Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 7

Luka 7:5-29

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5kwa sababu analipenda taifa letu, na ndiye aliyejenga sinagogi kwa ajili yetu”.
6Yesu akaendelea na safari yake pamoja nao. lakini kabla hajaenda mbali na nyumba, afisa mmoja aliwatuma marafiki zake kuzungumza naye. “Bwana, usijichoshe mwenyewe kwa sababu mimi sistahili wewe kuingia kwenye dari yangu.
7Kwa sababu hii sikufikiria hata mimi mwenyewe kuwa ninafaa kuja kwako, lakini sema neno tu na mtumishi wangu atapona.
8Kwani mimi pia ni mtu niliyewekwa kwenye mamlaka na nina askari chini yangu. Husema kwa huyu “Nenda” na huenda, na kwa mwingine, “Njoo” naye huja, na kwa mtumishi wangu 'Fanya hiki', na yeye hufanya”.
9Yesu aliposikia haya alishangaa, na kuwageukia makutano waliokuwa wanamfuata na kusema.” Nawaambia, hata katika Israeli, sijawahi kuona mtu mwenye imani kuu kama huyu.
10Kisha wale waliokuwa wametumwa walirudi nyumbani na kumkuta mtumishi akiwa mzima.
11fulani baada ya haya, ilitokea kuwa Yesu alikuwa anasafiri kwenda mji ulioitwa Naini. wanafunzi wake wakaenda pamoja naye wakiambana na umati wa watu.
12Alipofika karibu na Lango la jiji tazama, mtu aliyekufa alikuwa amebebwa, na ni mtoto wa pekee kwa mama yake. aliyekuwa mjane, na umati wa wawakilishi kutoka kwenye jiji walikuwa pamoja naye.
13Alipomwona, Bwana akamsogelea kwa huruma kubwa sana juu yake na akamwambia, “Usilie”.
14Kisha akasogea mbele akaligusa jeneza ambalo walibebea mwili, na wale waliobeba wakasimama akasema “Kijana nasema amka”
15Mfu akainuka na kukaa chini na akaanza kuongea. Kisha Yesu akamkabidhi kwa mama yake.
16Kisha hofu ikawajaa wote. wakaendelea kumtukuza Mungu wakisema “Nabii mkuu ameinuliwa miongoni mwetu” na “Mungu amewaangalia watu wake”
17Hizi habari njema za Yesu zilienea Yudea yote na kwa mikoa yote ya jirani.
18Wanafunzi wa Yohana walimwamwambia mambo haya yote.
19Ndipo Yohana akawaita wawili wa wanafunzi wake na kuwatuma kwa Bwana kusema “Wewe ndiye yule ajaye, au kuna mtu mwingine tumtazamie?
20Walipofika karibu na Yesu hawa wakasema, “Yohana mbatizaji ametutuma kwako kusema, 'Wewe ni yule ajaye au kuna mtu mwingine tumtazamie?”
21kwa wakati huo aliowaponya watu wengi kutoka katika magonjwa na mateso, kutoka kwa roho wachafu, na kwa watu wenye upofu aliwapa kuona.
22Yesu akajibu na kusema kwao. “Baada ya kuwa mmekwenda mlikotoka mtamjulisha Yohana mlichokiona na kukisikia. Wenye upofu wanapokea kuona na viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na kuwa hai tena, masikini wanaambiwa habari njema.
23Na mtu ambaye hataacha kuniamini mimi kwa sababu ya matendo yangu amebarikiwa”.
24Baada ya wale waliotumwa na Yohana kurudi walikotoka, Yesu akaanza kusema kwa makutano juu ya Yohana, “Mlikwenda nje kuona nini, mwanzi ukiwa unatikiswa na upepo?
25lakini mlikwenda nje kuona nini, mtu aliyevaa vizuri? tazama watu wale wanaovaa mavazi ya kifalme na kuishi maisha ya starehe wako kwenye nafasi za wafalme.
26lakini mnakwenda nje kuona nini, Nabii? Ndiyo, ninasema kwenu na zaidi sana kuliko nabii.
27Huyu ndiye aliyeandikiwa, “Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya macho yenu, atakeyeandaa njia kwa ajili yangu,
28Nasema kwenu, kati ya wale waliozaliwa na mwanamke, hakuna mkuu kama Yohana, lakini mtu asiye muhimu sana atakayeishi na Mungu mahali alipo yeye, atakuwa mkuu kuliko Yohana.”
29Na watu wote waliposikia haya pamoja na watoza ushuru, walitangaza kuwa Mungu ni mwenye Haki. Walikuwepo kati yao wale waliobatizwa kwa ubatizo wa Yohana.

Read Luka 7Luka 7
Compare Luka 7:5-29Luka 7:5-29