Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Ezekieli

Ezekieli 20

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ikawa ikaja katika mwaka wa saba, siku ya kumi ya mwezi wa tano, wazee wa Israeli wakaja kumuuliza Yahwe na kuketi mbele yangu.
2Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
3“mwanadamu, tangaza kwa wazee wa Israeli na uwaambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Je! Mmekuja kuniuliza swali? Kama niishivyo, sitaulizwa swali na ninyi! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.'
4Je! Utawahukumu? Utamuhukumu, mwanadamu? Wajulishe kuhusu machukizo ya baba zao.
5Waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Katika siku niliyoichagua Israeli na kuinua mkono wangu kuapa kiapo kwa uzao wa nyumba ya Yakobo, na kufanya kujulikana mimi mwenyewe kwao katika nchi ya Misri, wakati nilipoinua mkono wangu kuapa kiapo kwao. Nalisema, “Mimi ni Yahwe Mungu wenu”-
6siku hiyo niliinua mkono wangu kuapa kiapo kwa ajili yao kwamba nitawatoa kutoka nchi ya Misri kwenye nchi ambayo niliyokuwa nimeichagua kwa umakini kwa ajili yao. Ilikuwa ikitiririka maziwa na asali; ilikuwa nzuri sana utukufu miongoni mwa nchi mbali mbali.
7Nikawaambia, “Kila mtu atupilie mabli mambo ya machukizo kutoka mbele ya macho yake na sanamu za Misri. Msijitie unajisi; mimi ni Yahwe Mungu wenu.”
8Lakini wameasi juu yangu hawakuwa tayari kunisikiliza. Kila mtu hakutupilia mbali mambo ya machukizo kutoka mbele ya macho yake wala kwa ajili ya sanamu za Misri, hivyo nikaona nimwage ghadhabu yangu juu yao kukamilisha hasira yangu miongoni mwao katikati ya nchi ya Misri.
9Nilifanya kwa ajili ya jina langu ili lisinajisiwe katika macho ya mataifa ambao walikaa pamoja nao. Nilijifanya mwenyewe kujulikana kwao, katika macho yao, kwa kuwatoa katika nchi ya Misri.
10Basi nikawatoa katika nchi ya Misri na kuwaleta kwenye jangwa.
11Kisha nikawapa amri zangu na kufanya maagizo yangu kujulikana kwao, kwa kila mwanadamu atakayezishika ataishi.
12Pia nikawapatia Sabato zangu kama ishara kati yangu na wao, ili wajue kwamba mimi ni Yahwe niwafanyao wawe watakatifu.
13Lakini nyumba ya Israeli imeasi dhidi yangu jangwani. Hawakuenenda katika amri zangu; badala yake, wameyakataa maagizo yangu, ambayo mwanadamu ataishi kama akiyatii. Wamezinajisi Sabato zangu sana, basi nikasema nitamwaga hasira yangu juu yao jangwani ili kuwamalliza.
14Lakini nilifanya kwa ajili ya jina langu hivyo lisinajisiwe katika macho ya mataifa, ambao niliwatoa mbele ya macho yao kutoka Misri.
15Basi mimi mwenyewe pia nimeinua mkono wangu kuapa kiapo kwao jangwani sitawarudisha kwenye nchi ile niliyokuwa naenda kuwapatia, nchi inayotiririkayo maziwa na asali, ambayo ilikuwa nzuri sana ambayo ni nzuri kati ya nchi zote.
16Nimeapa hivi kwa sababu walikataa maagizo yangu na kutotembea katika amri zangu, na wazikufuru Sabato zangu.
17Lakini jicho langu likawahurumia kutokana na uharibifu na sikuwaangamiza jangwani.
18Nikawaambia watoto wao jangwani, “Msitembee kutokana na amri za wazazi wenu; msiweke maagizo yao au kujinajisi wenyewe kwa sanamu.

19Mimi ni Yahwe Mungu wenu, tembeeni katika amri zangu; tunzeni maagizo yangu na kuyatii.
20Zitunzeni Sabato zangu takatifu ili kwamba zitakuwa ishara kati yangu na ninyi, hivyo basi mtajua yakwamba mimi ni Yahwe Mungu wenu.”
21Lakini watoto wao waliniasi. Hawakutembea kwenye sheria zangu au kushika maagizo yangu, ambazo mwanadamu ataishi kama akizitii. Wamezinajisi Sabato zangu, hivyo nimeamua kumwaga ghadhabu yangu juu yao kutimiza ghadhabu yangu dhidi yao katika jangwa.
22Lakini niliurudisha mkono wangu na kutenda kwa ajili ya jina langu, hivyo lisitiwe unajisi katika macho ya mataifa ambao mbele ya macho yao niliwatoa Waisraeli.
23Mimi mwenyewe pia nimeuinua mkono wangu kuapa juu yao jangwani, kwamba nitawatawanya kati ya maifa na kuwatawanya miongoni mwa nchi mabali mbali.
24Nimeamua kufanya hivi kwa kuwa hawakuzitii amri zangu, na tangu walipo zikataa sheria zangu na kuzinajisi Sabato zangu. Macho yao yalizitamani sanamu za baba zao.
25Kisha niliwapa amri ambazo hazikuwa nzuri, na maagizo ambayo hawakuweza kuishi kwayo.
26Nikawafanya unajisi kwa zawadi zao wakati walipofanya dhabihu za kila limbuko la tumbo la uzazi na kutupa kwenye moto. Nalifanya hivi ili kuwaogofya hivyo wangeweza kujua kwamba mimi ni Yahwe!'
27Kwa hiyo, mwanadamu, waambie nyumba ya Israeli na waambie, 'Bwana Yahwe asema hivi: Katika hili pia baba zenu walinikufuru wakati walipokuwa sio waaminifu kwangu.
28Wakati nilipowaleta kwenye nchi ambayo niliyokuwa nimewaapia kuwapatia, na kisha popote walipoona jiwe lolote refu na mti wenye majani, walitoa sadaka zao, walinikasirisha kwa sadaka zao, na huko pia walichoma ubani wao wa kunukia na kumwaga sadaka zao za kinywaji.
29Kisha nikawaambia, “Nini maana ya mahali palipoinuka ambapo mmeleta sadaka huko?” Hivyo jina lake linaitwa Bana hata leo.'
30Kwa hiyo waambie nyumba ya Israeli, 'Bwana Yahwe asema hivi: Je! Kwa nini unajinajisi mwenyewe kwa njia za baba zako? Kwahiyo kwa nini unatenda kama makahaba, kutafuta kwa ajili ya mambo ya machukizo?
31Kwa kuwa wakati mtoapo zawadi zenu na kuwaweka watoto wenu kwenye moto, siku hii mnajitia unajisi pamoja na sanamu zenu zote. Kwa hiyo kwa nini niwaache mniulize mimi, nyumba ya Israeli? Kama niishivyo-Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-Sitawaacha mniulize swali.
32Mawazo yanayoumbika kwenye moyo wako hayatatokea kamwe. Mmesema, “Ngoja tuwe kama mataifa mengine, kama koo za nchi nyingine waabuduo mti na jiwe.”
33Kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-Nitatawala hakika juu yenu kwa mkono wenye nguvu, mkono ulionyooshwa, na ghadhabu itakayomwagwa juu yenu.
34Nitawatoa kutoka kwa watu wengine na kuwakusanya kutoka kwenye nchi mlizotawanyika ndani mwao. Nitafanya hivi kwa mkono hodari na kwa ghadhabu iliyomwagika.
35Kisha nitawaleta kwenye jangwa la watu, na huko nitawahukumu uso kwa uso.
36Kama nilivyo wahukumu baba zenu katika jangwa la nchi ya Misri, hivyo pia nitawahukumu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.

37Nitawafanya mpite chini ya fimbo yangu, na nitawafanya kutii maagizo yangu ya agano.
38Nitawasafisha kutoka miongoni mwenu maasi na wale ambao walionichukiza. Nitawatoa kutoka nchi ambayo wanayoishi kama wageni, lakini hawataingia kwenye nchi ya Israeli. Kisha mtajua yakwamba mimi ni Yahwe.
39Basi kwenu, nyumba ya Israeli, Bwana Yahwe asema hivi: Kila mmoja wenu ataenda kwa sanamu zake mwenyewe. Muwaabudu kama mtakataa kunisikiliza, lakini hamtalikufuru tena jina langu takatifu kwa zawadi zenu na sanamu zenu.
40Kwa kuwa juu ya mlima wangu mtakatifu, juu ya kilele cha mlima wa Israeli-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-wote wa nyumba ya Israeli mtaniabudu huko katika nchi. Nitabarikiwa kwa kutaka sadaka zenu huko, na pia malimbuko yenu ya shukrani pamoja na vitu vyenu vyote vitakatifu.
41Nitawapokea kama harufu nzuri ya ubani wakati nitakapowatoa kutoka wale watu na kuwakusanya toka nchi ambazo mlizotawanyika. Nitajifunua mimi mwenyewe kama mtakatifu ndani yenu kwa ajili ya mataifa waone.
42Kisha, wakati nitakapowaleta katika nchi ya Israeli, kwenye nchi ambayo niliuinulia mkono wangu kuapa kuwapatia baba zenu, mtajua yakwamba mimi ni Yahwe.
43Kisha mtazikumbuka njia zenu mbaya huko, na matendo yenu yote machafu mliyoyafanya wenyewe, na mtajichukia wenyewe katika macho yenu kwa matendo yenu yote maovu mliyoyafanya.
44Hivyo mtajua kwamba mimi ni Yahwe nifanyapo haya kwenu kwa ajili ya jina langu, sio kwa njia zenu mbaya au matendo yenu mabovu, nyumba ya Israeli-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”'
45Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
46“Mwanadamu, weka uso wako kuelekea nchi za kusini, na kuongea juu ya kusini; tabiri juu ya msitu wa Negebu.
47Uuambie msitu wa Negebu, 'Hivi ndivyo Yahwe asemavyo-Bwana Yahwe asema hivi: Tazama, nitaweka moto ndani yako. Utakula kila mti mbichi na kila mti mkavu ndani yako. Miali ya moto haitazimika; na kila uso utokao kusini hata kaskazini utateketezwa kwa moto.
48Kisha watu wote wenye mwili watajua yakwamba mimi ni Yahwe nimeuwasha moto, na hautazimika.”'
49Kisha nimesema, Ee! Bwana Yahwe, Wananisema mimi, 'Je! yeye sio mwenye kusema mafumbo?”'