kwa miaka kumi katika Samaria.
18Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe. Katika maisha yake yote, hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye alifanya Israeli kufanya dhambi.

19Kisha Pulu mfalme wa Ashuru akaja kinyume cha nchi, na Menahemu akampatia Pulu talanta elfu moja za fedha, hivyo msaada wa Pulu ungeweza kuwa na yeye kuimarisha utawala wa Israeli katika nchi yake.
20Menahemu akatoza hii pesa kutoka Israeli kwa kumtaka kila mtu tajiri alipe shekeli hamsini za fedha kwake kumpatia mfalme wa Ashura. Hivyo mfalme wa Ashuru akarudi na hakukaa pale katika ile nchi.
21Kama kwa mabo mengine yanayomuhusu Menahemu, na yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya waflme wa Israeli?
22Hivyo Menahemu akalala pamoja na babu zake, na Pekahia mtoto wake akawa mfalme katika mahala pake.
23Katika mwaka wa hamsini wa Azaria mfalme wa Yuda, Pekahia mwana wa Menahemu akaanza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala kwa muda wa miaka miwili.
24Alifanya yaliyo maovu usoni pa Yahwe. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambazo kwa hizo alisababisha Israeli kufanya dhambi.
25Pekahia alikuwa na afisa aliyekuwa anaitwa Peka mwana wa Remalia, ambaye alifanya njama dhidi yake. Pamoja na watu hamsini wa Gileadi, Peka akamuua Pekahia pamoja na Argobu na Arie katika Samaria, katika ngome ya nyumba ya mfalme. Peka akamuua alipomua Pekahia akawa mfalme katika mahala pake.
26Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Pekahia, yote aliyoyafanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.
27Katika mwaka wa hamsini na mbili wa Azia mfalme wa Yuda, Peka mwana wa Remalia akaanza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala miaka Ishirini.
28Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabati, ambaye alisababisha Israeli kufanya dhambi.
29Katika siku za Peka mfalme wa Israeli, Tiglath Pileseri mfalme wa Ashuru akaja na kuichukua Iyoni, Abel Beth Maaka, Yanoa, Kadeshi, Hazori, Gileadi, na nchi yote ya Naftali. Akawachukua hao watu hadi Ashuru.
30Hivyo Hoshea mwana wa Ela akafanya njama dhidi ya Peka mwana wa Remalia. Akaishambulia na kisha kumuua. Kisha akawa mfalme katika mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.
31Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Peka, yote aliyoyafanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.
32Katika mwaka wa pili wa Peka mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, Yothamu mwana wa Azaria, mfalme wa Yuda akaanza kutawala.
33Alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala; alitawala kwa muda wa miaka kumi na sita katika Yerusalimu. Mama yake alikuwa anaitwa Yerusha; alikuwa binti ya Sadoki.
34Yotahmu alifanya yaliyo sahihi usoni pa Yahwe. Alifuata mfano wa yote baba yake Azaria aliyofanya.
35Ila, mahali pa juu hapakuchukuliwa. Watu walikuwa wakitio sadaka na kufukiza ubani katika mahali pa juu. Yothamu akajenga lango la juu la nyumba ya Yahwe.
36Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yothamu, na yote aliyoyafanya, je yameandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?

37Katika zamani hizo Yahwe akaanza kumtuma dhidi ya Yuda Rezini mfalme wa Sahmu, na Peka mwana wa Remalia.
38Yothamu akalala pamoja na babu zake na akazikwa pamoja na babu zake katika mji wa Daudi, babu yake. Kisha Ahazi, mtoto wake, akwa mfalme katika mhali pake.