Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua - Yoshua 9

Yoshua 9:8-24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
8Wakamwambia Yoshua, “Sisi ni watumishi wako.” Yoshua akawauliza, “Ninyi ni akina nani? Mnatokea wapi?
9Wakamwambia, “Watumishi wako wamekuja hapa kutokea nchi ya mbali, kwasababu ya jina la Yahweh Mungu wako. Tumesikia habari kumhusu na kuhusu kila kitu alichokifanya Misri -
10na kila kitu alichokifanya kwa wafalme wawili wa Waamori katika upande mwingine wa Yordani - kwa mfalme Sihoni wa Heshiboni, na kwa Ogu wa Bashani aliyekuwa katika Ashitarothi.
11Wazee wetu na wenyeji wote wa nchi yetu walituambia,” Chukueni chakula mikononi mwenu kwa ajili ya safari. Nendeni mkakutane nao, na kisha muwambie, “Sisi ni watumishi wenu. Fanyeni agano pamoja nasi.”
12Huu ni mkate wetu, ulikuwa wa moto tulipouchukua kutoka katika nyumba zetu katika siku ile tulipotoka kuja kwenu. Lakini sasa, tazama, imekuwa kavu na yenye ukungu.
13Viriba hivi vilikuwa vipya tulipovijaza, na tazama, sasa vinavuja. Nguo zetu na viatu vyetu vimechakaa na kuwa vikuukuu kwasababu ya safari ndefu.”
14kwahiyo, Waisraeli wakatwaa sehemu ya vyakula vyao, lakini walifanya hivyo bila ya kumwuliza Yahweh ili awaongoze.
15Yoshua akafanya amani pamoja nao na kufanya agano pamoja nao ili waishi. Viongozi wa watu nao pia wakawaapia.
16Siku tatu baada ya Waisraeli kufanya agano pamoja nao, waligundua kuwa walikuwa ni majirani zao na ya kwamba waliishi karibu nao.
17Kisha watu wa Israeli walisafiri na kufika katika miji yao katika siku ya tatu. Miji yao ilikuwa Gibeoni, Kefira, Beerothi, na Kiriathi Yearimu.
18Watu wa Israeli wahakushambulia kwasababu viongozi wao walikuwa wamewaapia mbele za Yahweh, Mungu wa Israeli. Waisraeli wote walikuwa wananung'unika kinyume na viongozi wao.
19Lakini viongozi wote waliawaambia watu wote wa Israeli, “Tumeapa kwa Yahweh, Mungu wa Israeli kwa ajili yao, na sasa hatuwezi kuwadhuru.
20Hiki ndicho tutakachowafanyia: Tutawaacha waishi ili tuepuke ghadhabu ambayo yaweza kuja juu yetu kwasababu ya kiapo tulichowaapia.”
21Viongozi wakawaambia watu, “Waacheni waishi.” Hivyo Wagibeoni wakawa wakata kuni na wachota maji wa Waisraeli wote, kama vile viongozi walivyosema juu yao.
22Yoshua aliwaita na kuwaambia, “Kwanini mlitudanya wakati mliposema, “Tuko mbali sana nanyi' wakati mnaishi hapa hapa miongoni mwetu?
23Na kwasababu hii, mmelaaniwa na baadhi yenu mtakuwa watumwa siku zote, wenye kukata kuni na kuchota maji kwa ajli ya nyumba ya Mungu wangu.”
24Walimjibu Yoshua na kusema, “Ni kwasababu watumishi wako waliambiwa kwamba Yahweh Mungu wenu alimwagiza Musa mtumishi wake kuwapa ninyi nchi yote, na kuwateteza wenyeji wote wa nchi mbele yenu - hivyo tuliogopa kwasababu yenu kwa ajili ya maisha yetu. Ndio maana tulifanya jambo hili.

Read Yoshua 9Yoshua 9
Compare Yoshua 9:8-24Yoshua 9:8-24