Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - 2 Wafalme

2 Wafalme 7

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Elisha akasema, “Sikiliza neno la Yahwe. Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: “Kesho mda kama huu kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, kwenye lango la Samaria.””
2Basi yule nahodha ambaye alikuwa akitegemea mkono wake amemjibu mtu wa Mungu, na kusema, “Ona, hata kama Yahwe ataweka madirisha mbinguni, je jambo hili linawezekana?” Elisha akajibu, “Ona, utaona ikitokea kwa macho yako mwenyewe, lakini hutakula chochote katika hilo.”
3Basi, kulikuwa na watu wanne wenye ukoma upande wa nje wa lango la mji. Wakaambizana kila mmoja, “Kwa nini tukae hapa hadi hapo tutakapokufa?
4Kama tukisema kwamba tutaenda kwenye ule mji, maana mjini kuna njaa, na tutakufa hapo. Lakini kama tukiendelea kukaa hapa, bado tutakufa. Sawa, njoni, twendeni kwenye lile jeshi la Washami. Kama wakitupa uhai, tutakuwa hai, na kama wakituua, tutakufa tu.”
5Hivyo wakaamka asubuhi kabla giza halijaisha kwenda kwenye kambi ya Washami; Wakati walipofika sehemu ya mwanzo wa kambi, hapakuwa na mtu hapo.
6Kwa kuwa Bwana alikuwa ameunda jeshi la Washami kusikia sauti ya magari ya farasi, na sauti za farasi-sauti za jeshi jingine kubwa, ndipo wakaambizana kila mmoja wao, “Yule mfalme wa Israeli amekodisha wafalme wa Wahiti na Wamisri waje wapigane dhidi yetu.”
7Hivyo wale maaskari wakaondoka kungali giza; waliacha mahema yao, punda zao, na kambi kama ilivyokuwa, na kukimbia kwa ajili ya maisha yao.
8Wakati wale watu wenye ukoma walipokuja sehemu ya mwisho wa kambi, wakaenda kwenye hema moja na kula na kunywa, na kubeba fedha na dhahabu na nguo, na kwenda na kuzificha. Wakarudi na kuingia kwenye hema nyingine na kubeba kutoka pale pia, na kwenda kuvificha.
9Basi, wakaambizana kila mmoja, “Hatufanyi sahihi. Siku hii ni siku ya habari njema, lakini tunanyamaza kimya kuhusu hili. Kama tukisubiri mpaka kutakapopambazuka, adhabu itakuwa juu yetu. Basi, njoni, twendeni na kuwaambia nyumba ya mfalme.”
10Kwa hiyo wakaenda na kuwaita mabawabu wa mji. Wakawaambia, wakisema, “Tumeenda kambi ya Washami, lakini hapakuwa na mtu pale, hakuna sauti ya mtu yeyote, lakini kulikuwa na farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na zile hema kama zilivyokuwa.”
11Ndipo mabawabu wakatoa habari, ndipo wakaambiwa ndani ya nyumba ya mfalme.
12Basi yule mfalme akainuka usiku nakusema kwa watumishi wake, “Nitawaambia sasa kile ambacho Washami walichotufanyia. Wanajua kwamba tunanjaa, hivyo wameondoka kwenye kambi kwenda kujificha kwenye mashamba. Wanasema, 'Wakati watakapotoka mjini, tutawakamata wakiwa hai, na kuingia mjini.”
13Mmoja wa wale watumishi wa mfalme akajibu na kusema, “Nakuomba, ngoja baadhi ya watu wachukue farasi watano wale waliosalia, ambao wamebaki kwenye mji. Wako kama mkutano wote wa Israeli waliobaki-wengi wamekufa; ngoja tuwatume na tuone.”
14Hivyo wakachukua magari mawili ya farasi pamoja na farasi, na mfalme akawatuma baada ya jeshi la Washami, akisema, “Enendeni mkaone.”
15Wakawafuata kwenda Yordani, na barabara zote zilikuwa zimejaa na vifaa ambavyo Washami walivitupa wapate kukimbia haraka. Kwa hiyo wale wajumbe wakarudi na kumwambia mfalme.
16Wale watu wakatoka nje na wakaziteka nyara zile kambi za Washami. Hivyo kipimo cha unga mzuri uliuzwa kwa shekeli moja, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli moja, kama vile ambavyo neno la Yahwe lilivyosema.
17Naye mfalme alimwagiza yule nahodha ambaye alitegemea mkono wake kuwa mkuu wa lango, na watu wakamkanyaga chini langoni. Alikufa kama mtu wa Mungu alivyosema, ambaye ameongea wakati yule mfalme alipomshukia.
18Basi ikatokea kama yule mtu wa Mungu alivyosema kwa mfalme akisema, “Mda kama huu kwenye lango la Samaria, vipimo viwili vya shayiri vitapatikana kwa shekeli, na kipimo cha unga mzuri kwa shekeli.”

19Yule nahodha alimjibu yule mtu wa Mungu na kusema, “Tazama, hata kama Yahwe angefanya madirisha mbinguni, je hiki kitu kingeweza kutokea” Elisha akasema, “Tazama, utaona kikitokea kwa macho yako mwenyewe, lakini hutakula chochote katika hicho.”
20Hivyo ndivyo haswa kilichompata, kwa kuwa watu wakamkanyaga kwenye lango, na kufa.