Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 27

Mithali 27:1-12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Usijisifu kwa ajili ya kesho, maana hujui siku italeta nini.
2Mtu mwingine akusifu na wala si kinywa chako mwenyewe, mgeni na wala si midomo yako mwenyewe.
3Fikiria uzito wa jiwe na uzito wa mchanga- uchokozi wa mpumbavu ni mzito zaidi kuliko hivyo vyote.
4Kuna ukatili wenye ghadhabu kali na mafuriko ya hasira, lakini ni nani anayeweza kusimama mbele ya wivu?
5Ni bora karipio la wazi kuliko upendo uliofichwa.
6Mwaminifu ni jeraha zilizosababishwa na rafiki, lakini adui anaweza kukubusu kwa kuomba radhi mno.
7Mtu aliyekula na kushiba hulikataa hata sega la asali, bali kwa mtu mwenye njaa, kila kitu kichungu ni kitamu.
8Ndege anayezurura kutoka kwenye kiota chake ni kama mtu anayepotea sehemu ambayo anaishi.
9Pafumu na manukato huufanya moyo ufurahi, lakini utamu wa rafiki ni bora kuliko ushauri wake.
10Usimwache rafiki yako na rafiki wa baba yako, na usiende kwenye nyumba ya ndugu yako katika siku ya msiba wako. Ni bora rafiki ambaye yupo karibu kuliko ndugu ambaye yupo mbali.
11Mwanangu, uwe na busara, moyo wangu ufurahi; kisha nitamjibu yule anayenidhihaki.
12Mtu mwenye busara huiona taabu na kujificha mwenyewe, lakini mjinga huendelea mbele na kuteseka kwa ajili ya taabu.

Read Mithali 27Mithali 27
Compare Mithali 27:1-12Mithali 27:1-12