Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Wafalme

2 Wafalme 24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Katika siku za Yehoyakimu, Nebukadreza mfalme wa Babeli akaiteka Yuda; Yehoyakimu akawa mtumishi kwa muda wa miaka mitatu. Kisha Yehoyakimu akarudi na kuasi dhidi ya Nebukadreza.
2Yahwe akatuma vikosi vya Wakaldayo dhidi ya Yehoyakimu,, Washami, Wamoabu, na Waamoni; akawatuma dhidi ya Yuda kuiharibu. Hii ilikuwa ni kuthibitisha pamoja na neno la Yahwe ambalo aliloliongea kupitia watumishi wake manabii.
3Ilikuwa baada ya mda mfupi kwenye kinywa cha Yahwe kwamba hili likaja juu ya Yuda, kuwaondoa usoni mwa uso wake, kwa sabau ya dhambi za Manase, yote aliyoyafanya,
4na pia kwa sababu ya damu isiyokuwa na hatia aliyoimwaga, kwa kuijaza Yerusalemu kwa damu isiyokuwa na hatia. Yahwe hakuwa tayari kusamehe hilo.
5Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yehoyakimu, na yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
6Yehoyakimu akalala pamoja na wazee wake, na Yekonia mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.
7Mfalme wa Misri hakushambulia tena nje ya nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alakuwa amezishinda nchi zote ambazo zilikuwa zikitawaliwa na mfalme wa Misri, kutoka kwenye kitabu cha Misri mpaka Mto wa Frati.
8Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na nane alipoanza kutawala; alitawala Yerusalemu miezi mitatu. Mama yake alikuwa anaitwa Nehushta; alikuwa binti wa Elnathani wa Yerusalemu.
9Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe; alifanya yale yote ambayo baba yake aliyafanya.
10Katika kipindi hicho jeshi la Nebukadreza mfalme wa Babeli liliishambulia Yerusalemu na kuuzunguka mji.
11Nebukadreza mfalme wa Babeli akaja kwenye mji wakati maaskari wake walipokuwa wameuzunguka,
12na Yekonia mfalme wa Yuda akatoka nje kwenda kwa mfalme wa Babeli, yeye, mama yake, watumishi wake, watoto wake, na maafisa wake. Mfalme wa Babeli akamteka katika mwaka wa nane wa utawala wake.
13Nebukadreza akachukua kutoka pale vitu vyote vya thamani katika nyumba ya Yahwe, na walio katika nyumba ya kifalme. Akavikata vipande vipande vitu vyote vya dhahabu ambavyo Suleimani mfalme wa Israeli alivitengeneza katika hekalu la Yahwe, kama alivyokuwa amesema ingetokea.
14Akawachukua wote utumwani Yerusalemu, viongozi wote, na wapiganaji wote, mateka elfu kumi, na mafundi wote, na wafua vyuma. hakuna aliyekuwa amesalia isipokuwa watu maskini katika nchi.
15Nebukadreza akamchukua Yekonia utumwani Babeli, pia na mama yake na mfalme, wake, maafisa, na wakuu wa nchi. Akawachukua kwenda utumwani kutoka Yerusalemu mpaka Babeli.
16Wapiganaji wote, elfu saba kwa hesabu, na mafundi elfu moja na wafua vyuma, wote wanaostahili kumpiga- mfalme wa Babeli aliwaleta hawa watu kwenye utumwa Babeli.
17Mfalme wa Babeli akamfanya Matania, kaka yake na baba yake na Yehokimu, mfalme katika sehemu yake, na kubadilisha jina lake kuwa Sedekia.
18Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja wakati alipoanza kutawala; alitawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Hamutali; alikuwa binti wa Yeremia kutoka Libna.

19Alifanya yaliyo maovu machoni mwa Yahwe; aliyafanya yale yote ambayo Yehokimu aliyoyafanya.
20Kupitia hasira ya Yahwe, haya matukio yote yalitokea Yerusalemu na Yuda, hadi alipowaondoa kwenye uso wake. Kisha Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.