Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua

Yoshua 19

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Upigaji wa pili wa kura uliangukia kwa Simoni na waligawiwa kwa kila ukoo wao. Urithi wao ulikuwa katikati ya urithi ulikuwa ni mali ya kabila la Yuda.
2Urithi waliokuwa nao ni Beerisheba, Sheba, Molada,
3Hazari Shuali, Bala, Ezemu,
4Elitoladi, Bethuli na Horma.
5Simoni alikuwa pia na Ziklagi, Bethi Markabothi, Hazari Susa,
6Bethi Lebaothi, na Sharuheni. Kulikuwa na miji kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake. Vile vile
7Simoni alimiliki Aini, Rimon, Etheri, na Ashani. Hii ilikuwa ni miji minne pamoja na vijiji vyake.
8Miji hii pamoja na vijiji vilivyoizunguka hata kufika Baalathi Beeri (ambao ndio Rama katika Negevu). Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simoni, waliopewa kwa koo zao.
9Urithi wa kabila la Simoni ulikuwa sehemu ya himaya ya kabila la Yuda. Hii ni kwasababu nchi waliyopewa kabila la Yuda ilikuwa ni kubwa kwao, na hivyo kabila la Simoni lilipokea urithi wao kutoka katika sehemu yao ya katikati.
10Upigaji wa kura ya tatu uliangukia kwa kabila la Zabuloni, na walipewa kwa koo zao. Mpaka wa urithi wao ulianzia huko Saridi.
11Mpaka wao ulipanda upande wa magharibi kuelekea Marala na ukaigusa Dabeshethi, na kisha ukasonga kuelekea kijito kilichokuwa mkabala na Yokineamu.
12Kutoka Saridi mpaka ulizunguka upande wa mashariki kuelekea mashariki na ulienda hadi mpaka wa Kislothi Tabori. Kutoka hapo uliendelea hadi Daberathi na kisha ulipanda hata Yafia.
13Kutoka hapo ulipita katika upande wa mashariki mwa Gathi Heferi, na kisha ukafika Ethikazini, baadaye ulienda hadi Rimoni na kisha ukageuka kuelekea Nea.
14Mpaka ulizunguka kueleka kaskazini ukafika Hanathoni na ulikomea katika bonde la Ifta Eli.
15Mkoa huu ulijumuisha miji ya Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala, na Bethlehemu. Kulikuwa na miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.
16Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Zabuloni, waliopewa kwa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
17Upigaji kura wa nne uliangukia kwa Isakari, na waligawiwa kufuatana na koo zao.
18Eneo lao lilijumuisha Jezreelli, Kesuloothi, Shunemu,

19Hafaraimu, Shioni, na Anaharathi.
20Pia ilijumuisha miji ya Rabithi, Kishioni, Ebezi,
21Remethi, Enganimu, Enihada, na Bethipazezi.
22Mpaka wao ulifika Tabor, Shahazuma, na Bethi Shemeshi, na ukakomea katika Yordani. Ilikuwa ni miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.
23Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Isakari, na walipewa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
24Upigaji wa kura ya tano uliangukia kwa kabila la Asheri, na walipewa kwa koo zao.
25Eneo lao lilijumuisha miji ya Helikathi, Hali, Beteni, Akashafu,
26Alameleki, Amadi, na Mshali. Mpaka wa magharibi ulitanuka hadi Karmeli na Shihori Libnathi.
27Kisha ulizunguka upande wa mashariki kueleka Bethi Dagoni na ukaenda hadi Zabuloni, na kisha ukafika katika bonde la ifutaheli, upande wa kaskazini mwa Bethemeki na Neieli. Baadaye uliendelea mbele hata Kabuli kueleka upande wa Kaskazini.
28Na kisha ulienda hadi Ebroni, Rehobu, Hammoni, na Kana, hata kufika mji mkubwa wa Sidoni.
29Mpaka ulirudi nyuma kuelekea Rama, na kisha ukafika kwenye mji wa Tiro uliokuwa na ngome. Baada ya hapo mpaka ulizunguka kuelekea Hosa na ulikomea katika bahari, katika mkoa wa Akizibu,
30Umma, Afeki, na Rehobu. Kulikuwa na miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.
31Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Asheri, na waliopewa kwa koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
32Upigaji wa kura wa mara ya sita uliangukia kwa kabila la Nafutali, na walipewa kufuatana na koo zao.
33Mpaka wao ulianzia Helefu, kutoka katika mwaloni huko Zaananimu, ulipanda hadi Adaminekebu na Yabneeli, umbali kama Lakumu; na ulikomea katka Yordani.
34Mpaka ule ulizunguka upande wa magharibi kuelekea Aznothi Tabori na ulipanda hadi Hukoki; uligusa Zabuloni katika upande wa kusini, na ulifika hata Asheri katika upande wa magharibi, na Yuda katika upande wa mashariki huko katika mto Yordani.
35Miji yenye ngome ilikuwa ni Zidimu, Zeri, Hammathi, Rakathi, Kinnerethi,
36Adama, Rama, Hazori,

37Kedeshi, Edrei, na Eni Hazori.
38Pia kulikuwa na miji ya Yironi, Migdaleli, Horemu, Bethi Anathi, na Bethi Shemeshi. Kulikuwa na miji kumi na tisa, pamoja na vijiji vyake.
39Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Nafutali, na walipewa miji pamoja na vijiji vyake kufuatana na koo zao.
40Upigaji wa kura ya saba uliangukia kwa kabila la Dani, na walipewa kufuatana na koo zao.
41Eneo lao la urithi lilijumuisha miji ya Zora, Eshitaoli, Iri Shemeshi,
42Shaalabini, Aijaloni, na Ithila.
43Vile vile lilijumuisha miji ya Eloni, Timna, Ekroni,
44Eliteke, Gibethoni, Baalathi,
45Yehudi, Bene - Beraki, Gathi Rimoni,
46Me -Yarkoni, na Rakoni sambamba na eneo la karibu na Yopa.
47Ilitokea wakati mpaka wa kabila la Dani ulipowapotea, kabila la Dani waliishambulia Leshemu, wakapigana nao, na wakauteka. Waliua kila mtu kwa upanga, wakauchukua ukawa mali yao, na wakakaa ndani yake. Wakauita mji ule Dani jina la babu yao badala ya Leshemu.
48Huu ulikuwa urithi wa kabila la Dani, waliopewa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
49Walipomaliza kugawana urithi wa nchi, watu wa Israeli walimpa urithi Yoshua mwana wa Nuni kutoka miongoni mwao.
50Kwa amri ya Yahweh walimpatia mji wa Timnathi Sera ambao aliuomba, ulikuwa katika nchi ya milima ya Efraimu. Aliujenga mji na akaishi huko.
51Na huu ndio urithi ambao Eliazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa makabila ya familia za mababu zao miongoni mwa watu wa Israeli, waligawa kwa kupiga kura huko Shilo, mbele za Yahweh katika mlango wa hema la kukutania. Na hivyo wakamaliza kuigawa nchi.